Waziri wa Kilimo Mhe Japht Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya mfumo wa ununuzi wa mbolea kwa pamoja (BPS) kwa wenyeviti na mameneja wa vyama vikuu vya ushirika wa kahawa, tumbaku, chai, miwa na mazao mchangayiko yaliyofanyika Jijini dodoma novemba 05, 2019. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Waziri wa Kilimo Mhe Japht Hasunga (Mb) akiongoza kikao kazi wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya mfumo wa ununuzi wa mbolea kwa pamoja (BPS) kwa wenyeviti na mameneja wa vyama vikuu vya ushirika wa kahawa, tumbaku, chai, miwa na mazao mchangayiko yaliyofanyika Jijini dodoma novemba 05, 2019.Waziri wa Kilimo Mhe Japht Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya mfumo wa ununuzi wa mbolea kwa pamoja (BPS) kwa wenyeviti na mameneja wa vyama vikuu vya ushirika wa kahawa, tumbaku, chai, miwa na mazao mchangayiko yaliyofanyika Jijini dodoma novemba 05, 2019.
Waziri wa Kilimo Mhe Japht Hasunga (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na wenyeviti na mameneja wa vyama vikuu vya ushirika wa kahawa, tumbaku, chai, miwa na mazao mchangayiko wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya mfumo wa ununuzi wa mbolea kwa pamoja (BPS) kwa yaliyofanyika Jijini dodoma novemba 05, 2019.
Na
Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma
Pamoja
na Serikali kusisitiza wakulima kuvitumia Vyama vya Ushirika katika utatuzi wa
changamoto za kiuchumi na Kijamii, bado wanaushirika wameshindwa kubuni mfumo
madhubuti wa kuwaunganisha katika ununuzi wa Pembejeo ambazo zingewapa unafuu
wa gharama za uzalishaji pamoja na kwamba Sera ya Maendeleo ya Ushirika ya
mwaka 2002, kusisitiza kwamba Ushirika ni chombo pekee cha kumletea mwananchi
mnyonge maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
Waziri
wa Kilimo Mhe Japht Hasunga (Mb) ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa mafunzo
ya mfumo wa ununuzi wa mbolea kwa pamoja (BPS) kwa wenyeviti na mameneja wa
vyama vikuu vya ushirika wa kahawa, tumbaku, chai, miwa na mazao mchangayiko
iliyofanyika Jijini dodoma novemba 05, 2019
Alisema
kuwa pamoja na mafanikio ya Ushirika katika kutatua changamoto za kiuchumi za
wanachama wake na wakulima, bado kumekuwa na changamoto za kuwepo kwa gharama
kubwa za upatikanaji wa Pembejeo kutokana na Vyama vya Ushirika wa aina moja
kuwa na njia zake za kupata Pembejeo.
Hivyo,
ili kuondokana na gharama kubwa za upatikanaji wa mbolea na kuleta tija katika
uzalishaji, Serikali imeanzisha mfumo wa ununuzi wa mbolea kwa pamoja (BPS
– Bulk Procurement System)kupitia Kanuni za Ununuzi wa Mbolea kwa Pamoja (Fertilizer
(Bulk Procurement) Regulations, 2017).
Lengo
la mfumo huo ni ili wakulima wawezekunufaika na punguzo la bei litokanalo na
ununuzi na usafirishaji wa mbolea nyingi kwa wakati mmoja (Economies of
Scale).
Katika Mafunzo hayo Mhe Hasunga amewataka
washiriki hao kuagiza mbolea kupitia BPS, ambapo watatakiwa kupata mahitaji ya
jumla ikiwa ni pamoja na dhamana za Benki (Bank Guarantees) zinazowezesha
kupata mbolea na kulipia ndani ya siku 180 kwa tozo ndogo tu za benki za
asilimia 1 hadi 2 baada ya kufungua muamana (LC – Letter of Credit).
Pamoja na kwamba BPS inawalenga zaidi
wakulima, bado kuna changamoto ya wakulima wadogo kupitia Vyama vyao vya
Ushirika kutoshiriki katika BPS kwani tangu kuanza kwa BPS mwaka 2017, uagizaji
wa mbolea kupitia BPS umekuwa ukitumiwa na wafanyabiashara wakubwa peke yake
na, wanapoifikisha mbolea kwa wakulima na kuwakuta hawana fedha za kununua
mbolea, wakulima hao hulazimika kuwekewa dhamana za mikopo (Credit
Guarantees) na wanunuzi wa mazao na/au wenye viwanda vya mazao ya
kilimoili wapate mikopo ya Benki yenye riba kubwa (asilimia 15 – 20 ya fedha
iliyokopwa).
“Gharama
za usambazaji nchini ni kubwa sana ikilinganishwa na gharama za kuingiza mbolea
nchini. Jambo hili limekuwa likiwafanya wakulima wadogo wapate mbolea kwa bei
kubwa sana kutokana na faida kubwa za wafanyabiashara, riba za mabenki na
mifumo ya uingizaji wa mbolea nje ya BPS isiyo na uwazi na hivyo kufanya hata
bei ya mbolea kwa wakulima kuwa kubwa kuliko uhalisia wa gharama ” Alisisitiza
Mhe Hasunga
MBOLEA
YA UREA
Katika
zabuni ya uingizaji wa mbolea aina ya Urea kupitia BPS iliyofanyika Julai 04,
2019;bei ya mbolea katika chanzo ilikuwa US$ 275 na bei ya kusafirisha
baharini na bima ilikuwa US$ 29 kwa tani 1. Hii ilifanya gharama ya
kufikisha mfuko mmoja wa mbolea bandari ya DSM iwe Tshs 34,500/=. Kama
nilivyozungumza siku ya kutangaza bei elekezi kwa mbolea ya Urea, gharama ya
kutoa mfuko mmoja bandarini, kuufungasha, kuusafirisha hadi kwa mkulima na
faida za wafanyabiashara hadi Sumbawanga ni Tshs 22,500/=. Hii inafanya bei ya
mkulima wa Sumbawanga iwe Tshs 57,000/=.
