Aliyekuwa Katibu Mkuu, Ofisi ya
Waziri Mkuu (Bunge na Waziri Mkuu), Bi. Maimuna Tarishi, akimkabidhi
taarifa ya makabidhiano ya Ofisi hiyo, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu
(Sera na Uratibu), Bi. Dorothy Mwaluko, tarehe, 9 Septemba, 2019, Jijini
Dodoma.
Aliyekuwa Katibu Mkuu, Ofisi ya
Waziri Mkuu (Bunge na Waziri Mkuu), Bi. Maimuna Tarishi, (kushoto) akiwa
na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu), Bi. Dorothy
Mwaluko, (kulia) wakifuatilia shughuli za ujenzi zinazoratibiwa na Ofisi
hiyo, wakati wa kumkabidhi miradi ya Ujenzi aliyokuwa anairatibu,
tarehe, 9 Septemba, 2019, Jijini Dodoma.
………………..
Aliyekuwa Katibu Mkuu Ofisi ya
Waziri Mkuu (Bunge na Waziri Mkuu), Bi. Maimuna Tarishi, ambaye
amehudumu katika ofisi hiyo tangu, tarehe 4 Aprili, 2017, amestaafu
rasmi utumishi wa umma, huku akiwashauri watumishi wa umma wanaobaki
katika utumishi huo kutekeleza majukumu ya utumishi wa umma kibiashara.
“Ninapozungumzia Utumishi wa Umma
wa kibiashara siimanishi kuuza na kununua bidhaa fulani, kimsingi
ninachokusudia hapa ni kuwa watumishi wa umma wanaobaki katika utumishi
huo nawashauri utendaji wao wa majukumu uwe unajikita katika kuwezesha
na sekta nyingine zinastawi ili kupata matokeo chanya yaliyokusudiwa kwa
watanzania wanao wahudumia” amesema Tarishi
Bi.Tarishi amefafanua kuwa katika
kuhakikisha kuwa utumishi wa umma wa kibiashara unatekelezwa lazima
watumishi wa umma watekeleze majukumu yao kwa wakati na kasi
inayotakiwa, kutumia weledi na ubunifu pamoja na kuzingatia sheria,
kanuni na taratibu pia kuhakikisha viwango bora vya huduma na lazima
matokeo chanya yanapatikane kwa huduma wanazo zitoa kwa wananchi.
Akiongea wakati akiwaaga rasmi,
watumishi wa Ofisi hiyo, tarehe 9 Septemba 2019, jijini Dodoma,
Bi.Tarishi alieleza kuwa utumishi wa umma ndiyo injini ya kufanyika kwa
shughuli zote katika nchi yoyote duniani. Ameeleza kuwa bila utumishi wa
umma sekta nyingine zikiwemo sekta binafsi haziwezi kustawi, hivyo
utumishi wa umma ukitekelezwa kibiashara huduma zinazotolewa na
serikali zitawafikie wananchi wanao wahudumia na zitakuwa na matokea
chanya.
Katika hatua nyingine, Bi Tarishi
amemshukuru Rais wa Jamhuri yas Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli kwa kumuamini na kumpa dhamana ya kulitumikia Taifa kwa nafasi
ya Katibu Mkuu, Aidha, amemshukuru Mhe. Waziri Mkuu, Mhe. Kassim
Majaliwa, kwa miongozo na maelekezo yaliyomsaidia kutekeleza majukumu
yake. Bi Tarishi hakusita kushukuru ushirikiano mzuri aliopata kutoka
kwa Mawaziri wa Nchi wa Ofisi hiyo, Mhe. Jenista Mhagama na Mhe.
Angellah Kairuki pamoja na Katibu Mkuu anayeendelea kuhudumu kwenye
ofisi hiyo, Bi. Dorothy Mwaluko, pia na watumishi wa ofisi hiyo.
Akiongea katika mkutano huo,
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu), Bi. Dorothy Mwaluko
alifafanua kuwa watumishi wa Ofisi hiyo hawana budi kuwa wabunifu,
watiifu na waaminifu na kutumia weledi katika kutekeleza majukumu yao
ili kuweza kuhakikisha aliyoyasisitiza Katibu Mkuu mstaafu yanakuwa
katika vitendo.
Katibu Mkuu Mstaafu, Bi
Maimuna Tarishi aliaza rasmi utumishi wake wa umma tarehe 6 Mei, 1985 na
amestaafu utumishi huo tarehe, 7 Septemba, 2017. Awali kabla ya kuwa
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu amewahi pia kuwa Katibu Mkuu Ofisi ya
Rais-TAMISEMI, Wizara ya Maliasili na Utalii, Wizara ya Katiba na
Sheria, Wizara ya Elimu Sayansi na teknolojia kabla ya kuhamia Ofisi ya
Waziri Mkuu (Waziri Mkuu na Bunge) alipostaafia.
No comments:
Post a Comment