TUNAENDELEA KUBORESHA SEKTA YA ELIMU-WAZIRI NDALICHAKO
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia,
Prof. Joyce Ndalichako akizungumza wakati wa hafla ya Siku ya Elimu
iliyoambatana na utoaji tuzo kwa Wanafunzi Bora wa Darasa la Saba,
Kidato cha Nne na Kidato cha Sita kwa Mwaka 2018 leo jijini Dodoma.
Hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Wasichana
Msalato na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa sekta ya elimu.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu,
Sayansi na Teknolojia, Dkt. Avemaria Semakafu akizungumza wakati wa
hafla ya Siku ya Elimu iliyoambatana na utoaji tuzo kwa Wanafunzi Bora
wa Darasa la Saba, Kidato cha Nne na Kidato cha Sita kwa Mwaka 2018 leo
jijini Dodoma. Hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Shule ya
Sekondari Wasichana Msalato na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa sekta
ya elimu.
Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Ofisi ya
Rais –TAMISEMI, Bibi. Odilia Joseph Mushi akizungumza wakati wa hafla ya
Siku ya Elimu iliyoambatana na utoaji tuzo kwa Wanafunzi Bora wa
Darasa la Saba, Kidato cha Nne na Kidato cha Sita kwa Mwaka 2018 leo
jijini Dodoma. Hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Shule ya Sekondari
Wasichana Msalato na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa sekta ya elimu.
Kaimu Kamishna wa Elimu Tanzania, Lyabwna
Mtahabwa akielezea tuzo za Wanafunzi Bora wa Darasa la Saba, Kidato cha
Nne na Kidato cha Sita kwa Mwaka 2018 wakati wa hafla ya Siku ya Elimu
iliyoambatana na utoaji tuzo hizo leo jijini Dodoma. Hafla hiyo
imefanyika katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Wasichana Msalato na
kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa sekta ya elimu.
Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari
Wasichana Msalato ya jijini Dodoma wakifuatilia hafla ya Siku ya Elimu
iliyoambatana na utoaji tuzo kwa Wanafunzi Bora wa Darasa la Saba,
Kidato cha Nne na Kidato cha Sita kwa Mwaka 2018 leo jijini Dodoma.
Hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Wasichana
Msalato na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa sekta ya elimu.
Miongoni mwa wanafunzi bora wa Kidato cha
Sita mwaka 2018 tokea Shule ya Sekondari Mvumi, Erick Maximilian
akipokea cheti na zawadi pesa taslimu shilingi milioni 1.5 toka kwa
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako wakati wa
hafla ya Siku ya Elimu iliyoambatana na utoaji tuzo kwa Wanafunzi Bora
wa Darasa la Saba, Kidato cha Nne na Kidato cha Sita kwa Mwaka 2018
leo jijini Dodoma. Pamoja na kuwa mwanafunzi huyo kuwa ni mwenye
mahitaji maalum.
Meneja wa Shule ya Kaizirege and Kemebos
toka Bukoba,Eulogius William akipokea cheti na tuzo toka kwa Waziri wa
Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako kutambua mchango
wa Shule zilizofanya vizuri katika matokeo ya mwaka 2018 wakati wa hafla
ya Siku ya Elimu iliyoambatana na utoaji tuzo kwa Wanafunzi Bora wa
Darasa la Saba, Kidato cha Nne na Kidato cha Sita kwa Mwaka 2018 leo
jijini Dodoma. Pamoja na kuwa mwanafunzi huyo kuwa ni mwenye mahitaji
maalum.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia,
Prof. Joyce Ndalichako akiwa katika picha ya pamoja na Wanafunzi Kumi
bora wa Darasa la Saba 2018 mara baada ya kumaliza hafla ya Siku ya
Elimu iliyoambatana na utoaji tuzo kwa Wanafunzi Bora wa Darasa la
Saba, Kidato cha Nne na Kidato cha Sita kwa Mwaka 2018 leo jijini
Dodoma. Hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Shule ya Sekondari
