Mwakilishi wa Katibu Tawala Mkoa
wa Mwanza ambaye ni Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na Uzalishaji Emil
Kasagara akifungua kikao kazi cha wadau wa maendeleo ya Wanawake na
Jinsia waliokutana na Wizara kujadili na kutoa maoni katika kuboresha
Sera ya Maendeleo ya Wanawake na Jinsia kwa mikoa ya Kanda ya Ziwa
mkoani Mwanza.
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya
Maendeleo ya Jinsia kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto Bi. Grace Mwangwa akitoa maneno ya awali kabla ya
ufunguzi wa kikao kazi cha wadau wa maendeleo ya Wanawake na Jinsia
waliokutana na Wizara kujadili na kutoa maoni katika kuboresha Sera ya
Maendeleo ya Wanawake na Jinsia kwa mikoa ya Kanda ya Ziwa mkoani
Mwanza.
Mshauri Elekezi Prof. Linah Mhando
akifafanua jambo kwa Wadau wa maendeleo ya Wanawake na Jinsia katika
kikao kilichowakutanisha na Wizara kujadili na kutoa maoni katika
kuboresha Sera ya Maendeleo ya Wanawake na Jinsia kwa mikoa ya Kanda ya
Ziwa mkoani Mwanza.
Wadau wa Maendeleo ya Wanawake na
Jinsia wakifuatilia majadiliano katika kikao kilichowakutanisha na
Wizara kujadili na kutoa maoni katika kuboresha Sera ya Maendeleo ya
Wanawake na Jinsia kwa mikoa ya Kanda ya Ziwa mkoani Mwanza.
Wadau wa Maendeleo ya Wanawake na
Jinsia wakifanya majadiliano katika kikao kilichowakutanisha na Wizara
kujadili na kutoa maoni katika kuboresha Sera ya Maendeleo ya Wanawake
na Jinsia kwa mikoa ya Kanda ya Ziwa mkoani Mwanza.
Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW
………….
Na Mwandishi Wetu Mwanza
Wizara ya Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imekutana na wadau wa maendeleo ya
wanawake na Jinsia kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa katika kufanya
tathimini ya Sera ya Maendeleo ya Wanawake na Jinsia ya mwaka 2000 na
Mkakati wa utekelezaji wa mwaka 2005 ili tathimini hiyo isaidie kufanya
mapitio na maboresho ya Sera itakayozingatia makubaliano ya mikataba
mbalimbali, Dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2025, Mpango wa pili wa Taifa
wa maendeleo wa miaka mitano.
Haya yameelezwa leo mkoani Mwanza
na Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Jinsia kutoka Wizara ya
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Grace Mwangwa
wakati wa ufunguzi wa kikao kazi kilichowakutanisha wadau wa maendeleo
ya wanawake na Jinsia kutoka mikoa ya Mwanza. Mara, Kagera, Geita,
Simiyu, Shinyanga na Kagera na Wizara.
Bi. Grace amesema Wizara ndio
yenye jukumu ya utekelzaji wa Msualaya jinsi nchini yanazingatiwa na
hivyo ili yaweze kutekelzwa yanahitaji kuwa na Sera na Mikakati ni
muhimu katika kuleta maendeleo ya wanawake na jinsia.
Amesisitiza kuwa madhumuni ya Sera
iliyopo yalikuwa ni kutoa mwelekeo ambao ungehakikisha kuwa mipango,
Mikakati na shughuli mbalimbali za uongozi na maendeleo katika kila
Sekta na Taasisi inazingatia usawa wa kijinsia.
Ameongeza kuwa lengo kuu la
kupitia Sera hiyo ni kuifanya iendane na wakati na iwezi kubeba
mabadiliko yaliyojitokeza katika miaka kumi na tisa tangu kuandaliwa
kwake mwaka 2000 ikiwemo changamoto katika utekelezaji wa Sera hii
ikiwemo mapungufu yake na nini kifanyike ili kuiboresha Sera ili
kueandana na wakati husika.
“Tunahitaji kupata maoni yenu
tunahitaji maelekezo yenu nini hakikuzingatiwa tunaomba maoni yenu ili
tuwe na Sera itakayosaidia maendelo ya Waanwake na Jinsia nchini
”Alisema Bi. Grace
Bi Grace ameongeza kuwa bali na
kukutana na wadau na kupata maoni pia watakutana na vikundi vya kijamii
na mwananchi mmoja mmjoja kwa kupita katika baadhi ya vijiji vya mikoa
ya Kanda ya Ziwa kwa kuwafuata walipo ili kuweza kupata maoni yao ili
kuweza kiboresha Sera hiyo.
Akifungua kikao kazi hicho kwa
niaba ya Katibu Tawala Mkoa wa Singida, Katibu Tawala Msaidizi Uchumi
na Uzalishaji Bw. Emil Kasagara amesema kuwa Kikao hicho kinatarajia
kufikia malengo ya kufanya tathmini ya utekelezaji wa masuala ya Usawa
wa Jinsia na Uwezeshaji Wanawake katika kufikia maendeleo jumuishi
hususan katika Sekta ya Afya, Elimu, Kilimo na Masuala ya kifedha,
uwezeshaji wa wanawake katika nafasi za uongozi na siasa, mazingira na
Uzazi na Afya ya Mtoto na kukusanya Taarifa na Takwimu zitakazowezesha
kuandaa Rasimu ya Sera ya Maendeleo ya Wanawake na Jinsia.
Ameongeza kuwa kikao kazi
hicho kitawezesha kukusanya maoni yatayowezesha kuwa na Sera Shirikishi
inayozingatia masuala yote muhimu na kupata uelewa wa pamoja kuhusu
wajibu wa Serikali na wadau katika uwepo wa Sera ya maendeleo ya
Wanawake na Jinsia .
“Natumai mtatumia muda huu
vizrui kujadiliana na kupata maoni yatakayowezesha kupata Sera mbayo
itakuwa imekidhi mahitaji ya wakati tulionao na hata kuhakisi
yatakayojitokeza hapo mbele” Alizema Bw. Kasagara
Mshauri Elekezi Prof. Linah
Mhando ameeleza maeneo yanayopewa kipaumbelekatika Sera mpya ni Jinsia
na maendeleo ya Mji/Vijiji, Jinsai na haki za umiliki ardhi, Jinsia,
maji na usafi wa mazingira, Haki za mtoto wa kike, Jinsia na ulemavu,
Ukatili wa Kijinsia,jinsia, sayansi ,teknolojia na ufumbuzi , Jinsia,
afya uzazi na Ukimwi, Jinsia, uongozi na maamuzi, Jinsia, ajira na kazi,
Jinsia, Sheraia na haki za binadamu na Jinsia na hifadhi ya jamii.
Ameyataja maeneo mengine kuwa
ni Jinsia na kuwawezesha wanawake kiuchumi, Jinsia na ujumuishwaji wa
kifedha, Jinsia na mabadiliko ya tabianchi,Jinsia na Nishati, Jinsia na
Miundombinu, Jinsia na Takwimu, Jinsia na Madini, Jinsia na vyombo vya
habari na Mawasiliano, Jinsia na Mila na Desturi, Jinsia na Jmii za
ufugaji, Ufadhili na Jinsia na Jinsia na uvuvi.
Wizara ya Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ipo katika machakato wa kukusanya maoni
kwa wadau kutoka Kanda saba za Tanzania Bara ili kuwezesha maboresho ya
Sera ya Maendeleo ya Wanawake na Jinsia ya Mwaka 2000.
No comments:
Post a Comment