Waziri wa Nishati, Dkt Medard
Kalemani, akizungumza na wananchi katika Kijiji cha Mabundulu wilayani
Urambo, Mkoa wa Tabora wakati alipofika kijijini hapo kuwasha umeme.
Wengine ni viongozi mbalimbali kutoka wilayani Urambo.
Waziri wa Nishati, Dkt Medard
Kalemani (mwenye shati la bluu) akikagua mradi wa umeme katika Kijiji
cha Mabundulu wilayani Urambo, Mkoa wa Tabora wakati alipofika kijijini
hapo kuwasha umeme. Wengine ni viongozi mbalimbali kutoka wilayani
Urambo na wananchi.
Waziri wa Nishati, Dkt Medard
Kalemani (katikati) akikata utepe kuashiria uwashaji umeme katika Kijiji
cha Mabundulu wilayani Urambo, Mkoa wa Tabora. Wa Pili kushoto ni
Mbunge wa Urambo, Margaret Sitta.
Waziri wa Nishati, Dkt Medard
Kalemani (wa tatu kushoto), akitoa maelekezo wa wataalam wa TANESCO
wanaosimamia ujenzi wa kituo cha kupoza umeme cha Urambo ambacho
kinajengwa chini ya mradi wa njia ya kusafirisha umeme kutoka Tabora
hadi Kigoma.
………………..
Na Hafsa Omar, Tabora
Waziri
wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani amemuagiza Meneja wa Shirika la umeme
Tanzania (TANESCO), Mkoa wa Tabora, kuwa vijiji vyote vinavyozunguka
mradi wa ujenzi wa kituo cha kupoza umeme cha Urambo, vipatiwe umeme
ndani ya miezi Sita.
Alisema
hayo Agosti 24, 2019 wakati alipofanya ukaguzi kwenye mradi wa Ujenzi
wa njia ya kusafirisha umeme kutoka Urambo, Tabora hadi Kigoma na
kuzungumza na wananchi katika kijiji cha Uhuru kata ya Vumilia wilayani
humo.
Akizugumza
na wanachi wa kijiji hicho, Waziri Kalemani alisema “huwezi ukajenga
kituo cha kupoza hapa, halafu vijiji vilivyozunguka hapa visiwe na
umeme, kwahiyo vijiji vyote vinavyozunguka kituo hiki natoa miezi Sita
viwe vimeunganishiwa umeme.”
Aidha,
Dkt. Kalemani aliwapongeza wananchi wa Wilaya hiyo kwa uvumilivu wao
katika kipindi chote kwa kutopata umeme wa uhakika na kueleza kuwa
“mmehangaika miaka mingi lakini, Serikali yenu ni sikivu ndiyo maana
sasa inaleta umeme imara unaotabirika, na ninampongeza sana Mheshimiwa
Rais Magufuli kwa kutoa fedha za kutosha za kujenga mradi huu.”
Vilevile
Dkt. Kalemani alisema kukamilika kwa mradi huo kutaokoa pesa nyingi
zinazotumika kununua mafuta kwa ajili ya kuendeshea mitambo ya umeme.
Alitoa
mfano kuwa, Mkoa wa Kigoma unatumia takribani shilingi bilioni 1.1 kwa
mwezi kuendesha mitambo ya mafuta ambapo kwa mwaka inatumika bilioni
13.2 hivyo umeme wa gridi utaokoa fedha hizo.
Alieleza
kuwa, mradi huo wa njia ya kusafirisha umeme unatekelezwa na TANESCO
wenyewe na hawatatumia wakandarasi wa nje ya nchi.
Katika ziara hiyo, Dkt Kalemani aliwasha umeme katika kijiji cha Madundulu tarafa ya Usoke, wilayani Urambo.
No comments:
Post a Comment