Waziri wa Maji Mhe.Prof.Makame
Mbalawa ,akiwahutubia wananchi wa Kata ya Nghong’onha jijini Dodoma
Katika hafla ya uzinduzi wa Mradi wa Maji Katika kata hiyo .
Mkurugenzi wa Masuala ya Afrika
Mashariki wa Wizara ya Maendeleo ya Uchumi na Ushirikiano wa Serikali ya
Shirikisho la Ujerumani, Bi Vera Rosendahl,akitoa taarifa kwa wananchi
wa Kata ya Nghong’onha iliyopo Mkoani Dodoma Katika hafla ya uzinduzi wa
Mradi wa Maji Katika kata hiyo .
Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini
ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu ,Kazi ,vijana na
Ajira,Mhe.Anthony Mavunde,akiwaelezea wananchi wa Kata ya Nghong’onha
jijini Dodoma Katika hafla ya uzinduzi wa Mradi wa Maji Katika kata hiyo
.
Kaimu mkuu wa mkoa wa Dodoma
,ambaye pia ni Mkuu wa wilaya Patrobas Katambi,akizungumza na wananchi
wa Kata ya Nghong’onha jijini Dodoma wakati wa hafla ya uzinduzi wa
Mradi wa Maji Katika kata hiyo .
Sehemu ya wananchi wa Kata ya Nghong’onha jijini Dodoma wakifatilia hafla ya uzinduzi wa Mradi wa Maji Katika kata hiyo .
Waziri wa Maji Prof.Makame
Mbalawa,akifungua kitambaa akiwa na Mkurugenzi wa Masuala ya Afrika
Mashariki wa Wizara ya Maendeleo ya Uchumi na Ushirikiano wa Serikali ya
Shirikisho la Ujerumani, Bi Vera Rosendahl,tayari kwa ajili ya
kuzindua Mradi wa Maji katika Kata ya Nghong’onha iliyopo mkoani Dodoma
kulia ni Kaimu mkuu wa mkoa wa Dodoma ,ambaye pia ni Mkuu wa wilaya
Patrobas Katambi.
Waziri wa Maji Prof.Makame
Mbalawa,akipeana mkono na Mkurugenzi wa Masuala ya Afrika Mashariki wa
Wizara ya Maendeleo ya Uchumi na Ushirikiano wa Serikali ya Shirikisho
la Ujerumani, Bi Vera Rosendahl,mara baada ya kumaliza kuzindua Mradi wa
Maji katika Kata ya Nghong’onha iliyopo mkoani Dodoma kulia ni Kaimu
mkuu wa mkoa wa Dodoma ,ambaye pia ni Mkuu wa wilaya Patrobas Katambi.
Waziri wa Maji Prof.Makame
Mbalawa,aakiwa na Mkurugenzi wa Masuala ya Afrika Mashariki wa Wizara
ya Maendeleo ya Uchumi na Ushirikiano wa Serikali ya Shirikisho la
Ujerumani, Bi Vera Rosendahl,wakifungua maji kwenye kisima mara baada ya
kuzindua Mradi wa Maji katika Kata ya Nghong’onha iliyopo mkoani Dodoma
Waziri wa Maji Prof.Makame
Mbalawa,pamoja na Mkurugenzi wa Masuala ya Afrika Mashariki wa Wizara
ya Maendeleo ya Uchumi na Ushirikiano wa Serikali ya Shirikisho la
Ujerumani, Bi Vera Rosendahl,wakimtwisha maji mwanamama wa kata ya
Nghong’onho baada ya kuzindua Mradi wa Maji katika Kata ya Nghong’onha
iliyopo mkoani Dodoma .
Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini
ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu ,Kazi ,vijana na
Ajira,Mhe.Anthony Mavunde,akimtwisha ndoo ya maji wananchi wa Kata ya
Nghong’onha jijini Dodoma baada ya kuzinduliwa Mradi wa Maji Katika kata
hiyo
Waziri wa Maji Prof.Makame
Mbalawa,akimtwisha ndoo ya maji mwananchi wa kata ya Nghong’onho baada
ya kuzindua Mradi wa Maji katika Kata hiyo
Waziri wa Maji Prof.Makame
Mbalawa,akimtwisha ndoo ya maji Mkurugenzi wa Masuala ya Afrika
Mashariki wa Wizara ya Maendeleo ya Uchumi na Ushirikiano wa Serikali ya
Shirikisho la Ujerumani, Bi Vera Rosendahl,baada ya kzuindua Mradi wa
Maji katika Kata ya Nghong’onha iliyopo mkoani Dodoma .
Waziri wa Maji Prof.Makame Mbalawa,akiwa picha ya pamoja viongozi wa GIZ.
…………………
Na.Alex Sonna,Nghong’onha,Dodoma
SERIKALI imesema kuwa imejipanga
kukarabati miradi yote ya maji iliyotelekezwa kwa kipindi kirefu ili
kupunguza adha ya uhaba wa maji kwa wananchi.
Hayo yamebainishwa leo jijini
Dodoma na Waziri wa Maji Prof.Makame Mbalawa wakati akihutubia wananchi
wa Kata ya Nghong’onha Katika hafla ya uzinduzi wa Mradi wa maji Katika
kata hiyo .
Waziri Mbalawa amesema
makandarasi wa ovyo wamekuwa wakikwamisha juhudi za serikali Katika
maendeleo na kusababisha hasara hivyo kuwataka kujitathimini upya.
