Naibu Waziri wa Maliasili na
Utalii, Mhe, Constantine Kanyasu akizungumza na wananchi wa kijiji cha
Mhende kinachopakana na Hifadhi ya Taifa ya Mikumi kabla ya kukabidhi
Pembejeo za kilimo pamoja na vifaa vitakavyowasaidia Ulinzi shirikishi
katika mapambano dhidi ya Ujangili.
Balozi wa China nchini Tanzania,
WaNG KE akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mhende kinachopakana na
Hifadhi ya Taifa ya Mikumi kabla akiwaeleza wananchi kuwa Mabalozi kwa
kujikita katika kilimo kwa kuendesha shughuli za kilimo kwa njia ya
kisasa kwa kutumia mbegu za kisasa walizopewa na Ubalozi huo.
Naibu Waziri wa Maliasili na
Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akiwa na Balozi wa China nchini
Tanzania, Wang Ke (katikati) akimkabidhi Kamishna Mhifadhi wa Kanda ya
Mashariki, Steria Ndaga moja ya kompyuta mpakato kati ya nne ambazo
zimetolewa na Ubalozi wa China kwa ajili ya kusaidia katika mapambano
dhidi ya Ujangili.
Naibu Waziri wa Maliasili na
Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akikabidhi msaada wa runinga Kamishna
Mhifadhi wa Kanda ya Mashariki, Steria Ndaga ambazo zitatumika kwa ajili
ya kutolea elimu kwa njia ya video kwa wananchi wa kijiji cha Mhenda
kuhusu athari zinazotokana na vitendo vya Ujangili. Kulia ni Kamishna
Msaidizi wa Uhifadhi ya Taifa ya Mikumi, Mathew Mombona kushoto ni Mkuu
wa wilaya ya Kilosa Mhe.Adam Mgoi
Naibu Waziri wa Maliasili na
Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akiteta jambo na Balozi wa China nchini
Tanzania, Mhe.Wang Ke kabla ya kukabidhi vifaa vya ujangili pamoja
pembejeo za kilimo kwa wananchi wa Kijiji cha Mhende wilayani Kilosa
mkoani Morogoro.
Balozi wa China nchini Tanzania ,
Wang Ke akizungumza mara baada ya kukabidhi mbegu mbalimbali za mazao
kwa Diwani wa Kata ya Mhe. Ali Athuman kwa ajili ya kuwasaidia wananchi
kujikita kwenye shughuli za kilimo na kuachana na vitendo vya ujangili.
Naibu Waziri wa Maliasili na
Utalii, Mhe, Constantine Kanyasu akiwa pamoja na Balozi wa China nchini
Tanzania, Wang KE wakiwa kwenye pamoja na baaadhgi ya wananchi pamoja na
watumishi wa Hifadhi ya Taifa ya Mikumi mkoani Morogoro.
(PICHA NA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII)
……………………..
Ubalozi wa China
nchini Tanzania umeunga juhudi za Serikali ya Tanzania katika
mapambano dhidi ya ujangili kwa kuziwezesha jamii zinazoishi karibu na
Hifadhi ya Taifa ya Mikumi kwa kuzipa pembejeo za kilimo ikiwa pamoja
na kuzijengea uwezo wa kulima kisasa ili kuwasaidia wananchi hao kuacha
kujihusisha na vitendo vya ujangili.
Hayo yamebainishwa
leo na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu
wakati Ubalozi wa China nchini ukikabidhi msaada wa pembejeo za kilimo
kwa wananchi wa kijiji cha Mhenda katika wilaya ya Kilosa mkoani
Morogoro
Ubalozi wa China nchini Tanzania
umetoa msaada wa mbegu za mahindi yenye ujazo wa kilo 2500, mbegu za
alizeti zenye ujazo wa kilo 150 pamoja mbegu za choroko zenye ujazo
wa kilo 800
Mbali na msaada huo, Ubalozi huo
umetoa jumla ya jozi 13 za sare za ulinzi shirikishi, buti 13, komputa
mpakato nne pamoja runinga moja
Mhe.Kanyasu amesema lengo la
vifaa hivyo ni kuwasaidia wananchi kujikita katika kilimo cha kisasa kwa
kutumia mbegu zenye ubora wa hali ya juu.
Akizungumza katika mkutano huo,
Mhe. Kanyasu amesema vifaa hivyo vitatumika katika kutoa elimu kwa
wananchi katika mapambano dhidi ya vitendo vya ujangili.
Katika hatua
nyingine, Mhe.Kanyasu ameipongeza Jamhuri ya watu wa China kukomesha
soko la meno ya tembo na kuamua kutoa msaada kwa wanavijiji ili nao
waweze kuachana na biashara hiyo haramu.
Awali, Balozi wa
China nchini Tanzania, Wang Ke amesema pembejeo za kilimo walizozitoa
itakwenda sambamba na mafunzo yatakayotolewa na wataalam kutoka China
watakaowafundisha wanakijiji kulima kwa kisasa ili waweze kuachana na
vitendo vya ujangili.
Ameeleza kuwa Ubalozi wa China
umeamua kuanza na kijiji hicho ili kuwasaidia wananchi kuweza kuzalisha
mazao mengi ili wasiweze kujiingiza katika vitendo vya ujangili.
Amesema China imeamua
kuisaidia Tanzania katika mapambano ya vita dhidi ya ujangilli kwa vile
watalii wanakuja nchini kwa ajili ya kuangalia wanyama, hivyo vitendo
vya ujangili vinakwamisha juhudi za serikali katika kujiletea maendeleo.
Aidha, Balozi huyo ameipongeza
Taasisi ya Kova SUKOS Foundation inayoshughulikia majanga kwa kuratibu
tukio hilo ikiwa pamoja na kujitoa kuhakikisha wananchi wa Mhende
wanakabidhiwa misaada hiyo itakayowasaidia katika kujiondoa katika
umasikini huku utalii ukizidi kushamiri.
Naye Diwani wa kata
ya Mhenda, Ali Athumani amemshukuru Balozi wa China kwa msaada huo na
kuahidi kuwa watakuwa mabalozi kwa vijiji vingine vilivyo karibu na
Hifadhi hiyo.
No comments:
Post a Comment