……………………..
Na.Alex Sonna,Chamwino
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo,amesema kuwa
Serikali inatarajia kutoa jumla ya Sh bilioni 33.5 kwa ajili ya kujenga
wodi katika hospitali 67 Mpya za wilaya zinaoendelea kujengwa nchini
kote.
Waziri Jafo ameyasema leo wakati
wa ziara ya kukagua ujenzi hospitali ya Wilaya ya Chamwino inayojengwa
kijiji cha Mlowa Barabarani iliyopo jijini Dodoma
Waziri Jafo amesema kuwa Rais John
Magufuli ametoa shilingi milioni 500 kwa kila hospitali za wilaya
zilizojengwa ili zitumike kujenga wodi za kulaza wagonjwa.
Mhe.Jafo amefafanua kuwa fedha
hizo hatazitoa mpaka mnihakikishie kuwa ujenzi wa majengo saba
yanakamilika kwa asilimia 100, najua endapo fedha zitatolewa mapema watu
wanaweza ‘kuhamisha goli’ (kuzitumia kwa matumizi mengine).
”Mkishamaliza majengo ya awali kwa asilimia 100 fedha hizo nitawapa”Waziri Jafo
Aidha Mhe.Jafo amesema kuwa
ameridhishwa na hatua ya ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Chamwino na
kutaka umaliziaji ukamiliki kwa wakati.
” Naona mlipofika nimeridhishwa na
hatua hii japo kuwa mmechelewa, hali ambayo mlikuwa nayo awali ilikuwa
mbaya hivyo viongozi tusingesimamia kwa karibu mpaka sasa kungekuwa
hakuna kitu.” Amesema Mhe.Jafo
Mhe.Jafo amemtaka Mhadisi mshauri
kuhakikisha kuwaa anasisimami kwa karibu umaliziaji uliobaki ili kusiwe
na kasoro ambazo zinaweza kuharibu kazi nzuri iliyofanyika.
Awali Mkurugenzi wa Halmashauri ya
Wilaya Chamwino, Athuman Masasi amesema kuwa walipokea Sh bilioni 1.5
na kutumia Sh bilioni 1.438 tangu kuanza ujenzi huo Februari mwaka huu
na kubakiwa na Sh milioni 61.
” Ujenzi wa majengo haya umefikia zaidi ya asilimia 80 na tuko katika hatua za umaliziaji”amesema Masasi
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa
Dodoma, Dk Binilith Mahenge ametoa pongezi kwa Serikali na kuihakikishia
kuwa huduma za afya zinaimarika katika mkoa wa Dodoma, huku pia akisema
kuwa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) linatarajia kuingiza umeme
katika majengo hayo kuanzia wiki ijayo.
” Mkandarasi aliyepewa kazi ya
kufikisha umeme wa REA ndiye atakayeingiza umeme kwenye majengo yetu
haya na kazi hii inaanza wiki ijayo.”amesisitiza Dk.Mahenge
No comments:
Post a Comment