Kwa
lugha nyingine, gharama ya kufikisha mbolea kwa mkulima ni asilimia 60 ya
gharama za kuufikisha mzigo bandari ya Dar es salaam (CIF). Ukubwa wa gharama
hizi umechangiwa sana na faida za wafanyabiashara (Tshs 6,700/= ambayo ni zaidi
ya mara mbili ya gharama za kusafirisha mzigo hadi bandari ya DSM). Gharama hii
ingeweza kuepukika kama vyama vya ushirika vingeagiza mbolea moja kwa moja kwa
kutumia dhamana za benki.
Gharama
zingine zinazochangia kwenye kuongezeka kwa bei ya mkulima ni kukosekana kwa
mfumo wa uratibu wa usaifirishaji wa mbolea kutoka DSM hadi kwa mkulima. Kwa
sasa mbolea husafirishwakwa kutumia mikangafu/malori yanayobeba mzigo mdogo wa
tani 30 kwa Tshs 5,500/= kwa km 1,000.Hii ni karibu mara mbili ya gharama za
kuusafirisha mfuko huo kutoka kwenye chanzo (Tshs 3,336/= kutoka Qatar ambayo
iko zaidi ya km 5,000 kutoka bandari ya DSM). Gharama hizi zingepungua endapo
usafiri wa Reli ungetumika.
Aidha,
kutokana na riba za Benki (asilimia 20 au Tshs 11,400/=), mkulima hulazimika
kulipa Tshs 68,400/=. Endapo vyama vya ushirika vitaingia katika BPS, gharama
hii itaepukika.
Pamoja
na kuepuka gharama za usafirishaji kwa kutumia mikangafu badala ya reli, faida
kubwa za wafanyabiashara na riba za mabenki, bei ya mbolea aina ya urea kwa
wakulima itashuka kwa takriban Tshs 8,000/= ikilinganishwa na bei elekezi
zilizopo.
MBOLEA
YA DAP
Waziri
Hasunga alisema kuwa Pamoja na kwamba, wakati wa ufunguaji wa zabuni kupitia
BPS uliofanyika Juni 21, 2019, bei ya mbolea ya kupandia (DAP) iilkuwa kubwa
sana katika soko la Dunia (US$ 350 - 380) na bei za mbolea aina za NPK ilikuwa
ndogo sana (US$ 265 – 300), bado mbolea za NPK hapa nchini zimekuwa na bei
kubwa sana ikilinganishwa na bei za mbolea aina DAP ambayo ni Tshs 58,000 hadi
60,000/= katika mikoa ambako tumbaku huzalishwa (Tabora, Katavi, Ruvuma na
Mbeya). Bei ya NPK ya tumbaku katika mikoa hiyo hiyo ni US$ 34.5 (Sawa na Tshs
79,400). Kwa vile wakulima hupewa kwa mikopo ya mabenki, hulipa fedha hizo
pamoja na riba (asilimia 7 – 10) na hivyo kufanya mkulima ainunue mbolea hiyo
kwa Tshs 85,700/=.
Ili
mfumo wa ununuzi wa mbolea kwa pamoja uweze kunufaisha wakulima wadogo kwa
kupunguza bei za mbolea kwa kadri inavyowezekana Waziri
Hasunga ameagiza Vyama vikuu vya ushirika kuratibu ukusanyaji wa mahitaji ya
mbolea kutoka kwenye vyama vya msingi (AMCOS) kwa wakati na kutathmini gharama
zitakazohitajika, Vyama vikuu vya ushirika vihakikishe kwamba vinatunza
kumbukumbu sahahi za mahesabu ili hati za ukomo zitolewe kwa wakati ili
kurahisisha upatikanaji wa dhamana za Benki.
Maagizo mengine ni pamoja na
Mrajis wa ushirika kusimamia mchakato mzima wa upatikanaji wa ukomo wa madeni
ili kurahisisha upatikanaji wa dhamana za Benki kwa wakati, wauzaji wa mbolea
kuwa mawakala wa vyama vya ushirika na/au viwanda (mahali inapohitajika) ili
kurahisha zoezi la utoaji wa mbolea bandarini na kuisambaza kwa wakulima, na
Mbolea zote zitasafirishwa nchini kwa pamoja (Bulk Domestic
Distribution)
Kadhalika
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga ameagiza Usafiri wa Reli utatumika badala
ya barabara. Kikotoo cha bei elekezi kimechukulia usafiri wa mikangafu (Trucks)
kwa Tshs 5,500 kwa km 1,000. Gharama hii inaweza kupungua endapo mbolea
itasafirishwa kwa reli kwa Tshs 4,160 (TRC) au Tshs 4,600 (TAZARA). Gharama hii
inaweza kupungua zaidi kama mbolea nyingi itasafirishwa kwa wakati mmoja.
MWISHO
No comments:
Post a Comment