KANISA LA EFATAH LATAKIWA KUANDAA MPANGO KAZI WA KUENDELEZA NG’OMBE WA MAZIWA
Akizungumza na viongozi na wafanyakazi wa
shamba la g’ombe wa Maziwa la Malonje leo, Naibu Waziri wa Mifugo na
Uvuvi Mhe.Abdallah Ulega ameitaka taasisi ya kidini ya Kanisa la EFATAH
iliyopatiwa shamba la ng’ombe wa maziwa la Malonje baada ya
kubinafsishwa na serikali mwaka 2007,kuandaa mpango kazi utakaosaidia
kuendeleza ng’ombe wa mziwa na uzalishaji wa maziwa wenye tija endevu.
Aidha Naibu waziri ameitaka taasisi hiyo
ya kidini baada ya kuandaa mpango kazi huo ugawiwe kwa uongozi wa idara
ya mifugo Hamashauri ya Wilaya ya Sumbawanga,uongozi wa mifugo mkoa wa
Rukwa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi makao makuu kwa ajili ya kumbukumbu.
Mhe.Ulega ameseama kuwa mpango huo
utasaidia kufuatilia utekelezaji wake kuona kama wanafanya kazi kama
mpango huo unavyoelekeza au la na kuweza kuchukua hatua stahiki kwa
uongozi wa shamba ikiwa ni pamoja na kunyang’anywa shamba hilo na
kugawiwa kwa wafugaji endapo itagundulika hawafuati mpango kazi wa
shamba hilo.
Akizungumzia mafanikio ya shamba hilo
Naibu waziri alisema kuwa siya kuridhisha kwa kuwa tangu libinafsishwe
nakupewa taasisi hiyo inaonekana kuna shughuli zingine nje ya zile za
kuedekeza shamba hilo zinafanyika hivyo kutokuwa na mafanikio chanya.
“Haiwezekani hadi leo,2019 taasisi
inaidadi ya ng’ombe 337 toka idadi ya ng’ombe 174 iliwakuta wakati
wanapewa shamba hilo ,mwaka 2007”,alisema Ulega.
Awali akisoma taarifa ya shamba hilo
Meneja Mchunguji Bw.Rwiza Binamungu alisema kuwa shamba hilo lina ukubwa
wa hekta elfu kumi(10,000), ng’ombe wa maziwa 144 nauzalishaji wa
maziwa kwa siku ni lita 50.
Hivi karibuni Rais wa Tanzania Dkt.John
Pombe Magufuli alishasema kuwa Mashamba ya serikali ambayo yanasuasua
katika uzalishaji yagawiwe kwa wafugaji ili wafuge kibashara na kisasa.
No comments:
Post a Comment