Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu,
Bw. Jumanne Sagini akizungumza na watumishi wa Hospitali ya Halmashauri
ya Mji wa Bariadi, leo Agosti 15, 2019 mjini Bariadi, kwa lengo la
kutoa ufafanuzi juu ya kusitisha uamuzi wa watumishi hao kuchangia
mashine ya ULTRASOUND iliyoibiwa Agosti 05, 2019 ambao ulitolewa na Mkuu
wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga hapo jana .
Watumishi wa Hospitali ya
Halmashauri ya Mji wa Bariadi, wakimsikiliza Katibu Tawala wa Mkoa wa
Simiyu, Bw. Jumanne Sagini leo Agosti 15, 2019 mjini Bariadi, kwa lengo
la kutoa ufafanuzi juu ya kusitisha uamuzi wa watumishi hao kuchangia
mashine ya ULTRASOUND iliyoibiwa Agosti 05, 2019 ambao ulitolewa na Mkuu
wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga hapo jana . .
Baadhi ya Viongozi wa Vyombo vya
Ulinzi na Usalama Mkoani Simiyu wakiwa katika kikao na Watumishi wa
Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Bariadi, leo Agosti 15, 2019 mjini
Bariadi, kwa lengo la kutoa ufafanuzi juu ya kusitisha uamuzi wa
watumishi hao kuchangia mashine ya ULTRASOUND iliyoibiwa Agosti 05,
2019, ambao ulitolewa na Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga
hapo jana.
Watumishi wa Hospitali ya
Halmashauri ya Mji wa Bariadi, wakimsikiliza Katibu Tawala wa Mkoa wa
Simiyu, Bw. Jumanne Sagini leo Agosti 15, 2019 mjini Bariadi, kwa lengo
la kutoa ufafanuzi juu ya kusitisha uamuzi wa watumishi hao kuchangia
mashine ya ULTRASOUND iliyoibiwa Agosti 05, 2019.
Watumishi wa Hospitali ya
Halmashauri ya Mji wa Bariadi, wakimsikiliza Katibu Tawala wa Mkoa wa
Simiyu, Bw. Jumanne Sagini leo Agosti 15, 2019 mjini Bariadi, kwa lengo
la kutoa ufafanuzi juu ya kusitisha uamuzi wa watumishi hao kuchangia
mashine ya ULTRASOUND iliyoibiwa Agosti 05, 2019 ambao ulitolewa na Mkuu
wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga hapo jana . .
Katibu wa Chama cha Wafanyakazi wa
Serikali Kuu na Afya (TUGHE) Mkoa wa Simiyu, Bi. Catherine Nyingi
akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani mara baada ya kikao
cha uongozi wa Mkoa wa Simiyu na Watumishi wa Watumishi wa Hospitali ya
Halmashauri ya Mji wa Bariadi, leo Agosti 15, 2019 mjini Bariadi.
Mtumishi Frola Katoyo akizungumza
na waandishi wa habari hawapo pichani mara baada ya kikao cha uongozi wa
Mkoa wa Simiyu na Watumishi wa Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa
Bariadi, leo Agosti 15, 2019 mjini Bariadi.
………………….
Na Stella Kalinga, Simiyu RS
Uongozi wa Mkoa wa Simiyu kupitia
kwa Katibu Tawala wa Mkoa, Bw. Jumanne Sagini umesitisha uamuzi wa Mkuu
wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga, uliotolewa jana Agosti 14,
2019 ambapo watumishi wote 137 wa Hospitali ya Mji wa Bariadi walitakiwa
kukatwa mishahara yao kwa ajili ya kuchangia fedha ya kununua mashine
ya ULTRASOUND, iliyoibiwa katika wodi ya wazazi hospitalini hapo badala
yake ameagiza vyombo vya dola vifanye uchunguzi kubaini aliyeiba
mashine hiyo na hatua stahiki zichukuliwe.
