Saturday, September 28, 2019

TANGAZO LA MKUTANO WA WADAU WA TASNIA YA KOROSHO NCHINI WA MWAKA 2019/2020


Bodi ya korosho Tanzania, inapenda kuwaarifu wadau wote wa Tasnia ya Korosho nchini kuwa Mkutano Mkuu wa Wadau wa Mwaka2019 utafanyika tarehe 03 Oktoba, 2019 kuanzia saa 2:30 asubuhi katika ukumbi wa mikutano wa Benki kuu Tanzania(BOT) Jijini Dar es Saalam.

Mgeni Rasmi katika mkutano huo anatarajiwa kuwa Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Ngailonga Hasunga(Mb). Pamoja na mambo mengine katika mkutano huo,mada mbalimbali zitawasilishwa zikiwemo zinazohusu maendeleo ya Tasnia ya Korosho hapa nchini.

Waalikwa wanaombwa wajigharanie kuhudhuria Mkutano huo muhimu kwa usafiri,malazi,chakula na kadhalika.Bodi ya Korosho Tanzania itagharamia chakula na viburudisho wakati wa Mkutano.

Barua rasmi za mwaliko zitatumwa kwa waalikwa wote. Wadau waliopata mwaliko rasmi ndiyo wanaokaribishwa Mkutano huo.Wale ambao hawana mwaliko rasmi wa Bodi ya Korosho Tanzania hawataruhusiwa kushiriki kwenye Mkutano na Bodi haitahusika na usumbufu utakaowapata

Hivyo inasisitiza kuwa, kila mshiriki afike na barua yake ya mwaliko.

Tagazo hili limetolewa Na;

FRANSIS ALFRED
KAIMU MKURUGENZI MKUU,
BODI YA KOROSHO TANZANIA
S. L.P 533,
MTWARA

No comments:

Post a Comment