Naibu Waziri wa Madini Stanslaus
Nyongo akitolea majibu kero za wachimbaji wadogo wa madini ya vito
kiegei wilayani Nachingwea. Mwenye Tshirt ya blue na Mtandio ni Katibu
tawala wa Nachingwea Husna Sekibobo anae mwakilisha mkuu wa wilaya hiyo.
Machui Bausi akiwasilisha kero za wachimbaji wa eneo la kiegei kwa Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo kulia kwa mtoa kero.
- Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Liwale Sarah Chiwamba kushoto, akifuatiwa na Katibu Tawala wa Liwale Mbwana Kambangwa na wa kwanza kulia ni Katibu Tawala wa Nachingwea Husna Sekibobo mara baada ya kumaliza mkutano wa pamoja na wachimbaji wadogo
Sehemu ya Wachimbaji wadogo
waliokusanyika kumsikiliza Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo
hayupo pichani aliewasili machimboni hapo kusikiliza na kutatua kero
zao.
………………..
Na Issa Mtuwa “WM” Nachingwea Mtwara
Mgogoro ulio dumu kwa muda mrefu
kuhusu mpaka wa uchimbaji madini uliohusisha eneo (leseni) moja kwenye
ardhi ya halmashauri za wilaya mbili ya Nachingwea na Liwale kila
upande ukiwa na wachimbaji wadogo umetatuliwa na Naibu Waziri wa Madini
Stanslaus Nyongo tarehe 15/08/2019 mara baada ya kufanya ziara katika
eneo hilo na kufanya mkutano na wachimbaji wadogo wa pande zote mbili na
viongozi wa kuu wa wilaya zote mbili.
Mgogoro huo wa mpaka na leseni
umedumu kwa muda mrefu ukiwa na vyanzo viwili vikuu vya mgogoro. Moja,
mgogoro wa eneo ambalo wachimbaji wadogo wananchimba hivi sasa wamedai
eneo hilo lilikuwa la Omar Said Kojogo ambae kwa mujibu wa wachimbaji
wadogo walimlipa fidia ndugu Kojogi ili eneo hilo limilikishwe kwa
jumuia ya wachimbajio wadogo lakini bado walikuwa hawajapatiwa leseni
hiyo kama wamiliki wapya.
“Mhe. Naibu Waziri tatizo la
mgogoro wa leseni hapa bado haujatatuliwa kwa kuwa sisi wenyewe
wanaaporo tulichangishana na kumpa Omar Said Kojogo Tsh. 2,852,000/=
ili leseni hiyo iwe ya wanaaporo (Wachimbaji wadogo) lakini mpaka leo
hatujapatiwa” alisema Machui Bausi.
Chanzo cha pili cha mgogoro huo ni
mgao wa mapato yanayopatikana katika eneo hilo. Kila halmashauri
inataka ichukuwe mapato kitu ambacho kilikuwa kinaleta mvutano nani
anastahili kwa kuwa leseni ya eneo hilo ipo katika halmashauri zote
mbili. za Nachingwea na Liwale zote za mkoa wa Lindi.
Aidha, changamoto nyingine ambayo
wachimbaji wadogo wamemwambia Naibu Waziri ni tatizo la soko la kuuzia
madini ambapo wamemuomba Naibu Waziri kuwasongezea soko la madini katika
eneo hilo ili kuwaondolea ushawishi wa kutorosha na kwenda kutafuta
soko kwingine na ili mapato ya serikali yasipotee.
“Mhe. Naibu Waziri sisi hapa
kiliochetu ni soko, hapa tulipo hata ukitaka kuuza madini lazima uende
Ruangwa au Tunduru umbali uliopo ni mkubwa kufika huko. Na soko kubwa la
Madini ya vito ni Tunduru, kwa hiyo ili mapato ya serikali yasipoteee
tunaomba soko liwe hapa hapa sisi tuuze madini yetu na watu wa TRA
wawepo ili tukiuza tuu serikali inachukuwa chake hapo hapo” alisema
Ijumaa Iddi mwenyekiti wa wachimbaji wadogo katika eneo hilo.
Katika kupatia majibu hoja zote zilizo wasilishwa, Naibu Waziri alianza kwa kusema.
