Waziri wa Nishati, Dkt. Medard
Kalemani(kushoto) na Mbunge wa Jimbo la Lupembe,Joram Hongoli (kushoto)
wakipitia orodha ya vijiji vilivyopata na visivyopata katika jimbo hilo
ili vile ambavyo bado viweze kupatiwa umeme
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard
Kalemani akizungumza na wanakijiji wa Lole kabla ya kuwasha umeme katika
kijiji hicho katika Halmashauri ya Wilaya ya Njombe, mkoani Njombe.
Baadhi wa wanakijiji wa Lole,
katika Halmashauri ya Wilaya ya Njombe, mkoani Njombe, wakimshuhudia,
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani( haonekani pichani) akiwasha
umeme katika moja ya nyumba za ibada katika kijiji hicho.
Wanakijiji wa Kijiji cha Ninga,
katika Halmashauri ya Wilaya ya Njombe, mkoani Njombe,wakimsikiliza
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani, (hayupo pichani) wakati
akizungumza nao kuhusu mradi wa usambazaji wa umeme vijiji (REA), kabla
ya kuwasha umeme katika kijiji hicho.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard
Kalemani,( kulia) akitoa maelekezo ya kuboresha na kuharakisha
utekelezaji wa mradi wa kusambaza umeme vijiji ( REA) kwa wakandarasi
wanaotekeleza mradi huo wa Kampuni ya JV Mufindi Power Service Ltd na
Hegy Engineering Service Ltd, Shirika na Umeme nchini (Tanesco), na
Wakala wa Nishati vijijini REA.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard
Kalemani, (kushoto) akizungumza na wanakijiji wa kijiji cha Ninga, huku
watoto nao wakimsikiliza kwa shauku ya kupata umeme.
Baadhi ya wanakijiji wa Ninga,
wakipiga pushapu kwa furaha ikiwa ni kuunga mkono juhudi za Rais John
Magufuli ya kuwapatia wananchi maendeleo ikiwemo nishati ya umeme.
……………………..
Na Zuena Msuya , Njombe
Waziri Nishati, Dkt. Medard
Kalemani, amewagiza wakandarasi wanaotekeleza Mradi wa Usambazaji umeme
Vijijini, kuweka miundombinu ya umeme katika maeneo yaliyoidhinishwa na
Serikali za Vijiji kujengwa taasisi za umma kama vile shule, nyumba za
ibada, vituo vya afya pamoja na masoko , hata kabla ya ujenzi kuanza.
Dkt. Kalemani alisema kwa kufanya
hivyo kutarahisisha upatikanaji wa huduma ya umeme katika taasisi hizo
pindi ujenzi wa majengo utakapokamilika hata baada ya mradi wa
usambazaji umeme vijijini kukamilika.
Dkt.Kalemani alitoa agizo hilo,
Septemba 1,2019, wakati akiwasha umeme katika Kijiji cha Lole na Ninga
pamoja na kukagua maendeleo ya mradi wa usambazaji umeme vijijini katika
Halmashauri ya Wilaya ya Njombe mkoani Njombe.
“Wakandarasi wote nchini
mnaotekeleza Mradi wa REA, hakikisheni maeneo yaliyoidhinishwa na
serikali kujengwa taasisi za umma yanawekewa miundombinu ya
umeme,hatutaki kuona taasisi zinajengwa lakini hakuna umeme wakati
tayari mradi wa umeme ulikwishapita katika kijiji husika, hii
itaendeleza azma ya serikali ya kuwapatia wananchi huduma bora zaidi”,
alisema Dkt. Kalemani.
Wakandarasi wanaotekeleza mradi wa
REA, awamu ya Tatu Mzunguko wa kwanza katika Mkoa wa Njombe ni Kampuni
ya JV Mufindi Power Service Ltd na Hegy Engineering Service Ltd,
Kalemani aliweka wazi kuwa
kumekuwa na changamoto kwa taasisi nyingi za umma,Vituo vya Afya pamoja
na nyumba za ibada kukosa umeme na maeneo mengine miundombinu ya umeme
kupita mbali zaidi, hivyo wahusika kushindwa kuunganishwa na huduma hiyo
licha ya mradi wa usambazaji wa umeme vijijini kutekeleza katika maeneo
hayo.
Vilevile alisema baada ya
changamoto hiyo kutokea, wamebaini kuwa taasisi nyingi zilizokosa umeme
ni zile zilizokuwa bado hazijajengwa ama ujenzi wake ulikuwa
haujakamilika, kipindi ambacho wa mradi wa usambazaji umeme vijijini
unatekelezwa.
Waziri wa Nishati. Dkt.Kalemani
alieleza kuwa, maeneo yote yatakayoidhinishwa na serikali kujengwa
taasisi za umma, vituo vya afya na nyumba za ibada lazima yawekewe
miundombonu ya umeme wakati wa utekelezaji wa mradi wa usambazaji umeme
vijiji unaoendelea sasa.
Aidha ameendelea kuwakumbusha
wananchi wote nchini hasa waliopo vijijini kuendelea kulipia shilingi
27,000 ikiwa ni gharama ya kuunganishiwa umeme pia kutandaza nyaya
katika nyumba zao kurahisisha zoezi la kuwaunganishia umeme
utakapowafikia.
Aliendelea kusisitiza kuwa
serikali imetumia gharama kubwa kuhakikisha mradi huo unawafikia na
kuwanufaisha wananchi wote hasa wale walio vijijini kwa gharama nafuu,
hivyo haitakuwa busara endapo walengwa wa mradi huo watashindwa
kuchangamkia fursa hiyo.
Waziri Kalemani, alisesema hadi
kufikia Januari, 2020,tayari vijiji vyote vilivyokuwa katika mpango wa
kupata umeme wa mradi wa REA awamu ya tatu Mzunguko wa kwanza vitakuwa
tayari vimeunganishiwa umeme nchini kote na kuendelea na REA mzunguko wa
tatu awamu ya pili ambao ukomo wake ni Juni, 2020.
No comments:
Post a Comment