Friday, September 20, 2019

WAZIRI WA KILIMO TANZANIA MHE JAPHET HASUNGA AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA WAZIRI WA KILIMO WA ZIMBABWE PERRANCE SHIRI JIJINI DAR ES SALAAM

Waziri wa Kilimo wa Tanzania Mhe Japhet Hasunga (Mb) akizungumza na Waziri wa Kilimo wa Zimbabwe Kamanda wa jeshi jeshi la anga Perrance Shiri, leo tarehe 20 Septemba 2019 katika ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mtaa wa Posta Jijini Dar es salaam. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Sehemu ya wataalamu wa Kilimo wa Zimbabwe wakifatilia mkutano huo leo tarehe 20 Septemba 2019 katika ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mtaa wa Posta Jijini Dar es salaam.
Waziri wa Kilimo wa Tanzania Mhe Japhet Hasunga (Mb) akizungumza na Waziri wa Kilimo wa Zimbabwe Kamanda wa jeshi jeshi la anga Perrance Shiri, leo tarehe 20 Septemba 2019 katika ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mtaa wa Posta Jijini Dar es salaam.
Waziri wa Kilimo wa Tanzania Mhe Japhet Hasunga (Mb) akizungumza na Waziri wa Kilimo wa Zimbabwe Kamanda wa jeshi jeshi la anga Perrance Shiri, leo tarehe 20 Septemba 2019 katika ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mtaa wa Posta Jijini Dar es salaam.

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma

Waziri wa Kilimo wa Tanzania Mhe Japhet Hasunga (Mb) leo tarehe 20 Septemba 2019 amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Kilimo wa Zimbabwe Kamanda wa jeshi jeshi la anga Perrance Shiri.

Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mtaa wa Posta Jijini Dar es salaam.

Akizungumza mara baada ya mkutano huo Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga amesema kuwa miongoni mwa mambo yaliyojadiliwa katika mkutano huo ni pamoja na kuongeza ushirikiano katika sekta ya kilimo baina ya Zimbabwe na Tanzania.

Alisema kuwa nchi zote mbili zina uzoefu katika sekta ya kilimo hivyo uzoefu huo unapaswa kuhuishwa katika nchi zote mbili ili kuwa na tija ya kilimo na kuimarisha usalama wa chakula.

Mhe Hasunga alisema kuwa ujumbe wa wataalamu wa Kilimo kutoka nchini Zimbabwe ukiongozwa na Waziri wao wa Kilimo umeiomba serikali ya Tanzania kuwaongezea Tani 70,000 ili kufikia Tani 100,000 waweze kurudi nazo nchini Zimbabwe

Katika kikao hicho Waziri Hasunga amesema kuwa wamekubaliana wataalamu wa wizara ya Kilimo wa Zimbabwe na Wataalamu wa Kilimo wa Tanzania wakutane katika kikao kazi kujadiliana namna bora ya kufanya biashara hiyo.

“Jana wameshuhudia treni ya kwanza ikiondoka kuelekea Zimbabwe ikiwa imebeba Tani 1200 za mahindi na wanategemea Tani 17,000 za awali ambazo wamechukua ziwasili mapema iwezekanavyo” Alisisitiza Mhe Hasunga

Kwa upande wake Waziri wa Kilimo wa Zimbabwe Kamanda wa jeshi la anga Perrance Shiri amesema kuwa lengo la ziara yake nchini Tanzania ni pamoja na kufuatilia utekelezaji wa mauzo ya mahindi kutoka Tanzania kuelekea Zimbabwe.

Pia amemuomba waziri wa kilimo wa Tanzania kuwa na ushirikiano wa pamoja kwenye sekta ya kilimo hususani katika zao la mpunga na mazao mengine.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Magufuli aliingia makubaliano na Rais wa Zimbabwe Mhe Emmerson Mnangagwa kuwa Tanzania itaiuzia Zimbabwe tani 700,000 za mahindi kufuatia nchi hiyo kukabiliwa na upungufu wa chakula.

MWISHO

No comments:

Post a Comment