Naibu
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula
akiangalia picha zinazoonesha maeneo yaliyovamiwa wilaya ya Ilemela
wakati wa ziara yake ya kukagua utekelezaji wa kupitia maeneo
yaliyovamiwa katika wilaya za Ilemela na Nyamagana jana. Katikati
aliyevaa Miwani ni Kamishna Msaidizi wa Ardhi Kanda ya Ziwa Makwasa
Biswalo.
Naibu
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula
akiangalia moja ya eneo lililovamiwa wilaya ya Ilemela jana wakati wa
ziara yake ya kukagua utekelezaji wa kupitia maeneo yaliyovamiwa katika
wilaya za Ilemela na Nyamagana jana. Kushoto ni Kamishna Msaidizi wa
Ardhi Kanda ya Ziwa Makwasa Biswalo.
Naibu
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula
akiangalia picha zinazoonesha maeneo yaliyovamiwa wilaya ya Ilemela jana
wakati wa ziara yake ya kukagua utekelezaji wa kupitia maeneo
yaliyovamiwa katika wilaya za Ilemela na Nyamagana jana. Katikati
aliyevaa Miwani ni Kamishna Msaidizi wa Ardhi Kanda ya Ziwa Makwasa
Biswalo.
……………………
Na Munir Shemweta, WANMM MWANZA
Halmashauri
zote nchini zimetakiwa kupitia upya maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya
shughuli mbalimbali za kijamii kama vile makaburi, maeneo ya wazi,
ujenzi wa taasisi za umma na masoko ili kujiridhisha kama bado yanafaa
kwa matumizi yaliyokusudiwa au yamevamiwa ili kurasimisha.
Agizo
hilo limetolewa jana na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya
Makazi Dkt Angeline Mabula wakati akikagua utekelezaji wa kupitia maeneo
yaliyovamiwa katika wilaya za Ilemela na Nyamagana linalotekelezwa na
wataalamu wa Ardhi kutoka Wizarani, Ofisi ya kanda ya Ziwa na Maafisa
ardhi wa wilaya hizo.
Dkt
Mabula alikemea kitendo kinachofanywa na baadhi ya halmashauri nchini
kutolipa fidia katika maeneo wanayoyatwaa kunakosababisha kuzalisha
migogoro isiyo ya lazima na uvamizi mpya katika maeneo hayo.
‘’Halmashauri
zote nchini naziagiza kupitia upya maeneo yaliyotengwa kwa shughuli za
kijamii tujue maeneo hayo yamevamiwa kwa kiasi gani, tuwafanyie
urasimishaji wananchi walipe kodi ya serikali na kama eneo bado
halijavamiwa basi tulilinde ili lisiendelee kutumika kwa matumizi
yaliyo,kusudiwa ‘’ alisema Mabula
Aidha,
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi aliwataka wataalamu
wa ardhi nchini kuacha kukaa ofisini na badala yake waende kwa wananchi
ili kuepuka kuitia hasara serikali kwa kutoa taarifa zisizo na uhakika.
Alitoa
hofu wananchi wa mitaa ya Nyagungulu, Mwambani na Bukengwa yaliyopo
kata ya Ilemela mkoani Mwanza kuwa, serikali ya awamu ya tano itaendelea
kutatua migogoro ya ardhi kwa kuzingatia haki , sheria na ubinadamu.
Kwa
upande wake Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Stanslaus Mabula, mbali na
kumpongeza Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kazi
kubwa anayoifanya pia alimshukuru Rais John Pombe Magufuli kwa kuunda
timu ya Mawaziri kupitia maeneo yote yenye changamoto za ardhi huku
akiiomba halmashauri ya jiji la Mwanza kuhakikisha ulipaji fidia kwa
wananchi wenye migogoro ya ardhi unafanyika.
Naye
Kmaishna Msaidizi wa Ardhi kanda ya Ziwa Makwasa Biswalo alieleza kuwa,
zoezi la ukaguzi maeneo yaliyotengwa kwa shughuli za kijamii lilianza
septemba 30, 2019 na kumalizika Oktoba 4, 2019 kabla ya kuongezwa siku
nne na Naibu Waziri Dkt Mabula ambapo aliomba ushirikiano kutoka kwa
wananchi na viongozi ili kukamilisha zoezi hilo kwa haraka na ufanisi.
No comments:
Post a Comment