UVCCM TAIFA YAFANYA MAFUNZO MAALUM KWA WASICHANA MKOA WA DAR ES SALAAM
Ndg Makamu
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Bi Tabia Mwita akizungumza wakati wa
Ufunguzi wa Semina elekezi ya kimkakati kwa Wasichana Mkoa wa Dar es
Salaam.
Mjumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana Taifa Ndg Rose Manumba na Mratibu Mkuu wa Mafunzo hayo akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Semina elekezi ya kimkakati kwa Wasichana Mkoa wa Dar es Salaam.
Washiriki Mbalimbali wakifuatilia Mada
Sehemu ya Meza kuu ikiimba wimbo wa
Hamasa Wapili kulia ni Ndg Tabia Mwita Makamu mwenyekiti wa UVCCM,Ndg
Rose Manumba Mjumbe wa Baraza Kuu Taifa na Mratibu wa Mafunzo hayo(tatu
kulia),(pili kushoto)Ndg Jafari kubecha mgamba (MNEC)anaewakilisha kundi
la Vijana pamoja na wawasilishaji mada wakati wa Ufunguzi wa Semina elekezi ya kimkakati kwa Wasichana Mkoa wa Dar es Salaam.
Ndg Rose Manumba akiongoza Mjadala kwa Washiriki
Ndg Dorris Mollel ambaye ni Mkurugenzi wa Doris Mollel Foundation akiwasilisha mada
Suma Mwaitenda ambaye ni Mkurugenzi wa FURSA, kutokea Clouds Media Digita akiwasilisha mada
Ndg Jafari Kubecha Mgamba akizungumza
wakati wa ufangaji wa Mafunzo maaalum kwa ajili ya wasichana wa mkoa wa
dar es salaam (PICHA ZOTE NA FAHADI SIRAJI WA UVCCM)
Makamo
wa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Vijana wa CCM Taifa *Ndg Tabia Mwita*
amefungua mafunzo Maalum kwa Wasichana kwa Mkoa wa Dar Es Salaam.
Mafunzo
hayo Yaliyosimamiwa na kuratibiwa na *Mjumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa
Vijana wa Chama Cha Mapinduzi *Ndg.Rose Robert Manumba* kwa Kushirikiana
Taasisi ya Kijerumani FES kwa lengo la kuwaelimisha na kuwaongezea
ujuzi na Maarifa yakiuongozi.
Pamoja
na kufungua Mafunzo hayo Miongoni mwa waliyotoa na mada ni Ndg.Tabia
Mwita na amewasilisha Mada ya *Ushiriki wa wanawake katika siasa*
ambavyo amesisitiza wanawake kuendelea kujitokeza kwa wingi kuwania
nafasi mbalimbali za kisiasa bila kuogopa. Amewasihi wanawake kujiamini
na kutokukubali kukatishwa tamaa.
Makamu
huyo amesisitiza umuhimu wa kuwa na umoja na mshikamano ili kuendeleza
kusaidia Serikali katika juhudi zinazofanyika kumuinua Mwanamke.
Aidha,
Mjumbe wa Baraza Kuu UVCCM Taifa *Rose Manumba* akiwa amesisitiza kuwa
ni muhimu sisi kama wasichana kuwa sehemu ya mabadiliko tunayotamani
kuyaona katika nchi yetu na hata duniani kwa ujumla. Tuwe tayari
kutumikia nafasi zetu popote pale tulipo kuendelea kuunga mkono Juhudi
za Mhe. Rais Dr. John pombe Magufuli anayepambana usiku na mchana
kumuinua mwanamke wa kitanzania ili kuleta maendeleo katika Taifa letu.
Wameshiriki
wakufunzi mbalimbali kama Dorris Mollel ambaye ni Mkurugenzi wa Doris
Mollel Foundation aliyewasilisha mada ya *Mchango wa asasi za kiraia
katika kumuinua Mwanamke* Na Suma Mwaitenda ambaye ni Mkurugenzi wa
FURSA, kutokea Clouds Media Digital aliyewasilisha mada ya; *Namna gani
msichana anaweza kuziona na kuzipata Fursa.*
*Ndg.
Japhary Kubecha* ambaye ni Mjumbe wa Halmashauri kuu ya UVCCM Taifa
katika kufunga mafunzo hayo amesisitiza wanawake kujituma katika kazi na
sio kuridhika na nafasi mbalimbali ambazo wanaweza kupata kwa kigezo
kuwa ni wanawake.
Mafunzo
haya yamehudhuriwa na viongozi mbalimbali; Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya
ya Kinondoni Lilian Rwebangira, Abdul-Rahman Killo na Mwanaidi ambao ni
Maafisa kutoka UVCCM Makao Makuu.
No comments:
Post a Comment