UJENZI KIVUKO CHA KAYENZE KWENDA KISIWA CHA BEZI MWANZA KUKAMILIKA NOVEMBA 2019
Mkurugenzi
wa Songoro Marine Ltd Meja Songoro akimuonesha Mbunge wa Jimbo la
Ilemela na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt
Angeline Mabula (wa kwanza kushoto) maendeleo ya ujenzi wa Kivuko cha
Kayenze kwenda Kisiwa cha Bezi mkoani Mwanza wakati wa ziara yake ya
kukagua kivuko hicho kinachotarajiwa kukamilika Novemba 2019.
Mbunge wa
Jimbo la Ilemela ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo
ya Makazi Dkt Angeline Mabula akishuka kutoka katika kivuko cha Kayenze
kwenda Kisiwa cha Bezi mkoani Mwanza wakati alipofanya ukaguzi wa
kivuko hicho kinachotarajiwa kukamilika Novemba 2019.
Mkurugenzi
wa Songoro Marine Ltd Meja Songoro akimuonesha Mbunge wa Jimbo la
Ilemela na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt
Angeline Mabula (wa kwanza kushoto) maendeleo ya ujenzi wa Kivuko cha
Kayenze kwenda Kisiwa cha Bezi mkoani Mwanza wakati wa ziara yake ya
kukagua kivuko hicho kinachotarajiwa kukamilikaNovemba 2019.
Mbunge wa
Jimbo la Ilemela ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo
ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza ndani ya kivuko cha Kayenze
kwenda Kisiwa cha Bezi mkoani Mwanza na ujumbe alioambatana nao wakati
alipofanya ukaguzi wa kivuko hicho kinachotarajiwa kukamilika Novemba
2019.
Mbunge wa
Jimbo la Ilemela ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo
ya Makazi Dkt Angeline Mabula akiangalia kivuko cha Kayenze kwenda
Kisiwa cha Bezi mkoani Mwanza wakati alipofanya ukaguzi wa kivuko hicho
kinachotarajiwa kukamilika Novemba 2019.
Mbunge wa
Jimbo la Ilemela ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo
ya Makazi Dkt Angeline Mabula akikagua maendeleo ya ujenzi wa kivuko
cha Kayenze kwenda Kisiwa cha Bezi mkoani Mwanza wakati alipofanya
ukaguzi wa kivuko hicho kinachotarajiwa kukamilika Novemba 2019.
Mbunge wa
Jimbo la Ilemela ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo
ya Makazi Dkt Angeline Mabula akikagua maendeleo ya ujenzi wa kivuko
cha Kayenze kwenda Kisiwa cha Bezi mkoani Mwanza wakati alipofanya
ukaguzi wa kivuko hicho kinachotarajiwa kukamilika Novemba 2019.(PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI)
………………….
Na Munir Shemweta, WANMM MWANZA
Ujenzi wa
kivuko cha Kayenze kwenda Kisiwa cha Bezi mkoani Mwanza unaogharibu
kiasi cha bilioni 2.7 unatarajiwa kukamilika Novemba mwaka 2019.
Hayo
yamebainika juzi wakati Mbunge wa jimbo la Ilemela mkoani Mwanza ambaye
pia ni Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline
Mabula alipotembelea kivuko hicho kuangalia maendeleo ya ujenzi ikiwa ni
utekelezaji wa ahadi aliyoitoa kwa wananchi wa jimbo lake wakati wa
uchaguzi mkuu uliofanyika 2015.
Kwa mujibu wa Dkt Mabula, kivuko cha Kayenze kwenda Kisiwa cha Bezi chenye
uwezo wa kubeba abiria 250, magari 10 na ukubwa wa tani 10 kitaondoa
kero ya muda mrefu waliyokuwa wakiipata wananchi wa Kayenze na Bezi
katika suala la huduma ya usafiri wa majini.
‘’Wananchi
wa Kisiwa cha Bezi na Kayenze Mwaloni wamekuwa na shida ya usafiri
majini kwa muda mrefu na mimi niliahidi kuwapatia kivuko wakati wa
uchaguzi mwaka 2015 na ombi langu la kujenga kivuko hicho lilipokelewa
vyema na serikali toka mwaka 2016 kwa ahadi ya kujenga kivuko hicho’’
Alisema Dkt Mabula.
Mbunge huyo
wa Jimbo la Ilemela alisema, kuchelewa kukamilika mapema kivuko hicho
kulitokana na changamoto kadhaa na mojawapo ni kukwama kwa vifaa
bandarini kulikosababishwa na msamaha wa ushuru ambapo hata hivyo, Dkt.
Mabula aliahidi kushughulikia suala hilo na kufafanua kuwa Oktoba mwaka
2019 kivuko hicho kitafanyiwa majaribio rasmi kabla ya kukabidhiwa mwezi
mmoja baadaye kwa ajili yua kuanza kazi rasmi.
Kwa upande
wake Mkurugenzi wa Kampuni inayotengeneza kivuko hicho ya Songoro Marine
Ltd Meja Songoro alisema ujenzi wa kivuko higho ulioanza Januari 2019
uko katika hatua za mwisho za ukamilishaji ambapo sasa kampuni yake
inakamilisha kufunga mifumo ya maji, umeme, zimamoto , kufunga ingini na
vifaa vya kuendeshea kivuko hicho.
Kwa mujibu
wa Songoro, kampuni hiyo ya Songoro Marine Ltd ni mahiri katika
kutengeneza vivuko na kutolea mfano wa vivuko vya Mv Mwanza, Kazi pamoja
na kile cha Geita kuwa ni vivuko vilivyofanyiwa kazi na kampuni yake na
kufafanua kuwa hivi sasa kampuni hiyo imepata kazi za vivuko katika nchi jirani za Kenya na Uaganda.
No comments:
Post a Comment