KATIBU MKUU OFISI YA WAZIRI MKUU ATAKA DHANA YA AFYA MOJA KUTEKELEZWA KWA WAKATI
Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Uwekezaji Bi. Dorothy Mwaluko akizungumza wakati wa kikao cha Wadau
wa Afya Moja walipokutana kujadili utekelezaji wa mpango mkakati wa
afya moja nchini. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Uratibu Maafa,
Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Bashiru Taratibu.
Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu Maafa,
Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe akielezea jambo kwa wadau wa
Afya Moja walioshiriki kikao hiko kilichofanyika Hoteli ya Morena,
Jijini Dodoma.
Mtaalamu Mshauri wa Afya Moja Dkt. Kunda
John akichangia mada kuhusu umuhimu wa dhana ya Afya Moja wakati wa
kikao kilichofanyika Julai 12, 2019 Jijini Dodoma.
Baadhi ya wataalamu wa Dawati la Afya
Moja nchini wakifuatilia kwa makini maelezo ya Katibu Mkuu, Ofisi ya
Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Uwekezaji Bi. Dorothy Mwaluko (hayupo
pichani) wakati wa kikao cha Wadau wa Afya Moja walipokutana kujadili
utekelezaji wa mpango mkakati wa afya moja nchini.
Mratibu wa Dawati la Afya Moja kutoka
Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Hansom Chinyuka akiwasilisha mada kuhusu
utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Afya Moja nchini walipokutana Jijini
Dodoma.
Sehemu ya wataalamu wa dawati la Afya
Moja nchini wakifuatilia mada iliyokuwa ikiwasilishwa na Mratibu wa
Dawati la Afya Moja kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Hansom Chinyuka
(hayupo pichani).
Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,
Uratibu na Uwekezaji Bi. Dorothy Mwaluko akiteta jambo na Mkurugenzi wa
Idara ya Uratibu Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe mara
baada ya kikao kilichowakutanisha na Wadau wa Afya Moja kwa lengo la
kujadili utekelezaji wa mpango mkakati wa afya moja nchini.
PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU
(KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU)
……………………
Na; MWANDISHI WETU
Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,
Uratibu na Uwekezaji) Bi. Dorothy Mwaluko amewataka waratibu wa dawati
la Afya Moja kutekeleza dhana ya Afya Moja kwa wakati sambamba na kuweka
mikakati mahususi itakayowaongoza katika utendaji wa dhana hiyo.
Ametoa kauli hiyo wakati akifungua kikao
cha wadau wa afya moja na wataalam kutoka sekta ya Afya, Mifungo,
Wanyamapori na Mazingira kilichofanyika Julai 12, 2019, Jijini Dodoma.
Alieleza kuwa dhana ya afya moja
inajumuisha wataalam na wadau mbalimbali kwa lengo la kufanikisha
utekelezaji wa dhana hiyo ikiwemo kutoa fursa ya kushirikiana pamoja
katika kukabiliana na madhara au magojwa hatarishi nchini.
“Nimepitia Sera ya Afya moja na kuona
suala hili linatakiwa kusimamiwa vyema, ikiwa Ofisi ya Waziri Mkuu ni
mratibu wa Dawati la Afya moja kwa kushirikiana na Wizara, Taasisi za
Serikali na wadau wa maendeleo, katika kuhakikisha nchi yetu inakuwa
mahala salama,” alieleza Mwaluko
Aliongeza kuwa, suala la kujenga uwezo
kwa waratibu wa dawati la afya moja inatakiwa kuangalia ofisi kwa ujumla
na si mjumbe mmoja tu ambaye atakuwa anasimamia masuala hayo ya Afya
moja wakati wote.
“Mnatakiwa mtambue kuwa mkiwa kama
wafanyakazi mna majukumu mengine ya kiofisi ambayo mnatakiwa
kuyatekeleza, hivyo mtoe fursa kwa wafanyakazi wengine waliopo kwenye
ofisi zenu kujifunza na kuelewa dhana hii ya afya moja,” alieleza
Mwaluko.
Aidha, alitoa wito kwa waratibu wa dawati
hilo kuelimisha umma kuhusu maana ya Afya Moja na dhana nzima ya Afya
moja ili wananchi waweze kuwa na ufahamu wa suala hilo.
Pia, aliwahimiza washauri elekezi wa
dawati hilo kutimiza majukumu yao kwa weledi na kutoa ushauri mapema
kuhusu dhana ya Afya Moja.
Kwa upande wake, Prof. Robinson Mdegela
ambaye ni Mtaalamu Mshauri wa Afya Moja alisema kuwa kukutana kwao
katika kikao hiko ni kuonesha utayari wa kila mtaalamu katika kutekeleza
majukumu yake kwa ufanisi na kuongeza msukumo juu ya utekelezaji wa
mpango mkakati wa Afya Moja.
No comments:
Post a Comment