Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu
anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde akizungumza
na vijana wa Chuo cha Ufundi cha Mt. Anthony ambao wanasomeshwa kwa kwa
ufadhili wa Serikali kupitia Programu ya Ukuzaji Ujuzi Nchini iliyopo
chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu.
Sehemu ya vijana wa Chuo cha
Ufundi cha Mt. Anthony wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu
anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde (hayupo
pichani) alipowatembelea vijana hao kwa lengo la kukagua maendeleo ya
mafunzo yao.
Mkuu wa Wilaya ya Musoma Dkt. Vicent Naano akieleza jambo wakati wa ziara hiyo.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu
anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde akizungumza
jambo na vijana wanaojifunza fani ya Uchomeleaji na uungaji vyuma
alipotembelea karakana kujionea mafunzo ya vijana hao.
Baadhi ya vijana wanaojifunza ufundi wa magari wakijishughulisha ikiwa ni sehemu ya mafunzo yao.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu
anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde akizungumza
jambo na vijana wanaojifunza fani ya Ushonaji alipotembelea kujionea
mafunzo ya vijana hao.
PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU
(KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU)
………………….
Na; Mwandishi Wetu
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu
anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde amezitaka
Halmashauri za Wilaya, Manispaa na Majiji nchini kuwawezesha Vijana
kiuchumi kwa kutumia Vikundi na Kampuni za Vijana katika utekelezaji wa
miradi mbalimbali ya kimaendeleo kwa kuzipa zabuni kampuni na vikundi
hivyo kupitia utaratibu wa “force account” hasa katika utengenezaji wa
madawati na ujenzi wa madarasa, matundu ya vyoo, zahanati na vituo vya
Afya.
Naibu Waziri Mavunde kayasema hayo
Wilayani Musoma wakati alipotembelea Chuo cha Ufundi cha Mt. Anthony
ambapo jumla ya Vijana 240 wanasoma hapo fani mbalimbali kwa ufadhili wa
Serikali kupitia Programu ya Ukuzaji Ujuzi Nchini iliyopo chini ya
Ofisi ya Waziri Mkuu ambapo mwaka huu wa fedha 2019/2020 inatrajiwa
kuwajengea uwezo Vijana 46,000 katika fani mbalimbali.
“Serikali inayo nia ya dhati ya
kuhakikisha kwamba tunaijengea Ujuzi stahiki nguvukazi ya Taifa hili ili
vijana wengi zaidi waweze kushiriki kikamilifu katika uchumi wa viwanda
na kuwawezesha kujikwamua kiuchumi kupitia shughuli za uzalishaji
mali.Mamlaka za Serikali za Mitaa ziwe kichocheo katika kuwawezesha
Vijana kiuchumi kwa kutoa zabuni kwa vikundi na makampuni ya Vijana
nchini kote hasa zile zinapitia katika mfumo wa manunuzi wa force
account,” alisema Mavunde
Akitoa salamu za Mkoa, Mkuu wa
Wilaya ya Musoma Dkt. Vicent Naano amewahakikishia Vijana hao kupata
mikopo ya asilimia 4 na asilimia 2 kwa wenye ulemavu itokanayo na mapato
ya ndani ya Halmashauri na kuwataka kuunda vikundi kutokana na fani zao
za Ufundi.
Akizungumza kwa niaba ya Vijana
wenzake wanafuika ya Programu ya kukuza Ujuzi, Bw. Baraka Emmanuel
ameishukuru Serikali kwa kuwajali Vijana na kuwawezesha kupata Ujuzi
kupitia mafunzo wanayoyapata hapo Chuoni ambayo pia yatawafanya waweze
kujiajiri na kuajiri Vijana wengine.
No comments:
Post a Comment