Na Innocent Natai, Singida
Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt Rehema
Nchimbi amewataka wakazi wa mkoa wa Singida na mikoa mingine kujitokeza kwa
wingi katika maadhimisho ya siku ya chakula duniani yanayofanyikia kitaifa
mkoani Singida ili kupata elimu ya lishe bora na kilimo chenye tija ili kuepukana
na njaa kitaifa na Dunia kwa ujumla.
Ameyasema hayo leo tarehe 10 Octoba
2019 alipotembelea kukagua maandalizi ya maadhimisho hayo yaliyoanza rasmi katika
viwanja vya Bombadia (Peoples) ambapo ndipo maonyesho hayo yanapofanyikia.
Nchimbi amewataka wakazi wa singida
kuiona fursa waliyoipata ya maonyesho hayo kupangwa kufanyikia mkoani hapo na
kuitumia kwa kutembelea mabanda kwa ajili ya kupata elimu ya afya na lishe bora kwa ujumla na kujionea
fursa zilizopo katika kilimo pia.
Amesem kuwa endapo watatembelea
watapata fursa ya kujionea vyakula lishe na kujifunza namna bora ya kuandaaa na
kulima mazao lishe ili kuepukana na njaa katika jamiii yao na kwa dunia kwa
ujumla.
“Unapopata fursa ya kuja au kusikia
taarifa hizi hakikisha unamjulisha na mwenzako kwani hii ni fursa kubwa sana
nina imani hapa pia wajasiriliami wadogo wadogo kupitia maonyesho haya
watapata elimu na fursa ya kuuza bidhaa zao’’ Alisema Dkt Nchimbi.
Akizungumzia hali ya maandalizi ya
maonyesho hayo amesema kuwa mpaka sasa maandalizi yamekamilika na
muitikio ni mkubwa kwa wananchi wa mkoa wa Singida na mikoa ya jirani
kwani kwa siku ya kwanza tu wananchi wameonyesha kuvutiwa na maonyesho hayo kwa
kujitokeza kwa wingi katika viwanja hivyo.
Maonyesho hayo ya siku ya chakula
Duniani kitaifa mkoani Singida yameanza leo tarehe 10 Octoba 2019 na
yanatarajiwa kuzinduliwa rasmi tarehe 12 Octoba 2019 na kuhitimishwa tarehe 16
Octoba 2019 ambapo ndio siku ya kilele.
Mgeni rasmi wakati wa kilele cha
maadhimisho hayo anatarajiwa kuwa Waziri
wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) yakiwa na kaulimbiu ya “lishe bora kwa
ulimwengu usio na njaa’’
MWISHO
No comments:
Post a Comment