Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya
Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt.Hassan Abbasi,
akifafanua Jambo kuhusu Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Nchi za
Kusini mwa Afrika SADC, alipokuwa katika mahojiano ya kipindi cha 360
katika kituo cha Televisheni (Clouds TV) yaliyofanyika leo Agosti 14,
2019 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julias Nyerere Jijini Dar
es Salaa, kulia ni Mtangazaji wa Kipindi hicho, Baby Kabaye.
Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya
Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt.Hassan Abbasi, akieleza
Jambo kuhusu Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Nchi za Kusini mwa
Afrika SADC, alipokuwa katika mahojiano ya kipindi cha 360 katika kituo
cha Televisheni (Clouds TV) yaliyofanyika leo Agosti 14, 2019 katika
Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julias Nyerere Jijini Dar es Salaa,
kulia ni Mtangazaji wa Kipindi hicho, Baby Kabaye.
(Picha na Paschal Dotto-MAELEZO)
……………….
Na. Mwandishi Wetu-MAELEZO
Nchi 16 za Jumuiya ya Maendeleo ya
Kusini mwa Afrika (SADC) zimethibitisha kushiri Mkutano wa 39 wa Wakuu
wa Nchi wa Jumuiya hiyo utakaofanyika Jijini Dar es Salaam, Tanzania
Agost 17 na 18 mwaka huu.
Akizungumza katika Kipindi cha
360 cha Clouds Tv, Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji
Mkuu wa Serikali, Dkt.Hassan Abbasi alisema maandalizi yamekalika na
sasa Tanzania iko tayari kwa ugeni huo.
Dkt. Abbasi alisema kuwa
mkutano huo ulitanguliwa na matukio mbalimbali ikiwemo Maonesho ya Wiki
ya Viwanda kutoka nchi wanachama wa SADC, Vikao vya Maafisa Waandamizi
kutoka SADC, Vikao vya Mawaziri kutoka SADC na Mikutano mbalimbali ya
sekta za SADC, ambapo maeneo haya yote Tanzania inachukua uenyekiti wa
Nchi Wanachama.
“ Katika mikutano yote
iliyotangulia karibu nafasi zote za SADC kuanzia zile za kusimamia
kamati, kusimamia mabaraza mbalimbali, Tanzania imechukua hatamu, kwani
kuna sekta nyingi sasa zimeshachukua uenyekiti, Juzi Mtendaji Mkuu wa
Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania alichukua kiti hicho cha kwenye
kamati ya wanachama wa SADC, vilevile Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya
Mawasiliano Tanzania naye alichukua nafasi hiyo kwenye Kamati ya
Mawasiliano SADC”, Dkt. Hassan Abbasi.
Dkt.Abbasi alisema kuwa
kuelekea kwenye tukio lenyewe ambalo ni Mkutano wa Wakuu wa Nchi za
Wafalme kutoka Serikali 16 za nchi wanachama, zimethibitisha kushiriki
mkutano huo na kuwa viongozi wao wataanza kufika nchini kuanzia tarehe
15 na kuendelea.
Aidha Dkt.Abbasi alisema kuwa
Tanzania imebarikiwa kuwa Kitovu cha Amani kwa nchi za kusini mwa
Afrika, kwa hiyo viongozi wengi wa nchi hizo watakuja Tanzania kama
wanarudi nyumbani, ambako ni kituo cha ukombozi wa nchi zao, na kufanya
mkutano ambapo Agost 17 na 18 Wakuu wa Nchi Wanachama watasaini
mikataba mbalimbali na kuhitimisha ajenda zao.
Aliongeza kuwa kabla ya kufika
mkutano wa wakuu wa nchi kuna matukio mengine kama vile Mabalozi na
wawakilishi wa Tanzania kutoka nchi mbalimbali kuwasili nchini; ikiwa ni
lengo la kushiriki Mkutano Mkuu ambapo pia wamepata wasaa wa kufanya
ziara katika miradi mikubwa inayotekelezwa na Serikali ya Awamu ya
Tano.
“Kabla ya kufika Mkutano Mkuu,
kuna matukio mbalimbali ambayo pia ni makubwa na ni muhimu sana kwa
nchi yetu, leo tunatukio kubwa la Mabalozi 42 wa Tanzania kutoka nchi
mbalimbali duniani wanatembelea mradi mkubwa wa kuzalisha umeme wa
Julius Nyerere Hydro Power Project( JK HPP) na kesho watatembelea
mradi wa Ujenzi wa Reli ya kisasa (SGR) na hawa wote wako nchini kwa
ajili ya kushiriki Mkutano Mkuu wa SADC”, Alisisitiza Dkt.Abbasi.
Dkt.Abbasi alisema kuwa
Mabalozi hao wamekwenda kuona kwa mfano, ni nini serikali yao
inatekeleza ili wakirudi katika maeneo yao ya kazi wapate kuyatangaza
waliyoyaona na kuweza kuleta wawekezaji watakao kuja kuwekeza nchini na
kuleta mapato kwa taifa.
Pia, Dkt. Abbasi alisema kuwa
leo Tanzania itampokea Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa ambaye
atawasili nchini kwa ziara ya siku mbili kabla ya Kusiriki Mkutano Mkuu,
na ziara yake itajikita zaidi katika kutembelea eneo la wapigania uhuru
Mazimbu, Mkoani Morogoro, ili kujenga kumbukizi ya Udungu kati ya
Tanzania na Afrika Kusini.
No comments:
Post a Comment