Thursday, September 19, 2019

SHILINGI BILIONI 179 ZA WADAU WA MAENDELEO KUPELEKA UMEME VIJIJINI



 Baadhi ya Wananchi katika Kijiji cha Mwamanenge wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu wakati alipofika Kijijini hapo kuwasha umeme.


 Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akiwasha umeme katika Kijiji cha Mwamanenge wilayani Maswa mkoa wa Simiyu

 Mwananchi katika Kijiji cha Mwamanenge, Rahel Daniel  ambaye nyumba yake iliwashiwa umeme na Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (kulia) akishukuru juhudi za Serikali kupeleka umeme Kijijini hapo.

 Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, akifurahi mara baada ya kuweka jiwe la Msingi katika Shule ya Sekondari Simiyu iliyopo wilayani Bariadi, baadhi ya vyumba vya madarasa kwenye shule vimejengwa na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).

....................
Imeelezwa kuwa, zaidi ya shilingi bilioni 179 zilizotolewa na Wadau wa Maendeleo kama vile nchi za Norway, Sweden, Jumuiya ya Umoja wa Ulaya (EU)  na Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD) zinatarajia kutumika katika mradi wa usambazaji umeme wa ujazilizi ambapo vitongoji  zaidi ya 1103 vinatarajia kufaidika katika mikoaTisa nchini.
Hayo yalielezwa na Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu,  Septemba 18, mwaka huu wakati alipokuwa akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mwamanenge, Wilaya ya Maswa, Mkoa wa Simiyu kabda hajawasha umeme.
Mikoa itakayofaidika na mradi huo ni Kilimanjaro, Mbeya, Dodoma, Tanga, Pwani, Shinyanga, Mwanza, Singida na Tabora.
Alisema, Serikali imeleta umeme wa bei nafuu nchini ili kuleta usawa katika utoaji huduma kwa wananchi wenye vipato tofauti na kwamba wananchi wote waliopitiwa na miondombinu ya umeme watapatiwa nishati hiyo.
“Kwa upande wa Wilaya ya Maswa, matarajio yetu ni kuwa, mapema mwaka 2021 vijiji vyote vya Maswa takriban 125 vitakuwa vimeshaunganishiwa umeme, tumesema hatuchangui nyumba, nyumba zote zitawekewa umeme.” Alisemaa Mgalu
Naye mwananchi wa Kijiji cha Mwamanenge, Rahel Daniel  ambaye nyumba yake iliwashiwa umeme, aliishukuru Serikali kwa kuwajali wananchi wa kipato cha chini kwa kuwawekea bei ya umeme ya shilingi 27,000 ambayo hata wao wameweza kuimudu na alimhakikishia Naibu Waziri kuwa, ataitumia huduma hiyo ya umeme kujiendeleza kiuchumi.
 Naibu Waziri pia aliweka jiwe la msingi katika shule ya sekondari Simiyu iliyopo wilayani Bariadi ambayo  Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limejenga baadhi ya vyumba vya madarasa na aliwaasa   wanafunzi hao kusoma kwa bidii na watumie fursa ya umeme kujisomea haswa katika nyakati za usiku.

No comments:

Post a Comment