“Mimi na waziri wangu Biteko iwe
mchana iwe usiku, tutafika mahali popote ili kuhakikisha serikali
inapata mapato kupitia madini, hivyo uwepo wangu hapa ni kwa sababu
hiyo na ili pesa hiyo ipatikane lazima migogoro na hizi kero lazima
zimalizwe ili mchimbe, muuze na kisha mlipe mapato ya serikali” alisema
Nyongo.
Katika kujibu hoja, Naibu Waziri
alianza kwa msimamisha Kaimu Afisa Madini Mkazi mkoa wa Lindi Mhandisi
Iddi atoe ufafanuzi kuhusu leseni na umiliki wa eneo hilo.
“Mhe. Naibu Waziri, kwanza kabisa
niseme eneo hili lina leseni halali inayo milikiiwa na ndugu Omar Said
Kojogo anae miliki kihalali kwa leseni Na. PML 36821 Southern Zone
ya Tshs. 1,937,000. Na kwa mujibu wa sheria ya madini ya mwaka 2010 na
marekebisho yake ya mwaka 2017 hairuhusu kutoa leseni kwenye eneo moja
ambalo teyari ilishatolewa na mahali hapa palishatolewa leseni kama
nilivyosema, na kama itakuwa hivyo mlabda kwa kesi maalum, hata hivyo
suala hili lilishashugulikiwa na muda si mrefu leseni yao itakuwa
teyari” alisema Mhandisi Idd Msikozi.
Kuhusu kilio cha masoko, Naibu
waziri alisema kwanza anawashukuru wachimbaji hao kwa kitendo chao cha
kulilia soko ili madini yao yakauzwe kwenye masoko rasmi. Amesema
serikali imetoa agizo kila mkoa uwe na soko la madini ili serikali ipate
fedha za kutosha kupitia madini ili fedha hizo zikatumike kwenye
shuguli nyingine za maendeleo.
Amesema mpango wa sasa wa wizara
ni kuhakikisha kuwa kuna vituo vya kununulia madini kwenye maeneo ya
wachimbaji ili wanaporo wasitembee mwendo mrefu kufuata soko.
“Ndugu zangu wanaaporo, kiliochenu
kuhusu soko kimenigusa sanaa, na sisi kama wizara ndio kitu ambacho
tunakisisitiza kila mahali, kwa hiyo hapa hapa naagiza Afisa Madini Mkoa
na Uongozi wa Wilaya kaeni chini kwa haraka mjadili ili kituo cha
kununulia madini hapa kianzishwe mara moja na serikali ianze kukusanya
mapato yake”. Aliongeza Nyongo.
Baada ya kutolea majibu ya hoja za
wachimbaji hao, Naibu waziri pia aliwaagiza wachimbaji kuanzisha mfuko
wa mahafa na dharula ili uwezo kuwasaidia mara miongoni mwao anapopatwa
na tatizo ahudumiwe kwa huduma ya awali huku akisubiri utaratibu binafsi
wa kutatua tatizo lake.
Kwa upande mwingine Nyongo
ameuagiza uongozi wa Wilaya zote mbili ukae pamoja na kuweka utaratibu
utakao wezesha kuwa na kituo cha kutolea huduma ya kwanza kwa maana pawe
na “Nurse” kwenye eneo hilo kwa utaratibu watakao ukubaliana. Aidha,
halmashauri hizo ziweke vyoo maeneo hayo kwa kuwa wachimbaji hao
wanalipa fedha serikalini hivyo wanastahili huduma hiyo.
Wakati huo huo Naibu Waziri
amewapongeza viongozi wa Wilaya zote mbili kwa jitihada zao za kutatua
mgogoro huo awali kabla hajafika hasa katika kukubaliana namna kukusanya
mapato ya kila upande kwani mapato yote yanakwenda kwenye mfuko mmoja
wa serikali.
Kwa upande wao viongozi wa wilaya
ya Nachingwea Katibu Tawala Husna Sekibobo na Mkuu wa Wilaya ya Liwale
Sarah Chiwamba kwa pamoja walimshukuru Naibu Waziri kwa kufika katika
eneo hilo na kujione hali halisi kutoa majibu ya moja kwa moja ya hoja
zilizo wasilishwa na waliahidi maelekezo na maagizo yake
watayatekelezwa.
Ziara ya Naibu Waziri ilikuwa ya
kukamilisha ratiba ya ziara ya Waziri wa Madini Doto Biteko aliesitisha
ziara yake mkoani humo na kurejea Dar es Salaam kwa ajili ya majukumu
mengi
No comments:
Post a Comment