Naibu Waziri wa Nishati, Subira
Mgalu (wa nne kushoto) akiwasha umeme katika Kijiji cha Gasuma wilayani
Bariadi, Mkoa wa Simiyu.
Baadhi ya wananchi katika Kijiji
cha Gasuma wilayani Bariadi wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu
wakati alipofika kijijini hapo kuwasha umeme.
Baadhi ya wananchi, wilayani
Itilima, Mkoa wa Simiyu wakimlaki Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu
alipofika wilayani humo kuwasha umeme katika Kijiji cha Mwamanyangu na
Mwanunui.
Na
Hafsa Omar
Naibu
Waziri wa Nishati, Subira Mgalu ameziagiza taasisi za Serikali zenye madeni ya
umeme zihakikishe kuwa zinalipa madeni hayo kwa Shirika la Umeme Tanzania
(TANESCO), ili Shirika hilo liendelee kutoa huduma bora kwa watanzania wote.
Alitoa
agizo hilo Septemba 17 mwaka huu, wakati alipokuwa akizungumza na wananchi wa
kijiji cha Gasuma, wilaya ya Bariadi, Mkoa wa Simiyu wakati alipoenda kuwasha
umeme kwenye kijiji hicho.
Aidha,
Naibu Waziri alisema kuwa, Shirika hilo limepewa jukumu la kusaidiana na Wakala
wa Nishati Vijijini (REA), kusambaza umeme katika maeneo yote ambayo bado
hayajafikiwa na umeme nchini ifikapo Juni 2021 hivyo ikiwa wateja wake
hawatalipa madeni yao ndani ya muda stahiki, Shirika hilo halitafanya kazi kwa
ufanisi.
“Meneja
wa Mkoa, endelea kuchukua hatua za kisheria, nimeona tayari
umeshaanza kuchukua hatua hizo, lakini hazitoshi deni linazidi kukua endelea
kuwachukulia hatua wale wote ambao hawajalipa madeni yao.’’Alisema Mgalu
Pia
aliwaagiza, Wakuu wa Wilaya kulichukua suala hilo la madeni ya
umeme kwenye taasisi za Serikali kama moja ya ajenda zao katika vikao
vyao vya kila siku, kwani madeni yao yanaweza kusababisha Shirika hilo
likashindwa kujiendesha lenyewe.
Alifafanua
kuwa, kwa sasa Shirika hilo linajitegemea lenyewe na halipokei ruzuku tena
kutoka Serikalini na Wizara ya Nishati haitaki kuona Shirika hilo linafikia
hatua ya kuomba tena ruzuku ili kujiendesha.
Kuhusu
mahitaji ya umeme katika Mkoa wa Simiyu, alisema kuwa, mkoa huo unahitaji umeme
wa kutosha ili kutimiza lengo la Mkoa la ujenzi wa viwanda hivyo katika mwaka
huu wa fedha, Serikali imeamua kujenga kituo cha kupoza umeme, kazi ambayo
imekwishaanza.
‘Mkoa
huu ni mkoa unaojenga viwanda, kwahiyo mahitaji yanaongezeka, umeme
uliopo hautatosha lazima tujenge kituo cha ambacho kwakweli kitaweza kupokea
umeme na kupooza na kusambaza katika maeneo mengine na kazi hiyo
imeanza.’’Alisema Mgalu
Katika
ziara yake mkoani Simiyu, Naibu Waziri pia aliwasha umeme katika vijiji vya
Mwamanyangu na Mwanunui katika wilaya ya Itilima
No comments:
Post a Comment