BALOZI IDDI ATEMBELEA ENEO LITAKALOJENGWA OFISI ZA SERIKALI YA ZANZIBAR DODOMA
Makamuwa Pili wa Rais wa Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Balozi Seif Ali Iddi alisalimiana na Naibu
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Balozi Joseph Sokoine alipowasili Mahona Makuu jijini Dodoma ambako
alioneshwa eneo litakalojengwa Ofisi za Serikali hiyo.
Makamuwa Pili wa Rais wa Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Balozi Seif Ali Iddi alisalimiana na Kaimu
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samuel Mwashambwa, mara
baada ya kuwasili Mahona Makuu jijini Dodoma ambako alioneshwa eneo
litakalojengwa Ofisi za Serikali hiyo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Balozi Seif Ali Iddi alisalimiana na Kaimu
Mkurugenzi wa Idara ya Muungano kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais wa Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Sifuni Msangi, mara baada ya
kuwasili Mahona Makuu jijini Dodoma ambako alioneshwa eneo
litakalojengwa Ofisi za Serikali hiyo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Balozi Seif Ali Iddi (mbele katikati)
akiongozwa na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Balozi Joseph Sokoine (mwenye tai), kuangalia eneo
lililotolewa kwa SMZ kwa ajili ya ujenzi wa Ofisi zake Mahona Makulu
jijini Dodoma.
Mratibu wa Mchakato wa Kuhamishia
Serikali Dodoma kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Meshack Bandawe (kushoto)
akitoa maelezo kuhusu eneo lililotolewa kwa ajili ya ujenzi wa Ofisi za
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ).
PICHA ZOTE NA OFISI YA MAKAMU WA RAIS
…………………….
Na Ofisi ya Makamu wa Rais
Makamuwa Pili wa Rais wa Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Balozi Seif Ali Iddi ameoneshwa na kutembelea
eneo ambalo zitajengwa Ofisi za Serikali hiyo eneo la Mahoma Makulu
Jijini Dodoma.
Akizungumza mara baada ya kutembelea eneo
hilo, Balozi Iddi ambaye aliambatana na Waziri wa Biashara na Viwanda
Zanzibar Mhe Balozi Amina Salum Ali, alishukuru Serikali kwa kupewa eneo
hilo.
Aliahidi kuwa SMZ itaaaza ujenzi wa Ofisi
zake katika bajeti ya mwaka ujao wa fedha na kama watapata fungu ujenzi
utaanza mapema iwezekanavyo ili waweze kuhamia katika Makamo Makuu ya
Nchi.
Katika ziara hiyo ujumbe huo kutoka
Zanzibar ulipokelewa na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Balozi Joseph Sokoine, Kaimu Mkurugenzi
wa Utawala na Rasilimali Watu Ofisi, Samuel Mwashambwa hiyo na viongozi
mbalimbali
Balozi Seif alipata nafasi ya kutembelea
pia eneo la Mji wa Serikali wa Mtumba ambako zimejengwa Ofisi 25 za
Serikali zikiwemo za Wizara mbalimbali na tayari watumishi wake
wamehamia.
Akizungumza kuhusu eneo hilo Mratibu wa
Mchakato wa Kuhamishia Serikali Dodoma kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu,
Meshack Bandawe alisema eneo hilo lina ekari 30.
Alisema tangu Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Mhe Dkt. John Pombe Magufuli alipotangaza Serikali kuhamia
Makao Makuu ya Nchi Julai 25, 2016 ulianzishwa mchakato wa kuhamisha
watumishi.
No comments:
Post a Comment