Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli mapema
leo, amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Benki ya Maendeleo ya
Biashara Mashariki na Kusini mwa Afrika (TDB) Bw. Admassu Tadesse ,Ikulu
jijini Dodoma.
Bw.
Tadesse akiwa ameambatana na ujumbe wake amewasili uwanja wa ndege wa
jijini Dodoma leo, Novemba 25, 2019 na kulakiwa na Waziri wa Fedha na
Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango, na Mkuu wa Itifaki kutoka Wizara ya
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge.
Akizungumza
muda mfupi baada kumaliza mazungumzo na Mheshimiwa Rais Magufuli, Bw.
Tadesse amesema TDB itaendelea kufanya kazi kwa ukaribu na Serikali ya
Tanzania na kuipatia Tanzania mkopo wenye masharti nafuu kwa ajili ya
kutekeleza miradi mbalimbali maendeleo nchini.
Mhe.
Dkt. Mpango amesema TDB imekuwa moja ya Benki kinara ambayo imekuwa
ikitoa mikopo ya masharti nafuu kwa Tanzania hivyo kuchangia kwa kiasi
kikubwa kwenye miradi ya maendeleo.
Aidha,
Bw. Tadesse akiwa nchini atatembelea maeneo mbalimbali sambamba na
kujionea miradi ya maendeleo inayotelezwa na Serikali ikiwemo miradi ya
ujenzi wa miundombinu ya usafirishaji, mradi wa kuzalisha umeme wa Kilwa
na miradi mingine ambayo mkopo kutoka (TDB) utaelekezwa.
Bw.
Tadesse amesifu jitihada zinazofanywa na Serikali katika kufanya
mageuzi ya kiuchumi nchini na ushirikiano mzuri uliopo kati ya Serikali
ya Tanzania na Benki ya Maendeleo ya Biashara Mashariki na Kusini mwa
Afrika.
Viongozi na Watendaji wa Serikali wakiwa na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Biashara Mashariki na Kusini mwa Afrika (TDB) Bw. Admassu Tadesse mara baada ya kumlaki katika uwanja wa ndege jijini Dodoma. |
No comments:
Post a Comment