Na.Alex Sonna,Dodoma
BUNGE limeelezwa kuwa hakuna
ubaguzi wowote katika utoaji wa mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu
kwani hutolewa kwa wanafunzi watanzania wote wenye uhitaji na walioomba
mikopo wa kuzingatia sheria taratibu na vigezo vilivyowekwa.
Hayo yamesemwa leo bungeni na
Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha wakati
alipokuwa akijibu swali la mbunge wa Viti maalum (CCM) Halima Bulembo
ambapo alisema kuwa ni vema waombaji wakazingatia maelekezo yanayotolewa
na bodi wakati wa uombaji wa mikopo ikiwa ni pamoja na kujaza taarifa
zao kwa usahihi na kuambatanisha nyaraka zote muhimu.
Katika swali lake Mbunge Halima amesema kuwa Je,ni kwanini mikopo ya wanafunzi wa chuo kikuu imekuwa ikitolewa kwa ubaguzi.
Akijibu swali hilo Mhe.Ole Nasha
amesema kuwa mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu hotolewa kwa mujibu wa
sheria ya bodi ya mikopo (sura 178) ambayo inabainisha sifa za msingi.
Sifa hizo ni pamoja na awe
mtanzania aliye dahiliwa katika masomo ya shahada katika taasisi
inayotambuliwa na serikali,na asiwe na vyanzo vingine vinavyogaramia
masomo yake,na kwa mwanafunzi anayeendelea na masomo awe amefaulu
kuendelea na masomo katika mwaka unaofuata.
“Kwa mujibu wa sheria ya bodi ya
mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu,bodi inamamlaka ya kuweka utaratibu
wa kubaini wahitaji,hivyo bodi huandaa mwongozo unaoweka masharti kwa
waombaji pamoja na maelekezo juu ya mambo muhimu ya kuzingatiwa kwa
waombaji ambao yatima,wenye ulemavu au wenye wazazi wenye ulemavu,na
wale ambao masomo yao ya sekondari au stashahada yalifadhiliwa na
maelekezo hayo ni pamoja na kuambatanisha uthibitisho wa hali
zao”amesisitiza
No comments:
Post a Comment