Na.Alex Sonna,Dodoma
WAZIRI wa Nchi,Ofisi ya
Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,(TAMISEMI) Seleman Jafo
amemtaka Katibu Mkuu Tamisemi,Joseph Nyamhanga kuwarejesha katika kituo
cha kazi cha Ipogoro Manispaa ya Iringa watumishi saba ambao
walihamishwa hivi karibuni bila kufuata utaratibu.
Waziri Jafo ameyabainisha hayo leo
wakati akifungua Mkutano wa mwaka wa Waganga Wakuu wa Mikoa na
wilayakote nchini waliokutana Dodoma kujengewa uwezo katika kutekeleza
majukumu yao.
Amesema kumekuwa na tabia ya
uonevu kwa kushirikiana na wakuu wa vituo hivyo vya afya na kuwahamisha
vituo vya kazi jambo ambalo linawafanya wapoteze morali ya kufanya kazi
ilihali ni watumishi wanaojituma bila kuchoka.
Aidha,Jafo amemuagiza Katibu
Mkuu wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto,Dk. Zainabu
Chaula kufuatilia kama mganga aliyeondolewa kazini kama hakiilitendeka
au ni uonevu.
“Kule Iringa Ipogoro watu saba
wamesimamamishwa na wewe DMO ni mzuri kwanini unataka kuharibu
ukubwani,Naagiza wale watumishi saba warudishwe na kule nimetuma
timu,hatuwezi kulea mambo ya hovyo,” amesema Jafo.
Ameeleza kuwa licha juhudi za
serikali bado kuna kazi kubwa ya kuwekeza katika miundombinu ya afya
ambapo bado haiko vizuri na kupelekea watumishi kufanya kazi katika
mazingira ambayo si rafiki kwao.
Kwa upande wake,Naibu Waziri wa
Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Dk.Faustine Ndugulile
amesema kuna haja ya Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri kusimamia
suala la lishe kwani hawafanyi vizuri katika sekta hiyo.
Aidha wamewataka Waganga hao kuwa
wachapa kazi na kuacha kulalamika kwani Serikali ipo inafanya jitihada
nyingi katika kuboresha maeneo yao ya kazi.
“Lazima mama mjamzito hapaswi
kufariki katika kituo cha afya,tafsiri yake kwamba tumeshindwa hili la
vifo vya mama na mtoto ni lazima tuliangalie swala hili kwa upana
wake”.amesema Ndungulile.
Naye,Mwenyekiti wa Waganga Wakuu
wa Mikoa,Dk.Paul Chaote akisoma risala,amesema bado kuna changamoto ya
upatikanaji wa vifaa tiba hivyo wakaiomba serikali kuharakisha mchakato
wa bima kwa wote.
No comments:
Post a Comment