Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo ( wa Mbele) akikagua jengo la
Utawala katika Hospitali ya Wilaya ya Sumbawanga iliyoko katika Kata ya
Mtowisa, bonde la ziwa Rukwa
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo ( wa pili toka kulia)
akiongozana akiongozana na Karani wa Mradi wa ujenzi wa Chuo Cha Ufundi
VETA Mkoani Rukwa Mhandisi Jeremiah Longido wakati wa ukaguzi wa ujenzi
wa chuo hicho.
Baadhi ya majengo ya Chuo Cha Ufundi VETA Mkoani Rukwa
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (wa mbele) pamoja na viongozi
na wataalamu wengine wakitoka katika jengo la Maabara la hospitali ya
Wilaya ya Nkasi.
.................
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amemtaka mkandarasi
wa Kampuni ya Tender International kuhakikisha anamaliza ujenzi wa Chuo cha
Ufundi VETA kilichopo Kata ya Sumbawanga Wenyeji Wilayani Sumbawanga ndani ya mwaka
huu ili kufikia mwezi Januari mwaka 2020 kianze kudahili wanafunzi katika fani
mbalimbali za ufundi.
Chuo hicho ambacho ujenzi wake ulitakiwa kumalizika Septemba
21, 2019 bado haujakamilika kutokana na Mkandarasi huyo kutegemea fedha za
ujenzi kutoka serikalini na hivyo kuomba kuongezewa muda wa miezi minne ili
aweze kumalizia ambapo hadi sasa ameshalipwa shilingi bilioni 2.6 kwaajili ya
ujenzi wa majengo 22 ikiwemo karakana mbalimbali za mafunzo, mabweni, madarasa
na nyumba za watumishi.
Mbali na changamoto hiyo Mh. Wangabo pia amepongeza kiwango
cha ubora wa majengo hayo ambayo kwasasa yapo katika hatua ya kupauliwa na
kuongeza kuwa kama kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa imeridhishwa na kiwango cha
majengo ya chuo hicho hadi hapo kilipofikia.
“VETA hii ilianza kujengwa mwaka jana mwezi wa tisa na ilitegemewa
iwe imemalizika mwaka huu, kipindi cha mwaka mmoja. Lakini kumekuwa na
changamoto za hapa na pale upande wa mkandarasi n ahata upande wa wizara
inayohusika, basi hizi changamoto zimefikia kwenye hatua ambayo sasa tunaweza
kwenda vizuri, Mkandarasi ameomba kuongezewa miezi minne na hii mimi
nitaifuatilia, kuhakikisha kwamba hii ‘extention’ inakwenda haraka ili
ikamilike ili ianze kuchukua wananfunzi Januari 2020,” Alisema.
Ameyasema hayo leo tarehe 29.8.2019 alipotembelea katika
eneo la Ujenzi wa Chuo hicho kinachotarajiwa kudahili wanafunzi 600 wa masomo
ya muda mrefu na wanafunzi 2000 wa masomo ya muda mfupi katika fani za umeme wa
majumbani, umeme wa magari, ushonaji, mapishi, ufundi wa kompyuta, ufundi wa
magari, useremala, na usindikaji wa chakula.
Awali akizungumza wakati wa kutoa taarifa ya ujenzi wa Chuo
hicho karani wa Mradi Mhandisi Jeremiah Longido alisema kuwa endapo serikali
italipa fedha za ujenzi kwa wakati wana uhakika kwamba majengo hayo
yatakamilika katika kipindi hicho cha miezi minne waliyoiomba na hatimae
kufikia mwezi January, 2020 kuanza kudahili wanafunzi.
“Kama ‘Cash flow’ itakwenda vizuri, hii miezi minne kama
kazi itafanyika kwa nguvu tunaweza kumaliza kazi, kwasababi amelipwa ‘certificate’
namba nne ambayo ni kama milioni 130 lakini kuna ‘certificate’ namba tano kama
milioni 640 amabyo ipo tayari ambapo mda wowote anaweza kulipwa kwahiyo kama hiyo
atapokea inamaanisha tutakuwa vizuri,” Alisema.
Katika Hatua nyingine, Mh. Wangabo amesikitishwa na
kasi ya konokono katika ujenzi wa hospitali za Wilaya ambazo kwa mujinbu wa
tarehe za Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, hospitali hizo
ziliongezewa muda wa kuisha kwake na zilitakiwa kumalizika na kukabidhiwa
tarehe 31.8.2019 kwaajili ya kuanza kutumika.
“Kasi yenu ni ndogo, kasi ya konokono, vifaa havipo hata
ujenzi katika jengo hili la utawala hakuna, hali kwakweli ni hovyo na si nzuri
ni mbaya muda umekwishaisha, kwahiyo nashindwa hata kuwaambia kuna siku za
nyongeza kwasababu kuna ‘deadline’ ya TAMISEMI. Sasa fanyeni juu chini kwa siku
zilizobakia mmalize hapa sasa sijui mtaweka hema ama mtafanyaje lakini fanyeni
juu chini hii kazi iishe,” Alisisitiza
Ameyasema hayo baada ya kukagua ujenzi wa hospitali ya
Wilaya ya Sumbawanga akiwa na kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa, viongozi na
wataalamu wa wilaya ya Sumbawanga ambapo kabla ya kufika hapo pia alitembelea
hospitali ya Wilaya ya Nkasi na hospitali ya Wilaya ya Kalambo.
No comments:
Post a Comment