Tuesday, June 18, 2019

WATU 168 WANUSURIKA AJALI YA TRENI JIJINI DODOMA

Na.Alex Mathias,Dodoma

Jumla ya watu 168 wamenusurika na ajali ya Treni  iliyotokea mkoani Dodoma katika maeneo ya level cross ya hazina katika halamshauri ya jiji la Dodoma.

Ajali hiyo imehusisha Gari lenye no za usajili T 860 APW aina ya isuzu likiendeshwa na Dereva  Hamis Salamu (49)  mkazi wa  Nkuhungu ambapo gari hilo liligonga Treni  ya abiria No, Y 12,ikiendeshwa na Michael  Mdachi (44) mkazi wa kisasa Jijini hapa  na Guard Abdala  Ngola (59) ambaye ni mkazi wa Area c Dodoma.

Akizungumza katika eneo la tukio, Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma Gilles Muroto amesema Treni hiyo ilikuwa ikitokea kigoma ,mwanza na mpanda kuelekea Dar es salaam ikiwa na behewa 9 za daraja tatu mbili za daraja kwanza,Behewa la mgahawa moja,Behea la vifurushi moja na Behea la Breki Moja na kusababisha majeruhi kwa abiria 32 waliokuwa kwenye Behewa namba 3648 na 3607 ambayo yalianguka.

”Mnamo tarehe 17a ya 11/06/2019 majira ya saa 11:25 usiku ilianza safari kutoka Tabora kuelekea Dar es Salaam ikiwa na mabehewa 14 kama yalivyotajwa hapo juu na ilipofika maeneo ya kuvuka makutano ya Reli na kugongwa na gari”amesema Muroto

Muroto amesema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa gari kutochukua tahadhari alipokuwa akivuka makutano ya Reli na barabara hivyo gari kuzima likiwa katikati ya Reli na Dereva wa gari aliruka na kukimbilia Polisi Kujisalimisha

Aidha, kamanda muroto ameongeza kuwa hali ya abiria waliopata ajali hiyo kati ya abiria 32 watatu hali sio za kuridhisha.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Dodoma mjini Patrobasi katambi ameliomba  jeshi la polisi kuendelea kufanya uchunguzi wa kina ili kujua chanzo cha ajali hiyo.

No comments:

Post a Comment