Friday, September 20, 2019

AfriFARM waja na Technolojia ya kupambana na kiwavijeshi Vamizi

Wajumbe wa mkutano wakiwa katika ukumbi wa mikutano wa Kilimo IV Uliopo wizara ya kilimo mkoani Dodoma  mara baada ya wasilisho la mfumo wa AfriFarm  wakichangia maoni yao katika kuboresha mfuo huo uliofanyika hivi karibuni
Wajumbe wa mkutano wa kujadili  mfumo wa AfriFarm wakiwa katika picha ya pamoja nje ya ukimbi wa kilimo IV mkoani Dodoma hivi karibuni

Na Bashiri Salum, Wizara ya Kilimo-Dodoma                                           

Shirika la Kimarekani linalojihusisha na miradi mbalimbali ya kilimo na elimu (project concern international) PCI leo wamewasilisha  matokeo ya matumizi ya mfumo wa Afrifarm katika kupambana na kiwavijeshi vamizi fall armyworms katika mkutano uliofanyika kwenye ukumbi  wa mikutano wa Kilimo IV Uliopo Dodoma na kuhusisha wataalamu mbalimbali na baadhi ya viongozi wa Wizara ya Kilimo .

Mfumo huo ambao hutumika Zaidi kwenye simu ganja uliogunduliwa na Shirila la PCI kwa lengo la kupambana na  kiwavijeshi vyamizi katika Mkoa wa Mara ikihusisha kutoa mafunzo ya utambuzi wa kiwavijeshi vamizi (FAW identification) ,ukaguzi wa mashamba,  FAW field scouting  na kutoa taarifa za kiwango cha mashambulizi katika ngazi ya jamii husika

Akiongea wakati wa ufunguzi wa kikao hicho mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya kilimo ambaye ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Sera na  Mipango sehemu ya Ukusanyaji wa Taqwimu Bwana… ..Rubboa amesema shirika hilo kwa kushirikiana na Kitengo cha Huduma ya Afya ya Mimea (PHS) chini ya Wizara ya Kilimo, Kampuni ya Dimag walifikia hatua kubwa ya kuvumbua mfumo huo wakielekitroniki unaoitwa AfriFARM, (Africa fall armyworm Response   Mechanism).

Akiuelezea mfumo huo Bwana Luboa amesema kwamba AfriFARM ni mfumo wa simu (mobile phone application) uliobuniwa  ili kumuwezesha Afisa ugani  au mkulima kujifunza juu ya ufahamu wa kiwavijeshi  vamizi, ukaguzi wa shamba na mbinu mbalimbali za kukabiliana na uvamizi huo.

Aidha shirika la PCI  limewekeza katika kukuza matumizi ya teknolojia ambapo lilifanya majaribio katika Kata  45 zilizoko katika wilaya ya Butiama, Bunda na Musoma vijijni katika Mkoa wa Mara ambako kulipata athari ya visumbufu vamizi alisema Bwana luboa.

Hata hivyo Bwana Rubuo ametoa wito kwa wataalamu walioshiriki katika mkutano huo kuahakikisha wanatoa michango yao katika kuimarisha mfumo huo ambao utasaidia kuimarisha usalama wa chakula hapa nchini.

Naye Meneja wa Idara ya Kilimo Bwana Amithay Kuhanda Amesema wameshirikiana na Wizara ya Kilimo katika kupambana na kiwavijeshi vyamizi ambao wanachangia kushusha kiwango cha uzalishaji wa mazao ya wakulima.

Anasema kuwa wanapambana na kiwavijeshi kwa kutumia mfumo wa kielektroniki simu janja ambao una saidia kufanya ufutiliaji wa mashamba yaliovamiwa na kiwavijeshi na kutoa taarifa kupitia mfumo wa simu hiyo.

Mfumo huu unafanya kazi zaidi kuanzia ngazi za Kata kufikisha taarifa ngazi ya wilaya kwa haraka zaidi hiyo kusaidia kutoa taarifa sahihi za maeneo ambayo yameathirika kwa hatua zaidi.

Mchango washirika hili la PIC ni kuandaa mfumo ambao unasaidia kuwa tambua viwavijeshi na kufikisha taarifa haraka kwa wataalamu na watoa maamuzi kwa maaana ya serikali alisema bwana Amithay Kuhanda.

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya uendelezaji wa mazao Bwana ….Malema amelishukuru shirika hilo kwa hatua walizochukua za kupambana na viwavijeshi vamizi na kuahidi kutoa ushirikiano mkubwa ili kuhakikisha huduma hiyo inatumika katika mikoa mingi Zaidi.

Bwana malema amesema kwamba mfumo huo utasaidia kupunguza gharama za ufuatiliaji na ambazo kwa kiasi kikubwa zilichangia visumbufu  hao kuenea kwa kasi katika maeneo mengine

Hata hivyo alimalizia kwa kuwataka wataalamu kujifunza tekinolojia hii ili kuwasaidia wakulima na kupunguza changamoto ya usafriri katika maeneoa mbayo yalikuwa hayafikiki kwa urahisi .

Naye kaimu Mkurugenzi wa huduma ya Afya ya mimea Bwana   Jubilant Mwangi amelishukuru Shirika la PCI kwa kujana mfumo wa AfriFarma mbao utawasaidia sana wakulima .

Ameshauri mfumo huu kutumika maeneo mengi Zaidi hapa nchini kwa ajili ya kusaidia kupunguza upotevu wa chakula ambao unaweza kusababisha hasara kwa wakulima wengi

Aidha amewataka wakulima wote nchini kutumia mbinu husihi kama IPM  mbinu husishi ya visumbufu na kuwa na mitego ambayo itawakamata kuliko kuongeza matumizi ya madawa yenye kemikali ambayo yanasababisha kushuka kwa soko la bidhaa husika alisema bwana Jubilant Mwangi.

MWISHO

No comments:

Post a Comment