Katibu Mkuu maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. John Jingu akisalimiana na Mkuu wa Chuo cha
Maendeleo ya Jamii Uyole Bw. Rajab Kaleranda wakati alipowasili mkoani
Morogoro kufungua mkutano uliowakutanisha Wakuu wa vyuo na Taasisi za
Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii nchini.
Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. John Jingu akizungumza na Wakuu wa Vyuo na
Taasisi za Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii nchini wakati wa kikao
kilichowakutanisha wakuu hao katika kupanga Mikakati ya kuboresha Kada
za Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii.
Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo
ya Jamii Patrick Golwike akielezea jinsi Kada ya Maendeleo ya Jamii
inavyosaidia katika kueta mabadiliko na kusaidia jamii wakati kikao
kilichowakutanisha Wakuu wa Vyuo na Taasisi za Maendeleo ya Jamii na
Ustawi wa Jamii nchini kupanga Mikakati ya kuboresha Kada za Maendeleo
ya Jamii na Ustawi wa Jamii.
Kamishna wa Ustawi wa Jamii Dkt.
Naftali Ng’ondi akielezea jinis a Kada ya Ustawi wa Jamii inavyosaidia
katika kueta mabadiliko na kusaidia jamii wakati kikao
kilichowakutanisha Wakuu wa Vyuo na Taasisi za Maendeleo ya Jamii na
Ustawi wa Jamii nchini kupanga Mikakati ya kuboresha Kada za Maendeleo
ya Jamii na Ustawi wa Jamii.
Wakuu wa Vyuo na Taasisi za
Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii nchini wakisikiliza mada
mbalimbali katika kikao kilichowakutanisha kupanga Mikakati ya kuboresha
Kada za Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii.
Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW
……………………
Na Mwandishi Wetu Morogoro
Katibu Mkuu Idara Kuu Maendeleo ya
Jamii Dkt. John Jingu amevitaka Vyuo na Taasisi za Maendeleo ya Jamii
na Ustawi wa Jamii nchini kutoa elimu itakayowasaidia wahitimu kuleta
mabadiliko katika jamii zao na kuweza kujiajiri na kuajiri watu wengine
kuliko kutegemea kuajiriwa.
Dkt.John Jingu ameyasema haya leo
mkoani Morogoro wakati akifungua kikao kazi cha wakuu wa Vyuo na Taasisi
za Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii nchini kilicholenga
kubadilishana uzoefu kwa wakuu hao wa vyuo katika utendaji kazi na
kujengeana uwezo ili Taasisi na Vyuo viweze kufanikisha malengo ya
Taifa.
Dkt. Jingu amesema kuwa taaluma ya
Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii lazima iwe nyenzo ya kutatua
changamoto zilizopo katika jamii ikiwemo tatizo la ajira kwa vijana kwa
kutoa taaluma itakayowapa fursa wahitimu kujiajiri kutokana na taaluma
waliyopata.
“Umefika wakati sasa Taasisi na
Vyuo kuja na Mpango Mkakati wa namna ya kutekeleza dhana ya kujiajiri
kwa lengo la kuzalisha wahitimu mahiri ” alisema Dkt. Jingu.
Ameongeza kuwa Vyuo vya Maendeleo
ya Jamii na Ustawi wa Jamii vimetoa mchango mkubwa sana katika kutatua
changamoto za jamii na hivyo jamii kuthamini uwepo wa vyuo katika jamii
na mafanikio yaliyoonekana kwa vyuo hivyo yaonekane kwa kila chuo.
Aidha Dkt. Jingu amevitaka Vyuo
hivyo kuanzisha Vituo vya kielektroniki vya ubunifu na maarifa (Digital
Innovation Centre) ambao utarahisisha upatikanaji wa maarifa na ujuzi
kwa haraka zaidi kuliko kusoma vitabu na itatoa fursa ya kupata maarifa
katika muda mfupi.
“Natumaini ushiriki wetu katika
kikao kazi hiki utatuongezea ari na ubunifu wa kazi katika maeneo yetu
na mtazingatia mafunzo na maelekezo yatakayotolewa katika kuhakikisha
vyuo vinatoa matokeo chanya kwa kuzalisha wataalam wenye ujuzi na
maarifa ya kazi.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa
Idara ya Maendeleo ya Jamii nchini Patrick Golwike amesema kuwa ili
kujipambanua katika jamii umuhimu wa Kada ya Maendeleo ya Jamii
inatakiwa kuwa na mbinu ya namna ambayo Vyuo vya Maendeleo ya Jamii
itatoa wataalam wakaosaidia kuleta mabadiliko kwa jamii.
Naye Kamishna wa Ustawi wa Jamii
nchini Dkt. Naftali Ng’ondi amesema kuwa Kada ya Ustawi wa Jamii ni moja
kati ya Kada ambazo zina uwanda mpana wa kujiajiri na kuajiriwa hivyo
Vyuo na Taasisi ya Ustawi wa Jamii zijikite katika kutoa elimu
itakayowasaidia wahitimu hasa kujiajiri.
Wakuu wa Vyuo na Taasisi za
Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii wamekutana mkoani Morogoro katika
kikao kazi kilicholenga kutafuta namna bora ya taaluma ya Maendeleo ya
Jamii na Ustawi wa Jamii katika kuleta mabadiliko katika jamii.
No comments:
Post a Comment