Sagini ameyasema hayo leo
Agosti 15, 2019 wakati akizungumza na watumishi wa Hospitali ya
Halmashauri ya Mji wa Bariadi katika Ukumbi wa Hospitali hiyo Mjini
Bariadi.
Amesema uongozi wa Mkoa
umetafakari na kuona kuwa si watumishi wote wa hospitali hiyo wamehusika
katika upotevu wa mashine hiyo kwa kuwa wanafanya kazi katika idara
tofauti na baadhi yao siku ya tukio hawakuwepo, hivyo ni vema vyombo vya
dola vikafanya uchunguzi kubaini waliohusika.
” Uongozi wa Mkoa tunarekebisha
baadhi ya hatua zilichukuliwa na Mhe. DC jana, hili jambo haliwezi kuwa
la watumishi wote 137, kama Serikali tunavyo vyombo vya dola ambavyo
kuna watu wanalipwa mishahara kwa kazi hizo za kiuchunguzi, tunataka
kifaa hicho kirejeshwe, vyombo hivi vifanye uchunguzi, vichukue hatua
kwa watakaobainika ikiwemo kupelekwa mahakamani” amesema.
Katika hatua nyingine Sagini
amewataka watumishi wa Hospitali ya Mji wa Bariadi kuimarisha mfumo wa
makabidhiano ya kazi na vifaa vya kazi ili kuwepo na taarifa sahihi za
wagonjwa na vifaa tiba kama utaratibu unavyotaka.
Kwa upande wao watumishi wa
Halmashauri ya Mji wa Bariadi wamewashukuru viongozi wa Mkoa wa Simiyu
kwa kusitisha uamuzi wa awali ambao ungewaathiri kiuchumi na kupunguza
ari ya kufanya kazi hususani wale ambao hawajahusika na upotevu wa
mashine hiyo.
” Tunamshukuru sana kiongozi wetu
kwa msamaha aliotutolea kwa sababu tangu jana tumelala kwa presha baada
ya kuambiwa kuwa kila mtu alip, mimi uwezo wangu mdogo na mshahara
wangu ni mdogo nilikuwa sioni pesa ya kulipa hicho kifaa;namshukuru
Mungu kwa uamuzi wa viongozi wa mkoa yaani naongea kwa uchungu mpaka
nasikia kulia kwa furaha niliyonayo” amesema Frola Katoyo Mtumishi
katika idara ya dawa.
“Nimepokea vizuri uamuzi
uliofanywa na viongozi wetu wa mkoa kwa sababu maanuzi yaliyotolewa jana
kiuhalisia si kila mtumishi alipaswa kuhusishwa kwenye hili, maana
wengine walikuwa likizo, wengine hawakuwepo kazini, hivyo ni sahihi
kabisa kuviachia vyombo vya dola; nina uhakikia kuanzia leo watu
watafanya kazi maana jana utendaji kazi ulipungua baada ya kupata tu
taarifa kuwa wanapaswa kuchangia” alisema Simon Chisomeko Afisa Afya.
Kwa upande wake Katibu wa Chama
cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) Mkoa wa Simiyu, Bi.
Catherine Nyingi amesema Chama hicho kinaushukuru uongozi wa mkoa kwa
kutambua sheria, kanuni na taratibu za Utumishi wa Umma na wameiomba
Serikali iendelee kuwa macho katika kusimamia sheria, kanuni na
taratibu.
Mashine ya kupima magonjwa ya
ndani ya mwili wa Binadamu (ULTRASOUND MACHINE) iliripotiwa kuibiwa
katika Wodi ya wazazi katika Hospitali ya Mji wa Bariadi Agosti 05,
2019 na jana Agosti 14, 2019 Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo
Kiswaga akaagiza watumishi wote 137 wa Hospitali hiyo wakatwe fedha
kwenye mishahara yao ili mashine hiyo iliyoibiwa inunuliwe.
No comments:
Post a Comment