Mchumi Mkuu kutoka Ofisi ya Waziri
Mkuu Bw. Silas Daudi akitoa mada kuhusu Mpango wa Biashara kwa vijana
wanajihusisha na shughuli mbalimbali za biashara na ujasiriamali katika
Mkoa wa Geita ikiwa ni awamu ya tatu ya Mafunzo ya Ujasiriamali na
Usimamizi wa Biashara kwa Vijana wenye umri kati ya miaka 18 hadi 35
yanayosimamiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu.
Baadhi ya Wajasiriamali
wakifuatilia kwa makini mada iliyokuwa ikiwasilishwa na mmoja ya watoa
mada wakati wa mafunzo ya ujasiriamali na usimamizi wa biashara kwa
vijana wenye umri wa miaka 18 hadi 35 yanayoratibiwa na Ofisi ya Waziri
Mkuu kwa kushirikiana na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi
(NEEC).
Mwezeshaji kutoka Ofisi ya Waziri
Mkuu Bw. Julius Tweneshe akielezea mada kuhusu taratibu za kufungua
kampuni wakati wa mafunzo hayo.
Sehemu ya wajasirimali kutoka Mkoa
wa Geita wakifuatilia mada iliyokuwa ikiwasilishwa wakati wa mafunzo
hayo yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano uliopo katika Ofisi ya Mkuu
wa Mkoa wa Geita.
Afisa Uwezeshaji kutoka Baraza la
Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) Bw. Halidi Mbwana akitoa
mada kuhusu masuala ya utafutaji wa vyanzo vya mapato kwa vijana
walioshiriki mafunzo hayo Mkoani Geita.
Baadhi ya Wajasiriamali walioshiriki kwenye mafunzo hayo wakijadiliana kazi kwenye vikundi.
Sehemu ya Sekretarieti
wakifuatilia mada zilizokuwa zikiwasilishwa na wawezeshaji wakati wa
mafunzo hayo yaliyofanyika Mkoani Geita Agosti 22, 2019.
PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU
(KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU)
No comments:
Post a Comment