Na Ezekiel Mtonyole, Dodoma.
Mwenyekiti wa Chama Cha
Mapinduzi CCM, Mkoa wa Dodoma, Godwin Mkanwa, amewataka viongozi wa
madhehebu mbalimbali ya dini hapa nchini katika nyumba za Ibada
kuhamasisha Jamii hasa vijana kuhakikisha wanafanya kazi za kujiingizia
vipato ili kwenda sambamba na falsafa ya hapa kazi tu.
Mkanwa ameyasema hayo
jijini Dodoma wakati wa ufunguzi wa Kongamano kubwa la kimataifa
lililondaliwa na kanisa la Tanzania Fellowship Churches, linalofanyika
Jijini hapa na kushirikisha makanisa yote ya ndani na nje ya nchi, tukio
lililoenda sambamba na harambee ya kuchangia ujenzi wa kanisa hilo hapa
Dodoma.
Amesema watumishi wa
Mungu katika nyumba za Ibada kuwaomba waendelee kuhamasisha Jamii hasa
vijana kutafuta kazi za kufanya ili kuhakikisha wanakuwa na vipato na
kujikwamua kiuchumi ili waendane na fulsafa ya Rais wetu ya hapa kazi
tu.
“Unajua watu wengi
hawajaelewa hii falsafa ya hapa kazi tu, lengo ni kuhakikisha kila mtu
anakuwa na shughuri ya kufanya kupata kipato, hata neno la Mungu
linasema asiyefanya kazi na asile, kwahiyo Watumishi wa Mungu kwenye
mahubiri yenu msiache kuhimiza Jamii kuhakikisha wanafanya kazi hasa
hawa vijana” amesema Mkanwa.
Amewataka watumishi wa
Mungu kuendelea kutoa elimu na kuwaonya hasa jamii kuachana na mambo
yasiyofaa hasa mimba za utotoni, mavazi, madawa ya kulevya, rushwa hivi
vyote vikemewe kwa nguvu ili tuwe na jamii njema na kwa vizazi vijavyo
maana Hali ya Sasa ni mbaya.
Amewashukuru kwa
kuendelea kuliombea taifa, pia amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Dkt John Magufuli kwa kutoa nafasi kwa walio magerezani kwa
kosa la uhujumu uchumi kuomba msamaha na kurejesha fedha, na amewataka
kutembelea katika magereza kuwahimiza wenye makosa Kama hayo kuomba
msamaha.
“Kwanza nimpongeze Rais
wetu kwa uamuzi wa kuwataka wenye makosa ya uhujumu uchumi kuomba
msamaha, Sasa na ninyi watumishi wa Mungu nendeni huko mkawakumbushe
maana kunawengine wamekaa huko mpaka wamechanganyikiwa Sasa muende huko
mkawakumbushe waone haja ya kukiri” amesema.
Kwa upande wake Askofu
wa Kanisa la Tanzania Fellowship of Churches, Godfrey Malasi, amesema
Kanisa hilo hufanya makongamano Kama hayo kila mwaka na kupitia
makongamano hayo hupita katika kutoa msaada kama kuisaidia jamii
mahospitalini, vituo vya kulelea yatima,magereza na katika mashule.
Amesema na kwa mwaka huu
Kongamano hilo linafanyika Jijini Dodoma, na kwa Mkoa wa Dodoma
wamepanga kutembelea katika gereza la Isanga na kutoa misaada kwa
wafungwa na kuwapa neno la kuwafariji na kuwapa matumaini ili nao
wajione bado wanathaminika.
Amesema Kanisa hilo lina
utaratibu wa ibada za nyumba kwa nyumba Jambo ambalo linasaidia
kuwafikia watu wengi na kueneza neno la Mungu, amesema wanautaratibu wa
shule za watoto katika kuhakikisha wanakuwa katika misingi bora na kuja
kuwa vijana wenye maadili hapo baadaye.
“Sisi kama watumishi wa
Mungu jukumu letu ni kuhakikisha kuwa tunaokoa roho za watu, na kujenga
kizazi chenye hofu na kumjua Mungu na kupitia ibada hizi tunawafikia
watu wengi na kufundishwa neno la Mungu kwa ukaribu na kwa undani zaidi
kupitia ibada za nyumba kwa nyumba” amesema Asikofu Malasi.
Amesema vijana wengi
wameharibika kutokana na kutowekewa misingi imara na kufundishwa neno la
Mungu tangu wakiwa wadogo, amesema bado kanisa linakazi kubwa ya
kuendelea kuokoa roho za watu na kuendelea kutoa maonyo mbalimbali
katika nyumba za ibada.
No comments:
Post a Comment