Thursday, November 28, 2019

RAIS MAGUFULI AMPA TANO WAZIRI BITEKO


*****************************************
Na Tito Mselem Bukombe,
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jonh Pombe Magufuli
amempongeza Waziri wa Madini ambae pia ni Mbunge wa Jimbo la
Bukombe kwa kazi nzuri za maendeleo anazozifanya katika kuleta
maendeleo jimboni humo.


Kauli hiyo aliitoa alipokuwa kwenye ziara yake ya kikazi akielekea
mapumzikoni Wilayani Chato ambapo alisimamisha msafala wake ili
awasalimie wananchi wa Jimbo la Bukombe.


Rais Magufuli amesema anawashukuru sana wananchi wa Bukombe
kwa kumchagua Mbunge wa Jimbo hilo ambapo ameeleza kuwa
anamsaidia sana katika kutekeleza majukumu yake.


Aidha, Rais Magufuli amewataka wananchi wa Bukombe kuendelea
kushirikiana na viongozi wa eneo hilo ambapo amesema amemchagua
Biteko kuwa Waziri wa Madini ili atatue migogoro iliyodumu kwa muda
mrefu.

“Naomba nichukua fursa hii kuwashukuru sana wananchi wa Bukombe
kwa kunichagulia Mbunge huyu, maana ananisaidia sana katika
kutimiza majukumu yangu, nawapongeza sana,” alisema Rais Magufuli.
Rais Magufuli ameeleza kwamba, amemchagua Waziri Biteko kwenye
Wizara ambayo inachangamoto nyingi katika ukusanyaji wa mapato
ambapo kwasasa anaona muelekeo mzuri katika sekta hiyo.

Wakati huo huo, Rais Magufuli, amewataka Wakurugenzi wa
Halmashauri zote nchi kuto kopa mikopo Bank ili wafanye miradi ya
maendeleo, kwayeyote atakaye kopa ajiandae kuondoka madarakani.


Kwa upande wake Mbunge wa Bukombe ambae pia ni Waziri wa
Madini Doto Biteko amempongeza Rais Magufuli kwa mradi wa
Barabara ambapo Rais Magufuli ameongeza mtandao huo kutoka kilometa 256 za lami mpaka kufikia kilometa 1480 na miradi tisa
mikubwa ya maji aliyotekelezwa na Rais wa awamu ya tano.


Pia, Waziri Biteko amemshukuru Rais Magufuli kwa kuwapa wananchi
eneo la kulima na kuchungia mifago yao ambapo sehemu hizo zilikuwa
hifadhi ya taifa.


Pamoja na mambo mengine, Waziri Biteko amemuomba Rais Magufuli
kuangalia uwezekano wa kuongeza mtandao wa barabara kutoka
Ushirombo mpaka Katoro.

No comments:

Post a Comment