Dokta Bingwa wa Magonjwa ya
Saratani, Dkt Heri Tungaraza ambaye ni madaktari bingwa wa Jumuiya ya
Madaktari Watanzania waliosoma China (DCAT) akizungumza na wanahabari
wakati wa zoezi la hitimisho la zoezi la utoaji wa huduma ya afya bure
iliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita Hospitali ya Wilaya ya
Kisarawe, Pwani ambapo amesema kuwa zoezi lao limekuwa la mafanikio
makubwa kwa vile wameweza kupata wananchi wengi zaidi. Picha zote na
Cathbert Kajuna – Kajunason/MMG.
Wananchi wakiojitokeza kupatiwa huduma ya huduma ya afya bure iliyofanyika iliyopita Hospitali ya Wilaya ya Kisarawe, Pwani
Mkurugenzi wa Miradi wa DCAT, Linas Kahisha (mwenye miwani)
akigawia wananchi maji wakati wa zoezi la hitimisho la zoezi la utoaji
wa huduma ya afya bure iliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita
Hospitali ya Wilaya ya Kisarawe, Pwani.
Dokta Bingwa wa Magonjwa ya
Saratani, Dkt Heri Tungaraza (mwenye miwani) ambaye ni madaktari bingwa
wa Jumuiya ya Madaktari Watanzania waliosoma China (DCAT) akisimamia
utoaji wa huduma ya afya bure.
Wananchi wakiwa katika dirisha la
kupata dawa wakati wa zoezi la hitimisho la zoezi la utoaji wa huduma
ya afya bure iliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita Hospitali ya
Wilaya ya Kisarawe, Pwani.
Mkurugenzi wa Wilaya ya Kisarawe Musa Gama (wa tatu toka kulia
msitari wa mbele) akiwa na Timu ya Madaktari na wauguzi wa Wilaya ya
Kisarawe na madaktari bingwa wa Jumuiya ya Madaktari Watanzania
waliosoma China (DCAT).
Na Cathbert Kajuna – Kajunason/MMG.
Zaidi ya wananchi 800 wa wilaya ya
Kisarawe, Pwani wamejitokeza katika zoezi la utoaji wa huduma ya afya
bure iliyoandaliwa na madaktari bingwa wa Jumuiya ya Madaktari
Watanzania waliosoma China (DCAT).
Akizungumza wakati wa zoezi la
hitimisho la zoezi la utoaji wa huduma ya afya bure iliyofanyika
mwishoni mwa wiki iliyopita Hospitali ya Wilaya ya Kisarawe, Pwani Dokta
Bingwa wa Magonjwa ya Saratani, Dkt Heri Tungaraza amesema kuwa zoezi
lao limekuwa la mafanikio makubwa kwa vile wameweza kupata wananchi
wengi zaidi.
“Kikubwa tunamshukuru Mungu kwa
kuweza kufanikisha zoezi hili na limekuwa la mafanikio zaidi maana
tulitarajia watu 400 ila tumepata watu mara mbili ya namba tuliyoiweka,
yani tumepata watu zaidi ya 800 na wote tumeweza kuwahudumia japo sisi
hatukuwa wengi,” amesema.
Amesema kuwa ushirikiano na umoja walionao ndiyo nguzo pekee iliyoweza kufanikisha zoezi walilopanga kulifanya.
“Kiukweli timu yetu imekuwa na
ushirikiano zaidi kuanzia Viongozi wa Wilaya ya Kisarawe wakiwemo
wafanyakazi wa Hospitali ya Wilaya, waandishi wa habari na wote
tuliokuwa nao kipindi hicho,” amesema Dkt Tungaraza.
Ameongeza kuwa magonjwa waliyokuwa
wakichunguza ni yale ambayo si ya kuambukiza kama vile Shinikizo la
damu, presha na idadi kubwa imeonyesha watu wengi wanaugua shinikizo la
damu hasa akina mama.
“Tunashukuru waliojitokeza idadi
kubwa ni akina mama kwa asilimia 60, akina baba asilimia 30 na watoto
asilimia 10% na magonjwa yaliyoongoza baada ya uchunguzi ni Saratani ya
Shingo ya Kizazi na Shinikizo la damu na kidogo Kisukari,’ amesema.
Ametoa ushauri kwa jamii kuendelea
kuchunguza afya zao mara kwa mara ili kuweza kujiimalisha kuliko
kusubiri mpaka waugue ndiyo waweze kukimbilia kutibiwa.
Kwa upande wa Mkurugenzi wa Miradi
wa DCAT, Linas Kahisha amesema wameshukuru kwa ushirikiano walioweza
kuupata kutoka katika serikali ya wilaya ya Kisarawe na pia ubalozi wa
China nchini Tanzania ambao ndiyo waliowawezesha kufanikisha zoezi la
utoaji huduma ya Afya Bure na pia amewaomba jamii na wadau wengine
kuweza kuwaunga mkono ili kufanikisha waweze kufika maeneo mengi zaidi.
“Tumefurahi jinsi uongozi mzima
ulivyoweza kutupa ushirikiano kuwezesha wakazi wa Kisarawe kupatiwa
matibabu ya afya bure ila japo idadi iliyojitokeza imekuwa ni kubwa nje
ya malengo yao waliyokuwa wamepanga,” amesema.
Nae Mganga Mkuu wa Halmashauri ya
hospitali ya wilaya ya Kisarawe, Stanford John amewashukuru madaktari wa
Jumuiya ya Madaktari Watanzania waliosoma China (DCAT) kwa moyo wao wa
kujitoa kuhudumia wananchi wa Kisarawe.
No comments:
Post a Comment