MBUNGE wa Singida Mashariki Mhe Miraji Mtaturu amechangia mifuko ya saruji 23 ili kusaidia ujenzi wa madrasa iliyopo msikiti wa Alqadiria Unyang’ongo Kata ya Makiungu.
Akikabidhi mchango huo kwa niaba ya mbunge, katibu wa mbunge huyo Mwiru Limu amewashukuru viongozi wa dini kwa malezi wanayoyatoa kupitia mafunzo ya dini kwa waumini wao.
“Nakabidhi mifuko hii kwa niaba ya Mbunge,niwaombe muendelee kuiombea nchi yetu iwe na amani,maana bila ya kuwa na amani hatuwezi kufanya haya tunayoyafanya ikiwemo kuabudu na kufanya shughuli za maendeleo,”alisema Limu.
Mbali na mifuko hiyo,wadau walioshiriki kwenye changizo hilo waliunga mkono kwa kuchangia zaidi ya laki 6.
Akipokea msaada huo Imam wa Msikiti Sheikh Aboubakari Msidada amemshukuru mbunge kwa msaada.
“Changizo hili lililenga tupate michango mbalimbali ili tuweze kufyatua matofali 5,000 kwa ajili ya kujenga chuo cha kufundishia vijana dini,tunawashukuru wote waliotuunga mkono na Insha Allah Mwenyezi Mungu atawalipa,”alishukuru Sheikh Msidada.
No comments:
Post a Comment