Na mwandishi wetu, Morogoro
Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa
Morogoro kimesema kitendo cha baadhi ya vyama vya upinzani kususia
uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji utakaofanyika Novemba
24 mwaka huu vimeonyesha jinsi vilivyo na uteke wa fikra kisiasa na
kukosa kujiamini.
Ikiwa aina ya viongozi walionao
wataendelea na siasa za kususia uchaguzi, kusubiria kupinga matokeo kama
alivyozoea aliyekuwa mgombea urais wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad
vitasubiria kwa miaka mingi ijayo kushika dola.
Matamshi hayo yametamkwa jana na
katibu wa CCM Mkoa wa Morogoro Shaka Hamdu Shaka wakati akitoa tathimini
ya CCM mkoa huo kuelekea uchaguzi ambapo kati ya vijiji 669 CCM imepita
664, mitaa 327 CCM imepita 325 na vitongoji 3,358 CCM imepita
3,320 huku vyama vya CUF, Chadema, UDP act wazalendo vikiendelea
kusimamisha wagombea katika vijiji 5, mitaa 2 na vitongoji 38.
Shaka alisema kususia uchaguzi
hakutoi majawabu yakinifu kutokana na malalamiko ya upinzani badala yake
vyama hivyo vilipaswa kushiriki kisha vilalamike huku wakiwa na
ushahidi kama zilikuwepo dosari, itikadi au mapungufu kadhaa
lakini kususia tu wakati hawana jambo la kuwaonyesha wananchi badala
yake wanabaki kulalamika kama vifaranga vya kuku ni kuonyesha uteke wa
maarifa ya kisiasa na udhaifu mkubwa kwa upinzani nchini.
“Wapinzani wa Tanzania wakubali
wasikubali bado wateke kisiasa.
Viongozi wao wepesi na dhaifu mno kiupeo
na kiufahamu. Hawajengi nguvu za hoja bali ni walalamishi .
Kama
wagombea wenu wamekiuka kanuni za uchaguzi jawabu si kususa ifikie
wakatiupinzani usitafute huruma huo ni uzembe na kwa vyovyote vile sasa
wabadilike na waache utoto wa kisiasa.”Alisema Shaka
Amefahamisha kuwa upinzani hauwezi
kujilinganisha na ukomavu wa viongozi wa CCM kisiasa kwani uchanga wa
wa vyama vyao na ikiwa vitaendelea na siasa za kupiga mayowe bila kuwa
na hoja za maana vyama hivyo vitaendelea kukosa mipango na
oganaizesheni ya kisiasa mwisho vitapoteza muelekeo na kupotea katika
ramani za kisiasa.
“Vinaonekana kwenye maeneo ya
mijini wakipiga kelele mitaani.Hawapo kwenye vitongoji wala vijijini
kwasababu haviungwi mkono. Hata wagombea wao mijini wana jazba na
kujikuta wakishindwa hata kujaza fomu kwa mujibu taratibu na kanuni
alafu etibaada ya kujimarisha kutokana na mapungufu yao wanaendelea
kujichimbia kaburi” Alieleza Shaka
Akitoa mfano alikitaja chama cha
ACT Wazalendo ambacho alidai hakikuwahi kuwa hata na wanachama visiwani
Zanzibar, nacho sasa kimeanza kujigamba kuwa kitashinda urais
mwaka 2020 kwakuamini tu Maalim seif aliyehama CUF atakipa ushindi Chama
hicho.
Hata hivyo Shaka alimtaka kiongozi
mkuu wa chama hicho Zitto kabwe kufuta ndoto za kupata ushindi Tanzania
bara wala Zanzibar kwa kuzingatia kuwa siasa za Zanzibar ni nzito na
atambue kuwa hata Maalim Seif Sharif Hamadi zilimshinda tokea akiwaCCM
na baadae CUF kisha kuamua kuhamia ACT Wazalendo ambako nako hataweza na
hatamudu kubadili hata koma kwenye sentensi.
“Wagomee kushiriki uchaguzi lakini
waache kabisa kuchochea ghasia na fujo. Msingi mkuu wa Serikali za CCM
ni kulinda amani, umoja na utulivu hivyo atakayethubutu kuanzisha fujo
dola haitamuacha azidi kugharimu maisha ya wasio na hatia,
nawaomba wananchi wote wajitokeze kwa wingi 24 Novemba kutimiza haki yao
ya kikatiba kuwachagua viongozi wao wa mitaa, vijiji na vitongoji”
Alieleza Shaka
Source Mtanzania, Uhuru, Majira, la Jiji
No comments:
Post a Comment