“Serikali haitomfumbia macho
mkandarasi yeyote anayegeuza miradi ya maji Kama kitega uchumi
chake,lazima kila mtu akae kwenye mstari kuhakikisha anafanya maendeleo
kwa moyo mmoja,”amesema.
WaziriProf.Mbalawa amesema
Mradi wa maji Katika kata hiyo ulianza tangu mwaka 2013 ambapo
umechukua miaka 7 kukamilika kwake huku akilipongeza Shirika la
Maendeleo la Ujeruman [ GIZ ]Kwa kufanikisha mradi huo.
“Huu ni uzembe mkubwa ,Mradi
wa maji unachukua miaka mingi tunaweza kuufananisha na umri wa mtoto
ambapo mwaka 2013 angezaliwa mwaka angeanza darasa la kwanza,”alisema na
kuongeza,
“Katika Mradi huu kulifanyika
uzembe wa hali ya juu na uhuni kwani Mradi huu ulitakiwa kukamilika kwa
kipindi Cha miezi sita tu tangu kuanza kwake,”alisisitiza Mbalawa.
Kutokana na hayo amewataka
watendaji wote wa wizara ya maji kuhakikisha wanakuwa makini
kushughulikia miradi ya huduma za kijamii ili kuhakikisha inaondoa kero
kwa wananchi.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa
Masuala ya Afrika Mashariki wa Wizara ya Maendeleo ya Uchumi na
Ushirikiano wa Serikali ya Shirikisho la Ujerumani, Bi Vera Rosendahl
amesema kukamilika kwa mradi huo ni mafanikio makubwa ya uhusiano wa
Tanzania na Ujerumani.
Mradi huo utasaidia zaidi ya watu
12,000 ambao hawakua na uwezo wa kupata maji safi na hivyo sasa suala la
ukosefu wa maji Nghong’onha . linaenda kuwa historia.
” Kwa kufahamu umuhimu wa maji kwa
wananchi na kumtua mama ndoo sisi tulitoa kiasi cha Shilingi Milioni
350 ili kuwezesha kukamilika kwa mradi huu.
Tunawashukuru sana Wizara ya Maji,
Halmashauri ya Jiji la Dodoma na zaidi wananchi wa eneo hili kwa namna
ambavyo wametoa ushirikiano wa kutosha katika kukamilisha mradi huu,”
Amesema Bi Rose.
Ameahidi kuendeleza ushirikiano
kwa Serikali ya Tanzania katika kuwaletea maendeleo wananchi hasa katika
miradi ambayo inayagusa maisha yao moja kwa moja.
Naye mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya
maji na usafi wa mazingira (DUWASA)Mhandisi David Palangyo aliishukuru
serikali ya Ujerumani kujitolea kushirikiana nao kutatua kero ya maji
kwa wakazi wa Kata ya Nghong’onha .
Mhandisi huyo amesema wao Kama
wadau wa maji watahakikisha wanakuwa karibu na wakazi hao kuhakikisha
wanalinda miundombinu ya maji huku wakijipanga kuanzisha kamati ya maji
ya kata hiyo itakayosimamia mapato kwa uzalendo.
“Hakuna asiyefahamu shida
nliokuwa mkiipata,na Sasa mmepata maji moiyoyatamani kwa kipindi kirefu
tafadhalini ndugu zangu tushirikiane kwa pamoja kuyaenzi kwani maji ni
uhai,”alisema.
Pia amefafanua kuwa kabla ya
Mradi huo kukamilika wananchi walikuwa wakitumia maji yasiyo salama na
kwamba walinunua ndoo moja ya maji kwa shilingi miatano ambapo kwa Sasa
Lita 20 ya maji itauzwa kwa shilingi 25.
Kaimu mkuu wa mkoa wa Dodoma
,ambaye pia ni Mkuu wa wilaya Patrobas Katambi aliwataka wananchi wa
Nghong’onha kuitunza miundombinu ya maji na kuepuka kuihujumu.
“Tunafahamu Kuna watu hawapendi
maendeleo nataka kuwaambia kila mtu awe mlinzi wa mwenzie ,hakikisheni
pia mnalinda mazingira ya vyanzo vya maji ili kiendelea kufurahia
huduma hiyo,”amesema.
Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini
ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu ,Kazi ,vijana na
Ajira,Mhe.Anthony Mavunde amesema kukamilika kwa mradi huo itakuwa
mkombozi mkubwa kwa wananchi wa eneo hilo ambapo amebainisha kuwa
alikuwa halali usiku na mchana kutafuta mwarobaini wa kutatua kero ya
maji.
“Wakati nasaka kura hapa
nilisema yasipokuja maji Nghong’ona mpaka kufikia mwaka 2020 msinipigie
kura,Moyo wangu ulikuwa unadunda sasa inakaribia 2020 na Maji
bado,nililuwa silali napita hapa na pale kuhakikisha tatizo la uhaba wa
maji linatatuliwa,lakini sasa imekuwa historia tujivunie tatizo hili ni
la muda mrefu .amesema.
Kwa upande wao Baadhi ya
Wananchi wa kata hiyo wamesema uzinduzi wa Mradi huo wa maji utawasaidia
kuepukana na kero kubwa ya adha ya maji ya kutembea umbali mrefu
kutafuta huduma hiyo ambapo awali ndoo moja walikuwa wananunua kwa
Tsh.300 hadi 400 lakini sasa watakuwa wananunua kwa Tsh.25 tu kwa ndoo
katika mradi huo hali ambayo itapunguza ukali wa Maisha.
Jumla ya wakazi 10500 wa Kata ya Nghong’onha wanatarajiwa kunufaika na Mradi huo.
No comments:
Post a Comment