WACHEZAJI 38 WA TIMU YA TAIFA STARS WAFANYIWA UCHUNGUZI WA MOYO
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo
Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akizungumza na Daktari wa
timu ya Taifa Stars Emily Urasa wakati wa kuwafanyia uchunguzi wa kina
wa magonjwa ya moyo wachezaji wa timu hiyo leo Jijini Dar es Salaam.
Wachezaji hao walifanyiwa vipimo vya kuangalia jinsi moyo unavyofanya
kazi (Echocardiograph) na mfumo wa umeme wa moyo unavyofanya kazi
(Electrocardiography –ECG).
Daktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
(JKCI) Siza Ngomero akimpima kipimo cha kuangalia jinsi moyo
unavyofanya kazi (Echocardiogram) mchezaji wa timu ya Taifa Stars Feisal
Salum wakati wa uchunguzi wa kina wa magonjwa ya moyo kwa wachezaji wa
timu hiyo leo Jijini Dar es Salaam.
Fundi Sanifu wa Moyo na Mishipa ya damu
wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Abuu Dalidali akimpima kipimo
cha kuangalia mfumo wa umeme wa moyo (Electricalcardiography –ECG)
mchezaji wa timu ya Taifa Stars Yahaya Zaid wakati wa kuwafanyia
uchunguzi wa kina wa magonjwa ya moyo wachezaji wa timu hiyo leo Jijini
Dar es Salaam. Wachezaji hao wamefanyiwa uchunguzi wa kina wa magonjwa
ya moyo kabla ya kwenda nchini Misri kushiriki mashindano ya AFCON
yatakayoanza tarehe 21/06/2019.
Picha na: Genofeva Matemu – JKCI
………………….
Wachezaji 38 wa timu ya Taifa Stars
wamefanyiwa uchuguzi wa kina wa magonjwa ya moyo kama Shirikisho la
Mpira wa Miguu Africa (CAF) linavyoelekeza kabla ya kuanza kwa
mashindano ya kombe la Mataifa ya Africa (AFCON) ni lazima wachezaji
wanaoshiriki mashindano hayo wapimwe afya zao.
Vipimo walivyofanyiwa wachezaji hao ni
vya kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (Echocardiograph) na mfumo wa
umeme wa moyo unavyofanya kazi (Electrocardiography –ECG). Upimaji huu
umefanywa na madaktari bingwa wa magonjwa ya moyo wa Taasisi ya Moyo
Jakaya Kikwete (JKCI).
Taasisi yetu ni Hospitali
iliyothibitishwa na CAF kuwa inakidhi vigezo vyote vya upimaji wa
magonjwa ya moyo. Uthibitisho huu ulitolewa kabla ya kuanza kwa
mashindano ya AFCON kwa vijana wenye umri wa chini ya miaka 17
yaliyofanyika mapema mwaka huu hapa nchini .JKCI ilikaguliwa na
kuthibitishwa na wakaguzi kutoka CAF.
Matokeo ya vipimo hivyo yatasaidia
kufahamu afya za wachezaji na utimamu wao wa kimwili kabla ya kwenda
kushiriki katika mashindano ya AFCON yanayotarajia kuanza tarehe
21/06/2019 huko nchini Misri.
Tunatoa wito kwa vilabu vya mpira hapa
nchini kuwaleta wachezaji wao kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa
magonjwa ya moyo hii itawasaidia wachezaji hao kufahamu kama
wanamatatizo au la na kuepukana na vifo vya ghafla vinavyoweza kuwapata
wakiwa uwanjani. Kwa upande wa wananchi kabla ya kujiunga na vilabu
vya mazoezi ni muhimu wakapima afya zao yakiwemo magonjwa ya moyo..
No comments:
Post a Comment