Friday, October 11, 2019

WANANCHI TEMBELEENI MAONESHO KUJUA ELIMU YA LISHE BORA - DKT NCHIMBI


Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt.Rehema Nchimbi akisaini kitabu cha wageni katika banda la Wizara ya Kilimo wakati alipofika kukagua hali ya maandalizi ya maadhimisho ya siku ya Chakula Duniani katika uwanja wa Bombadier mjini Singida.Kulia ni Victoria Shirima  Mkutubi Wizara ya Kilimo.
 Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt.Rehema Nchimbi akifanya tathmini ya hali ya lishe ( uwiano wa urefu na uzito)  wakati alipotembelea banda la Umoja wa Mataifa.Kulia ni Mtaalam wa Chakula na Lishe toka Shirika la Sema Singida Tito Mkemwa( aliyeshika kitabu).



Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhandisi Paskasi Muragili akisaini kitabu wakati alipotembelea banda la mradi wa Kudhibiti Sumu Kuvu kwenye nafaka (TANIPAC) kwenye maadhimisho ya Siku ya Chakula Duniani.Kushoto ni Mohamed Chikawe mwakilishi wa Mratibu toka Wizara ya Kilimo.

Na Revocatus Kassimba, Wizara ya Kilimo-Singida



Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe.Dkt.Rehema Nchimbi leo Ijumaa  tarehe 11 Octoba,2019ametembelea mabanda ya maonesho kwenye Maadhimisho ya Siku ya Chakula Duniani  yanayofanyika Kitaifa katika uwanja wa Bombardier,Manispaa ya Singida.

Amesema uwepo wa maadhimisho haya ni fursa kwa wananchi wote kutambua umuhimu wa lishe bora kwa afya .

Amebainisha kuwa elimu juu ya uandaaji chakula tangu kikiwa shambani,baada ya mavuno,wakati wa kukiandaa nyumbani na wakati wa kupika inatakiwa ili mwananchi ale mlo kamili na bora.

Mhe.Dkt.Nchimbi amewasihi wataalam wa lishe nchini kutoa elimu sahihi kwa wananchi kuelewa makundi  muhimu ya chakula kinachopaswa kutumiwa na binadamu.

"Uwepo wa maadhimisho haya ya kitaifa Singida usaidie jamii kutambua umuhimu wa lishe bora kwa ustawi wa afya za watu ili washiriki kikamilifu katika ujenzi wa taifa"Mhe. Nchimbi 

Aidha,amewasihi Mkuu huyo wa mkoa amewasihi wananchi kujitokeza kwa wingi kupata elimu juu ya lishe bora na teknolojia rahisi ya kuongeza thamani ya mazao ya chakula.


Uzinduzi rasmi wa maadhimisho hayo utafanyika Jumapili ijayo na yatahitimishwa tarehe 16 mwezi huu.

Kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ni " Lishe Bora kwa Ulimwengu Usio na Njaa".

No comments:

Post a Comment