Tuesday, September 17, 2019

DKT TULIA AAHIDI KUPIGA JEKI MIUNDOMBINU YA SOKO DOGO LA DARAJANI JIJINI MBEYA


 



Leo Septemba 17, 2019 Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson amezindua rasmi tawi la Wakereketwa wa Umoja wa Wanawake wa CCM Tanzania (U.W.T) Kata ya Ruanda, mkoani Mbeya.

Tawi hilo limezinduliwa ikiwa ni sehemu ya uimarishaji wa Chama Cha Mapinduzi Mkoani Mbeya na katika eneo hilo la Ruanda pia ni Wafanyabiashara wa soko dogo la Darajani tawi la Mkapa.

Akizungumza wakati akifungua Tawi hilo la wakareketwa wa UWT Kata ya Ruanda Dkt Tulia ameahidi kuwasaidia kuboresha miundombinu iliyo mibovu katika soko hilo pamoja na kuwawezesha kupata mikopo yenye riba nafuu ili kuwawezesha kuendeleza biashara zao kwa ufanisi mkubwa.

 “Ndugu zangu wamesoma risala hapa yenye changamoto kubwa mbili ambazo ni pamoja na ubovu wa miundombinu haswa katika kipindi cha mvua, niwaahidi kwamba tutasaidiana kuezeka vizuri eneo hili ili kuondoa changamoto hiyo” Alikaririwa Dkt Tulia na kuongeza kuwa

“Changamoto ya pili imetajwa ni kukosekana kwa mikopo yenye riba nafuu, nitawaagiza wafanyakazi wa taasisi ya Tulia Trust waje hapa ili waweze kuwasikiliza, kuwashauri na kuwawezesha kupata hiyo mikopo ili msipate tena kikwazo chochote cha kuwawezesha kufanya biashara zenu”- Alisema

MWISHO

No comments:

Post a Comment