Mabingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom
Tanzania bara Simba wameshindwa kusonga mbele katika michuano ya klabu
bingwa Afrika baada ya kutoka sare ya kufungana 1-1 na U Desportiva Do
Songo (UD SONGO) kutoka Msumbiji na kuwatupa nje .Mchezo uliomalizika
kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Wageni walianza kwa kasi dakika za
mwanzo kwa kuwasambuliaji wenyeji huku wakikosa mabao mawili ya wazi
hata hivyo Simba waliamka na kushambaulia kwa nguvu.
Mnamo dakika ya 13 Nahodha wa UD
SONGO aliwanyanyua wageni akifunga bao kwa mpira wa faulo ulioenda moja
kwa moja na kumshinda Aisha Manula aliyeshindwa kupaanga vizuri safu
yake ya ukuta.
Baada ya kufungwa bao hilo Simba
walianza kulishambulia lango la UD SONGO kama nyuki hata hivyo kipindi
cha kwanza hawakuweza kupata bao.
Kipindi cha pili timu zote
zilianza kwa kushambuliana kwa zamu huku zikifanya mabadiliko hata hivyo
wageni waliweza kunufaika zaidi.
Beki kisiki wa timu ya Taifa Stars
Erasto Nyoni,aliisawazishia Simba kwa njia ya mkwaju wa Penalti dakika
ya 85 hata hivyo bao hilo halikuweza kuwa na faida kwa wenyeji.
Hadi dakika 90 za Mwamuzi kutoka
nchini Rwanda Jean Claude Ishimwe,anapuliza kipenga cha mwisho UD SONGO
wamesonga hatua ya 32 na kuwatupa nje Simba ambao msimu uliopita
waliweza kuishia hatua ya Robo Fainali kwa kufungwa na TP Mazembe mabao
4-1.
Tegemeo kwa Tanzania kwa sasa
limebaki kwa timu tatu ambazo zimesonga mbele Yanga bado wapo katika
klabu Bingwa huku kwenye shirikisho Azam FC na Malindi FC kutoka
visiwani Zanzibar
No comments:
Post a Comment