Menejimenti ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na
Watumishi kutoka Ofisi ya Rais Tawala na Serikali za Mitaa na Idara
maalum ya Zanznibar wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa Mhe. Selemani Jafo wakati akifungua kikao kazi
kilichofanyika katika Ofisi za OR-TAMISEMI Jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Mhe. Selemani Jafo
akiongea na menejimenti ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa na Watumishi kutoka Ofisi ya Rais Tawala na
Serikali za Mitaa na Idara maalum ya Zanznibar wakati akifungua
kikao kazi kilichofanyika katika Ofisi za OR-TAMISEMI Jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Mhe. Selemani Jafo
wakati akiwa katika picha ya pamoja Watumishi kutoka Ofisi ya Rais
Tawala na Serikali za Mitaa na Idara maalum ya Zanznibar mara
baada ya kufungua kikao kazi kilichofanyika katika Ofisi za OR-
TAMISEMI Jijini Dodoma.
*********************************
Na. Angela Msimbira OR-TAMISEMI
Waziri
Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani
Jafo amesema ili Mamlaka za Serikali za Mitaa ziweze kujiendesha lazima
kuwepo na demokrasia ambapo ugatuaji wa madaraka ni muhimu katika
Mamlaka za Serikali za Mitaa
Ameyasema
hayo leo wakati akifungua Kikao kazi kati ya Menejimenti ya Ofisi ya
Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Watumishi kutoka Ofisi ya
Rais Tawala na Serikali za Mitaa na Idara maalum ya Zanznibar
kilichofanyika katika Ofisi za OR-TAMISEMI Jijini Dodoma.
Mhe.
Jafo amesema katika kuhakikisha wananchi wanapata viongozi bora katika
jamii Ofisi ya Rais TAMISEMI husimamia viongozi wa vijiji wasiopungua
12,000, viongozi wa Mitaa ambao wao wanapatikana katika Majiji, Manispaa
na Halmashauri za Mijiambao ni zaidi ya 4000 na viongozi wa vitongoji
zaidi ya elfu 64.
Amefafanua
kuwa OR-TAMIEMI ni kiungo muhimu katika kusimamia utekelezaji wa sera
mbalimbali zinazoandaliwa na Wizara zote nchini hivyo inaposhindwa
kutimiza majukumu yake, kunakuwepo na ongezeko kubwa la Malalamiko kwa
wananchi.
“Ofisi
ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ni kiungo muhimu katika
Sekta zote ambapo isipotimiza wajibu wake kwa weledi haitatimiza lengo
la Serikali la kuhakikisha uwepo wa maendeleo katika kila sekta nchini”
Amefafanua Jafo.
Amesema
kuwa OR-TAMISEMI ni watekelezaji wa Sera na miongozo mbalimbali
inayotolewa na Wizara za Kisekta kwa kuwa ndio yenye Halmashauri ambazo
hutoa huduma kuanzia ngazi ya kitongoji, kijiji na mtaa lengo likiwa ni
kutatua kero mbalimbali za wananchi.
Amezitaja
Taasisi ambazo zipo chini ya OR-TAMISEMI kuwa ni elimu Kibaha ambayo
inasimamia masuala ya elimu, Taasisi ya Mabasi ya Mwendokasi, Chuo cha
Hombolo ambacho kinaendesha mafunzo kwa ajili ya kutengeneza watumishi
watakaosimamia utendaji kazi katika Mamlaka za Serikali za Mitaa
Mhe.
Jafo amesema ugatuaji wa madaraka hufanyika pia katika Sekta ya Elimu
ambapo kazi ya Wizara ya Elimu ni kutunga Sera na miongozo mbalimbali
wakati OR-TAMISEMI kazi yake ni kusimamia miundombinu ya Elimu kuanzia
ngazi ya Msingi hadi Sekondari lengo likiwa ni kuboresha utoaji wa
elimu nchini.
Hata
hivyo amesema kwa upande wa Sekta ya Afya Serikali imeweza kufanya
mabadiliko makubwa ambapo mpaka sasa Hospitali za Wilaya 67 zinajengwa
na Vituo vya kutolea huduma 352 vimekarabatiwa na kujengwa katika
Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini.
Amewataka
watumishi kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Serikali za Mitaa na Idara
maalum kutoka Zanzibar kujifunza kazi zinazofanywa na Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tanzania Bara ili waweze kufanyia
kazi yale ambayo watayapata katika kikao kazi hicho.
Wakati
huohuo Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
Mhandisi Joseph Nyamhanga amewapongeza watumishi hao kwa kuamua
kujifunza kuhusu ugatuaji wa madaraka katika Mamlaka za Serikali za
Mitaa lengo likiwa ni kubadilishana uzoefu katika majukumu ili kuleta
mabadiliko katika jamii.
Naye
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Tawala na Serikali za Mitaa na Idara
Maalum Zanzibar Mhe. Shamata Khamisi amesema kuwa lengo la ujio wao ni
kubadilishana uzoefu kwa kuwa Zanzibar imeanza kupeleka majukumu kwa
wananchi ikiwa ni ugatuaji wa madaraka.
Amesema
kuwa kwa upande wa Zanzibar utekelezaji wa Sera ya ugatuaji wa madaraka
inatakribani miaka miwili ambapo yapo mafanikio ambayo yanaonekana
hivyo ni wajibu wetu kuja kujifunza zaidi juu ya ugatuaji wa madaraka
ili kuweza kuendelea kutoa huduma bora kwa jamii.
No comments:
Post a Comment