Thursday, November 14, 2019

VIJIJI VYOTE VYA JIMBO LA MTERA KUWA NA UMEME IFIKAPO 2020-KALEMANI

Waziri wa Nishati Mhe.Dkt.Medard Kalemani pamoja na Mbunge wa jimbo la Mtera Mh. Livingstone Lusinde awakitia saini kwenye daftari la wageni leo walipokuwa wakiwasha umeme katika hospitali ya wilaya ya chamwino iliyojengwa kijiji cha Mlowa Barabarani iliyopo jijini Dodoma.
Afisa Tarafa ya Makanjwa Bi.Anifa Byemelwa,akimkarisha Waziri wa Nishati Mhe.Dkt.Medard Kalemani,ambaye leo ameweza kuwasha umeme katika hospitali ya wilaya ya chamwino iliyojengwa kijiji cha Mlowa Barabarani iliyopo jijini Dodoma.
Diwani Kata ya Mlowa Barabarani Bw.Allan Matewa,akizungumza mbele ya Waziri wa Nishati Mhe.Dkt.Medard Kalemani,ambaye leo amewasha umeme katika hospitali ya wilaya ya chamwino iliyojengwa kijiji cha Mlowa Barabarani iliyopo jijini Dodoma.
Meneja Tanesco wilaya ya Chamwino Bw.Baltazar Massawe,akitoa taarifa ya usambazaji umeme wilayani humo kwa Waziri wa Nishati Dkt.Medard Kalemani,alipokuwa ameenda kuwasha umeme katika hospitali ya wilaya ya chamwino iliyojengwa kijiji cha Mlowa Barabarani iliyopo jijini Dodoma.
Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Mhe.Vumilia Nyamoga,akizungumza  kabla ya kumkaribisha Waziri wa Nishati Mhe.Dkt.Medard Kalemani,ambaye amewasha umeme katika hospitali ya wilaya ya chamwino iliyojengwa kijiji cha Mlowa Barabarani iliyopo jijini Dodoma.
Waziri wa Nishati Mhe.Dkt.Medard Kalemani,akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mlowa Barabarani wakati wa kuwasha umeme katika hospitali ya wilaya ya chamwino iliyojengwa kijiji cha Mlowa Barabarani iliyopo jijini Dodoma.
Mbunge wa jimbo la Mtera Mh. Livingstone Lusinde akiwahutubia wananchi wa jimbo lake katika kijiji cha Mlowa Barabarani ambapo Waziri wa Nishati Mhe.Dkt.Medard Kalemani,leo  amewasha umeme katika hospitali ya wilaya ya chamwino iliyojengwa kijiji cha Mlowa Barabarani iliyopo jijini Dodoma.
Sehemu ya jengo la  hospitali ya wilaya ya chamwino iliyojengwa kijiji cha Mlowa Barabarani iliyopo jijini Dodoma ambayo leo imepata umeme.
Waziri wa Nishati Mhe.Dkt.Medard Kalemani,akisisitiza jambo kwa wananchi wa kijiji cha Mlowa Barabarani kabla ya kuwasha umeme katika  hospitali ya wilaya ya chamwino iliyojengwa kijiji cha Mlowa Barabarani iliyopo jijini Dodoma.
Waziri wa Nishati Mhe.Dkt.Medard Kalemani,akitoa mkono wa shukrani mara baada ya kupewa zawadi ya Mbuzi wawili na wanakiji wa Mlowa Barabarani mara baada ya kuwasha  umeme katika  hospitali ya wilaya ya chamwino iliyojengwa kijiji cha Mlowa Barabarani iliyopo jijini Dodoma.
Waziri wa Nishati Mhe.Dkt.Medard Kalemani (katikati) akiwa na viongozi akikata utepe wa kuashiria uzinduzi wa umeme katika  hospitali ya wilaya ya chamwino iliyojengwa kijiji cha Mlowa Barabarani iliyopo jijini Dodoma.
Waziri wa Nishati Mhe.Dkt.Medard Kalemani,akipiga makofi mara baada ya kuzindua uwashaji wa  umeme katika  hospitali ya wilaya ya chamwino iliyojengwa kijiji cha Mlowa Barabarani iliyopo jijini Dodoma.
Waziri wa Nishati Mhe.Dkt.Medard Kalemani,akiwasha umeme katika  hospitali ya wilaya ya chamwino iliyojengwa kijiji cha Mlowa Barabarani iliyopo jijini Dodoma.

……………………
Na.Alex Sonna,Dodoma

Waziri wa Nishati, Dk.Medard Kalemani amesema hakuna kijiji cha jimbo la Mtera kitakachobaki kutokuwa na umeme kufikia Juni mwaka 2020.
  Aidha, ameagiza Shirika la Umeme nchini(Tanesco) kuhakikisha linapeleka umeme katika vitongoji vyote vya Mlowa kuanzia wiki ijayo.
  Kalemani ametoa kauli hiyo alipokuwa akiwasha umeme katika hospitali ya Mlowa wilaya ya Chamwino.
  Amesema hadi Juni mwakani jimbo zima litakuwa na umeme kwenye vijiji vyote na kazi ya kupeleka kwenye vitongoji itaendelea hadi Juni 2021.
  “Leo tunapoongea kuna vijiji 38 ndani ya miaka minne na viwili vinawaka umeme kesho vinafikia 40, naomba tumpongeze Rais John Magufuli kwa kazi nzuri anayofanya,”amesema.
  Ameeleza kuwa vijiji 20 vinavyobaki vipo kwenye mpango ambapo vijiji vinne kati ya 20 vilivyobaki vitapelekewa umeme wiki ijayo na Tanesco.
  “Vijiji 16 vitakavyobaki vitapelekewa umeme mwezi februari 2020,”amesema.
  Amewaonya Tanesco kutojaribu kuwatoza wananchi gharama kubwa ya kuunganisha umeme zaidi ya Sh.27,000.
  “Msijaribu awe mkandarasi au Tanesco mwenyewe au REA atakayefanya hivyo Meneja nikute umemfukuza, usipomfukuza nakufukuza wewe,”amesema.
  Kalemani amepiga marufuku ulipishaji wananchi nguzo za umeme na atakayetoza ajifukuzishe kazi mwenyewe.
  Waziri huyo amesema kuwaka kwa umeme kwenye jimbo hilo kutaharakisha maendeleo. “Rais ametoa fedha nyingi zaidi ya Sh.Bilioni 36 kuwaletea umeme mkoa wa Dodoma, ni wajibu wenu kuchangamkia, nitakapokuja hapa tutakuja kukagua,”amesema.
  Kwa upande wake, Meneja Tanesco wilaya ya Chamwino Bw.Baltazar Massawe,amesema umeme huo utasaidia wananchi kwenye shughuli mbalimbali ikiwemo wanafunzi na walimu.
  “Huduma za Afya zitaboreshwa kutokana na umeme kuwepo, wananchi wataweza kuanzisha viwanda vidogo vidogo,”amesema
  Naye, Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde amesema alimuomba Waziri huyo kufikisha umeme kwenye hospitali hiyo na akakubali.
  “Kuna baadhi ya maeneo yamerukwa tunaomba umeme kwenye vitongoji, nikuombe sana ujio wako uwe neema kwa kuhakikisha tunapata umeme katika kitongoji cha Sokoine ambacho kuna mradi wa maji pale lakini hakuna umeme,pia umeme ufike kwenye makanisa na misikiti,”amesema.

No comments:

Post a Comment