Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.
Anthony Mtaka akizungumza na Wadau mbalimbali wa kilimo cha pamba katika
ufunguzi wa Mkutano wa kuboresha Mkakati maalum wa Mapinduzi ya Kilimo
cha Zao la Pamba Mkoa wa Simiyu, katika kipindi cha miaka mitano
2019-2014, uliofanyika Agosti 28, 2019 Mjini Bariadi
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu,
Bw. Jumanne Sagini akizungumza na Wadau mbalimbali wa kilimo cha pamba
katika Mkutano wa kuboresha Mkakati maalum wa Mapinduzi ya Kilimo cha
Zao la Pamba Mkoa wa Simiyu, katika kipindi cha miaka mitano 2019-2014,
uliofanyika Agosti 28, 2019 Mjini Bariadi.
Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Komredi
Kheri James akitoa salamu zake kwa Wadau mbalimbali wa kilimo cha pamba
katika Mkutano wa kuboresha Mkakati maalum wa Mapinduzi ya Kilimo cha
Zao la Pamba Mkoa wa Simiyu, katika kipindi cha miaka mitano 2019-2014,
uliofanyika Agosti 28, 2019 Mjini Bariadi.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu,
Komredi Enock Yakobo akizungumza na Wadau mbalimbali wa kilimo cha
pamba katika Mkutano wa kuboresha Mkakati maalum wa Mapinduzi ya Kilimo
cha Zao la Pamba Mkoa wa Simiyu, katika kipindi cha miaka mitano
2019-2014, uliofanyika Agosti 28, 2019 Mjini Bariadi.
Baadhi ya wadau wa kilimo cha
pamba wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (hayupo
pichani) wakati akifungua Mkutano wa kuboresha Mkakati maalum wa
Mapinduzi ya Kilimo cha Zao la Pamba Mkoa wa Simiyu, katika kipindi cha
miaka mitano 2019-2014, uliofanyika Agosti 28, 2019 Mjini Bariadi.
Baadhi ya wadau wa kilimo cha
pamba Mkoani Simiyu wakifuatilia uwasilishaji wa Mkakati Maalum wa
Mapinduzi ya Kilimo cha Zao la Pamba Mkoa wa Simiyu, katika kipindi cha
miaka mitano 2019-2014, katika Mkutano wa kuboresha Mkakati huo
uliofanyika Agosti 28, 2019 Mjini Bariadi.
Mkurugenzi wa Miradi wa Gatsby
Africa, Samweli Kilua akitoa taarifa ya namna shirika hilo
lilivyoshiriki katika uaandaaji wa Mkakati maalum wa Mapinduzi ya Kilimo
cha Zao la Pamba Mkoa wa Simiyu, katika kipindi cha miaka mitano
2019-2014, kwenye mkutano wa kuboresha mkakati huo uliofanyika Agosti
28, 2019 Mjini Bariadi.
Mkurugenzi wa Miradi kutoka
Shirika la Maendeleo la Umoja wwa Mataifa(UNDP), Amon Manyama akichangia
hoja Mkutano wa kuboresha Mkakati maalum wa Mapinduzi ya Kilimo cha Zao
la Pamba Mkoa wa Simiyu, katika kipindi cha miaka mitano 2019-2014,
uliofanyika Agosti 28, 2019 Mjini Bariadi.
Katibu Tawala Msaidizi Seksheni ya
Mipango na Uratibu katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Donatus
Weginah akiwasilisha mkakati wa maalum wa Mapinduzi ya Kilimo cha Zao la
Pamba Mkoa wa Simiyu katika kipindi cha miaka mitano 2019-2014, katika
Mkutano wa kuboresha Mkakati huo uliofanyika Agosti 28, 2019 Mjini
Bariadi.
Mmoja wa Wawakilishi wa
Wakurugenzi na wamiliki wa Viwanda vya Kuchambua pamba kutoka kiwanda
cha Alliance Ginneries Ltd, akichangia hoja katika Mkutano wa kuboresha
Mkakati maalum wa Mapinduzi ya Kilimo cha Zao la Pamba Mkoa wa Simiyu,
katika kipindi cha miaka mitano 2019-2014, uliofanyika Agosti 28, 2019
Mjini Bariadi.
…………………….
