Mkurugenzi wa Manispaa ya
Sumbawanga James Mtalitinya ameendelea kuwahamasisha vijana, wanawake na
watu wenye ulemavu kuhakikisha wanajiunga katika vikundi ili kuweza
kupata fursa ya kupewa mikopo ili kuweza kujiajiri hali itakayopelekea
kupunga wimbi la wasio na ajira na hatimae kujiongezea kipato.
Amesema kuwa moja ya majukumu ya
Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga ni kutoa mikopo ya asilimia 10 kwa
wanawake, vijana na watu wenye ulemavu na kuongeza kuwa katika mwaka wa
fedha 2018/2019 halmashauri ilitoa shilingi milioni 253 na kusisitiza
kuwa bado kuna milioni 32 zilizovuka mwaka ambapo kwa mwaka wa fedha
2019/2020 halmashauri inatakiwa kutoa shilingi milioni 230.
“Kufikia Mwezi wa 10 tarehe 15
tunategemea kutoa kiasi cha shilingi milino 120 ikiwa ni makusanyo ya
robo ya kwanza kwa maana ya Julai – Septemba, kwahiyo tunaomba wananchi
wa bangwe pamoja na wananchi wa Sumbawanga wajiunge katika vikundi
visivypongua watu watano mpaka kumi halafu waainishe shughuli
wanayofanya na waje waombe mkopo wa kiasi chochote, tutawakagua na baada
ya hapo tutawapatia mkopo,” alimalizia.
Ameyasema hayo wakati wa ziara ya
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo walipokuwa wakitembelea masoko
yaliyopo katika mji wa Sumbawanga ili kujionea hali halisi ya maendeleo
ya biashara na kujua changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo wananchi
katika masoko hayo.
No comments:
Post a Comment