MBUNGE DITOPILE ATIMIZA AHADI YAKE KWA KUCHIMBA KISIMA

Na.Alex Sonna,Kongwa
Mbunge wa Viti Maalum anaewakilisha
Vijana mkoani Dodoma, Mhe Mariam Ditopile ametekeleza ahadi yake ya
kuchimba kisima kwa wananchi wa eneo la Mkoka Jimbo la Kongwa chenye
uwezo wa kutoa Lita 25000 kwa saa.
Mhe Ditopile amekabidhi kisima hicho kwa
wananchi wa Kongwa mbele ya Mbunge wa Jimbo hilo ambaye pia ni Spika wa
Bunge, Mhe Job Ndugai.
“Niliahidi kuchimba kisima kwenu ndugu
zangu wa Kongwa, sisi kama wasaidizi wa Rais Magufuli tunapaswa
kuhakikisha tunamsaidia Rais wetu ambaye ameuletea Maendeleo Mkoa wetu
wa Dodoma. Tunapaswa kumuunga mkono kwa vitendo katika kuwatumikia
wananchi wanyonge ambao Rais wetu amekua akiwapigania kila siku,”
amesema Mhe Ditopile.
Kwa upande wake Spika wa Bunge, Mhe Job
Ndugai amempongeza Mhe Ditopile kwa namna ambavyo amekua akiwatumikia
wananchi wa Dodoma huku akimtaka kutosita kuongeza nguvu katika sekta
zingine ikiwemo Afya na Elimu.
” Mimi sina shaka na Mhe Ditopile, huyu
ni kijana ambaye amekua akitoa ahadi na kutimiza, hivi karibuni alitoa
ahadi ya kusomesha wasichana watakaofaulu kwenda kidato cha tano na
ametimiza, hivyo nimpongeze na nimtie moyo katika kuwatumikia wananchi
wa Dodoma,” amesema Spika Ndugai.
No comments:
Post a Comment