Na Stella Kalinga, Simiyu RS
Katika kukabiliana na changamoto
ya ukosefu wa soko la pamba mkoa wa Simiyu umeandaa mkakati maalum wa
miaka mitano (2019-2024) wa mapinduzi ya kilimo cha zao hilo ili kujibu
changamoto zinazowakabili wakulima wa pamba.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa
wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka katika Mkutano wa Wadau wa Pamba
uliofanyika uliofanyika Agosti 28, 2019 Mjini Bariadi kwa lengo la
kuboresha Mkakati maalum wa Mapinduzi ya Kilimo cha Zao la Pamba Mkoa wa
Simiyu, katika kipindi cha miaka mitano 2019-2014,
Akifungua Mkutano huo Mtaka
amesema upo umuhimu mkubwa kwa Mkoa wa Simiyu kuwa na kiwanda/viwanda
vya kuongeza thamani ya zao la pamba ikiwemo viwanda vya nguo kama
suluhisho la soko la pamba kwa wakulima.
“Kama hatutakuwa na viwanda
vinavyoongeza thamani kwenye pamba,hata kama tukiongeza uzalishaji,
itafika mahali tutatukanana tu, maana pamba itakuwa nyingi na hakuna mtu
wa kukununua na wanaonunua wanajua hatuna kwa kuipeleka, kwa hiyo ni
lazima tukubaliane na ndiyo maana tukasema tuje na mkakati huu unaoanza
na mkulima kuanzia kwenye kulima” alisema Mtaka.
Aidha, Mtaka amesema ili
kuwasaidia wakulima katika upatikanaji wa mikopo ni vema benki zikaweka
utaratibu rafiki wa kutoa mikopo kwa wakulima huku akitoa wito kwa Benki
Kuu kupitia Kurugenzi ya Sera kuandika maandiko ya miradi ya mazao ya
mikakati likiwemo pamba ambayo yatasaidia katika kuyaongezea thamani
mazao hayo.
Akiwasilisha mkakati huo kwa
wadau wa pamba mkoani Simiyu, Katibu Tawala Msaidizi wa Mipango na
Uratibu Mkoa wa Simiyu, Bw. Donatus Weginah amesema uongezaji thamani
kwenye pamba mkoani Simiyu bado liko chini; ambapo kwa sasa
kinachofanyika ni kutengenisha pamba nyuzi, mbegu na kuchuja mafuta,
huku akibainisha kuwa matarajio ya mkoa ni kwenda kwenye hatua nyingine
zaidi ya kuchambua pamba.
Pamoja na kuongeza thamani ya
zao la pamba wadau wa pamba wametoa maoni mbalimbali katika kuboresha
kilimo cha Pamba ili kiwe chenye tija na kubainisha kuwa “Ili tuweze
kuboresha kilimo cha pamba ni lazima teknolojia zitakazokabiliana na
changamoto za mabadiliko ya tabianchi, wadudu na magonjwa” alisema
Epifania Temu kutoka Taasisi ya Utafiti wa Kilimo(TARI) Ukiriguru
“Mbegu ndiyo msingi wa tija ya
pamba inayopaswa kuzalishwa kwenye soko, hivyo kwenye eneo
lililokubaliwa kuzalisha mbegu kama Meatu na Igunga ginners (wenye
viwanda vya kuchambua pamba) watakaokununua pamba ya eneo wapewe jukumu
la kuzalisha mbegu ili kuwa na mwendelezo wa mbegu bora” alisema Mkondo
Cornelius Afisa Kilimo Mkuu, Wizara ya Kilimo.
Mkurugenzi wa Miradi kutoka
Gatsby Africa, Samweli Kilua ametoa wito kwa wadau wote kuhakikisha kila
mdau anatimiza wajibu wake katika kuhakikisha mkakati huo unatekelezwa
kwa ufanisi katika kuboresha kilimo cha pamba.
Akifunga kikao Katibu Tawalawa
Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini amesema mkakati wa mapinduzi ya
kilimo cha pamba Mkoani Simiyu utatekelezwa kwa vitendo na akazitaka
Taasisi za fedha, viongozi na wataalam wanaosimamia wakulima, vyama vya
ushirika na wadau wengine waanze mazungumzo ili mkakati huo
utakapoanza kutekelezwa kuwe na uelewa wa pamoja kwa wadau wote.
Mkutano wa kuboresha mkakati
maalum wa miaka mitano (2019-2024) wa mapinduzi ya kilimo cha pamba
ulijumuisha wadau mbalimbali wa kilimo cha pamba ambao ni pamoja na
viongozi wa Chama na Serikali Mkoa wa Simiyu, Watalaam wa kilimo kutoka
Taasisi za Utafiti wa Kilimo, Wizara ya Kilimo, Halmashauri na Mkoa,
Watendaji wa Taasisi za Fedha, viongozi wa vyama vya msingi vya
ushirika.
No comments:
Post a Comment