Friday, November 15, 2019

MISA YAWATAKA WAANDISHI WA HABARI MKOA WA IRINGA KURUDI DARASANI

  Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Africa (MISA) tawi la Tanzania Salome Kitomari akienelea kutoa elimu juu ya waandishi wa kujua umuhimu wa kuendelea kusoma kwa kuwa elimu haina mwisho
 Waandishi wa habari wa mkoa wa Iringa wakiwa makini kusikiliza mjadala ambao ulikuwa unaendelea kuhusu umuhimu wa elimu ya uandishi wa habari
  Waandishi wa habari wa mkoa wa Iringa wakiwa makini kusikiliza mjadala ambao ulikuwa unaendelea kuhusu umuhimu wa elimu ya uandishi wa habari 
Waandishi wa habari na wadau wa habari wa mkoa wa Iringa wakiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa MISA Tanzania

NA FREDY MGUNDA,IRINGA.

Wanahabari mkoa wa Iringa wametakiwa kuongeza kiwango cha elimu ili kuweza kufanya kazi kwa kujiamini na kwa weledi wa hali ya juu katika kazi zao.

Akizungumza kwenye majadiliano ya kubaini changamoto za waandishi wa habari mkoani Iringa mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Africa (MISA) tawi la Tanzania kwa kushirikiana na Internews,Salome Kitomari alisema kuwa waandishi wa habari mkoani Iringa wanatakiwa kufanya kazi kwa weledi kutokana na elimu uliyonayo.

“Waandishi wakiwa na elimu ya uandishi wa habari wanapaswa kuishi maisha yaliyo mazuri kwa manufaa ya jamii kwa kuwa waandishi wa habari ni kioo cha jamii,mwandishi unapaswa kujiuliza kwenye jamii unaonekanaje kutokana na kazi yako” alisema Kitomari

Kitomari alisema kuwa waandishi wa habari wanatakiwa kuwa nadhifu muda wote kutokana na taaluma inavyotaka ili kuweza kutambulika kisheria kama taaluma nyingine ambazo zinatambuliwa vizuri kwa muonekano wao kwa wanataaluma wao.

“Waandishi wa habari mnatakiwa kuvaa mavazi nadhifu kama ilivyo wanasheria ambavyo wamekuwa wanaonekana wawapo kazini ndio maana wanaaminika zaidi ya waandishi wa habari hivyo inatupaswa kubadilika kimuonekano” alisema Kitomari

Aidha Kitomari alisema ikifika 2021 kama huna elimu ya stashada ya elimu ya uandishi wa habari hautakuwa na fursa ya kuendelea kufanya kazi ya uandishi wa habari kwa mujibu wa sheria za nchi hii.

“Kama ujaanza kusoma stashada ya elimu ya uandishi wa habari basi ikifika 2021 utakuwa hujamaliza hivyo hutakuwa na sifa za kuwa mwandishi wa habari hasa usisubili changamoto hiyo ikukute jiongeze kitaaluma.” Alisema Kitomari

Lakini katika majadiliano ya kubaini changamoto kwa waandishi wa habari mkoani Iringa kuliibuka changamoto kama tatizo la uchumi kwa mwandishi mmoja mmoja ambapo ilionekana waandishi wengi hawaandiki habari kiweledi kutokana na na tatizo la kiuchumi.

Raymond Minja mwandishi wa gazeti la Mtanzania alisema kuwa waandishi wengi wa sasa wamekuwa wakiandika habari za kusifu na kuabudu kutokana na tatizo la uchumi kwa kuandika kile kitu anachokita mtoa habari.

“Tunaandika sana habari za kusifu na kuabudu kutokana na waandishi wengi kuwategemea watoa habari ambao mara nyingi wanakuwa viongozi wa kada mbalimbali na kupelekea kutoka katika misingi ya taaluma ya uandishi wa habari” alisema Minja

Waandishi wa habari wanachuki wao kwa wao,hawapendani na wanaubinafsi kutokana na tatizo la changamoto ya uchumi duni hiyo kupelekea waandishi wengi kuanza kutoka kwenye weledi wa taaluma hiyo, alisema Denis Mlowe mwandishi wa gazeti la Tanzania Daima


No comments:

Post a Comment