Gari aina ya ISUZU
lori lililotekea kwa moto ulitokea mwishoni mwa wiki kwa muda wa siku 6
katika Shamba la misitu la Sao Hill ambapo jumla ya hekta za miti 1000
aina ya misindano na mikaratusi zimeathiriwa na moto na kusababisha
jumla ya hasara ya kiasi cha shilingi bilioni tano
Miti aina ya
misindano yenye miaka miwili iliyoathiriwa na moto uliotokea mwishoni
mwa wiki uliosababishwa na wananchi wanaoandaa mashamba kwa ajili ya
kilimo ambapo jumla y ya hekta za miti 1000 aina ya misindano na
mikaratusi zimeathiriwa na moto na kusababisha jumla ya hasara ya kiasi
cha shilingi bilioni tano.
Naibu Waziri wa
Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akizungumza na Waandishi
wa Habari baada ya kutembelea sehemu ya shamba la miti la Sao Hill baada
ya kujionea hasara kubwa iliyosabishwa na moto.
Naibu Waziri wa
Maliasili na Utalii, Mhe, Constantine Kanyasu akisalimiana na baadhi ya
watuishi wa shamba la miti la Sao Hill mara baada ya kuwasili kwa ajilli
ya kutembelea shamab hilo lililoungua kwa muda wa siku sita na
kusababisha hekta 1000 kuungua kwa moto na kusababisha hasara ya zaidi
ya shilingi bilioni 5.
…………
Naibu Waziri wa
Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu jana amefanya ziara ya
kutembelea sehemu ya Shamba la miti Sao Hill lilipo wilayani Mufindi
mkoani Iringa ambalo limeathiriwa na moto.
Moto huo uliotokea
mwishoni mwa wiki katika kipindi cha siku sita na umeathiri zaidi ya
hekta 1000 za miti likiwemo shamba hilo la Serikali pamoja na mashamba
mengine ya Taasisi zingine na watu binafsi.
Katika shamba hilo
pekee jumla ya hekta 600 za miti aina ya misindano na mikaratusi
imeathirika na moto huku vyanzo vya moto huo vikidaiwa kuwa ni wananchi
kuandaa mashamba kwa ajili ya kilimo, urinaji wa asali pamoja na
shughuli za uvunaji miti.
Mbali ya hasara hiyo, Moto huo
pia umeleta madhara makubwa ikiwa ni pamoja na kumuunguza mtumishi wa
kiwanda cha Sao Hill alipokuwa katika jitihada za kuzima moto huo,
Aidha, moto huo umeteketeza
gari aina Isuzu Lori. mizinga ya nyuki 24 kati ya 83 , mbao, magogo
pamoja na mashine za kuchania mbao zilizokuwemo katika shamba hilo.
Akizungumzia kuhusu hasara hiyo,
Naibu Waziri Kanyasu amesema moto huo umesababisha hasara ya zaidi ya
jumla ya kiasi cha shilingi bilioni tano huku ukiwaacha wananchi
waliokuwa na mashamba ya miti kwenye wakati mgumu.
Amesema kwa mwaka jana pekee
Shamba hilo la miti la Sao Hill, moto huo uliunguza hekta 400 za miti
na hivyo kusababisha hasara ya zaidi ya kiasi cha shilingi bilioni 1.
Kufuatia hali hiyo Waziri
Kanyasu ameuagiza Uongozi wa Shamba hilo kuiuza haraka miti iliyokuwa
imefikia umri wa kuanzia miaka 10 hadi miaka 27.
Amesema taratibu hizo zifanyike
haraka kwa vile miti iliyoungua kwa moto ikiendelea kubaki kama ilivyo
huharibika kwa haraka na hivyo kupelekea kutokufaa kwa mbao.
Hata hivyo, Mhe. Kanyasu amesema
licha ya kuwa miti hiyo itauzwa , Shamba hilo limepata hasara kubwa
kwa vile sehemu kubwa ya miti iliyoathiriwa na moto ni yenye umri wa
miaka mitatu ambayo haiwezi kutumika kwa matumizi yoyote.
Kufuatia hali hiyo Naibu Waziri Kanyasu ameutaka Uongozi wa
wilaya ya Mufindi kuandaa sera itakayowazuia wananchi kuandaa mashamba
yao katika kipindi cha msimu wa kilimo kwa kutumia moto ili kuzuia
hasara kubwa inayotokea kila mwaka.
Aidha, Ameuagiza Uongozi wa
shamba hilo kuja na mkakati mpya wa namna ya kukabiliana na janga hilo
la moto ikiwa ni pamoja na kuandaa kingo zenye ukubwa wa kutosha kati ya
shamba moja na jingine ili kuzuia moto endapo utaweza kutokea usiweze
kuathiri sehemu kubwa ya miti.
”Matukio haya ya moto
yanayotokea kila mwaka inabidi yatufundishe namna ya kuweza kukabiliana
nayo, tusipotaka kujifunza mwakani tutapoteza hekta nyingi zaidi”
alisisitiza Kanyasu.
Amesema licha ya kuwa inaonekana
kulikuwa na maandalizi ya kutosha kutoka kwenye vikosi vya kuzuia moto
lakini hata hivyo kuna haja ya kutumia teknolojia mpya ya namna ya
kupambana na moto huo uliounguza hekta 1000 kwa muda wa masaa mawili.
Akizungumzia kuhusu hatua
zilizochukuliwa hadi hivi sasa za kukabiliana na majanga ya moto katika
shamba hilo, Mhe. Kanyasu amesema licha ya kuwa shamba hilo limeagiza
gari la zima moto lenye thamani ya kiasi cha shilingi milioni 800 lakini
hata hivyo kutokana na jiografia la eneo hilo halitaweza kuleta
ufanisi.
kwa upande wake Kaimu Meneja wa
Shamba hilo, Sillima Kombe amesema ili kukabiliana na majanga hayo ya
moto katika shamba hilo la Sao Hill lenye ukubwa hekta 135,903
linahitaji ndege zisizo na rubani tatu, Helikopta 3 pamoja Darubini za
kisasa 20.
No comments:
Post a Comment