Wasichana Msalato na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa sekta ya elimu.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia,
Prof. Joyce Ndalichako akiwa katika picha ya pamoja na Wanafunzi Kumi
bora wa Kidato cha Nne mwaka 2018 mara baada ya kumaliza hafla ya Siku
ya Elimu iliyoambatana na utoaji tuzo kwa Wanafunzi Bora wa Darasa la
Saba, Kidato cha Nne na Kidato cha Sita kwa Mwaka 2018 leo jijini
Dodoma. Hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Shule ya Sekondari
Wasichana Msalato na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa sekta ya elimu.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia,
Prof. Joyce Ndalichako akiwa katika picha ya pamoja na Wanafunzi Kumi
bora wa Kidato cha Sita mwaka 2018 mara baada ya kumaliza hafla ya Siku
ya Elimu iliyoambatana na utoaji tuzo kwa Wanafunzi Bora wa Darasa la
Saba, Kidato cha Nne na Kidato cha Sita kwa Mwaka 2018 leo jijini
Dodoma. Hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Shule ya Sekondari
Wasichana Msalato na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa sekta ya elimu.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia,
Prof. Joyce Ndalichako akiwa katika picha ya pamoja na na wajumbe wa
Kamati ya Maandalizi ya hafla ya Siku ya Elimu ya Siku ya Elimu
iliyoambatana na utoaji tuzo kwa Wanafunzi Bora wa Darasa la Saba,
Kidato cha Nne na Kidato cha Sita kwa Mwaka 2018 mara baada ya kumaliza
hafla hiyo leo jijini Dodoma. Hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa
Shule ya Sekondari Wasichana Msalato na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali
wa sekta ya elimu.
(Picha na: Frank Shija –MAELEZO)
……………….
Na.Alex Mathias,Dodoma
Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia
Profesa Joyce Ndalichako, amesema serikali kupitia wizara ya elimu
inaendelea kuboresha miundombinu katika elimu, ili kuhakikisha
inaboresha sekta ya elimu hapa nchini.
Ameyasema hayo leo Jijini Dodoma katika
maadhimisho ya wiki ya elimu iliyoenda sambamba na kutoa tuzo kwa
wanafunzi waliofanya vizuri katika mitihani yao ya mwisho ya kumaliza
elimu ya Msingi na Sekondari hapa nchini tukio lililofanyika Shule ya
sekondari ya wasichana Msalato.
Amesema serikali inafanya jitihada kubwa
kuhakikisha inatoa elimu bora, ikiwamo kukarabati shule kongwe pamoja na
vyuo vya ngazi zote sambamba na kuweka usimamizi thabiti katika vyuo
ambayo vinazalisha walimu ili kupata walimu bora.
“Sisi kama serikali tunafanya jitihada
kubwa kuhakikisha elimu yetu inapanda, tunahakikisha shule zote kongwe
tunazikarabati angalau ziendane na hadhi ili watoto wetu wanasoma katika
mazingira mazuri tukiwa pia tunasimamia kikamilifu vyuo vyetu vizalishe
walimu ambao watatufikisha tunapotaka” amesema.
Katika sekta ya elimu ya ufundi amesema
serikali imetenga kiasi cha bilioni ishirini na mbili(22) kujenga chuo
cha veta katika mkoa wa Kagera ili kuinua sekta ya elimu ya ufundi
sambamba na kuvikarabati vyuo vya veta kote nchini pamoja na kujenga
vyuo vipya katika wilaya mbalimbali hapa nchini ili kuinua elimu ya
ufundi.
Katika elimu ya juu amesema serikali
imeboresha vyuo vikuu vyote na imejenga maktaba kubwa chuo kikuu cha Dar
es saalam, yenye uwezo wa kubeba wanafunzi wengi kwa wakati mmoja, pia
imetenga zaidi ya bilioni sita(6) kujenga hosteli katika chuo kikuu
cha Mzumbe itakayoondoa changamoto ya makazi kwa wanafunzi.
Amewataka wanafunzi kusoma kwa bidii na
kuacha uzembe, kwani serikali imekuwa ikifanya jitihada kubwa katika
kuboresha elimu, wao kama hawatafanya jitihada kusoma itakuwa kazi
bure.
“Niwaambie wanafunzi serikali hata
ikijenga magorofa au kuleta vitabu lori zima kama hamjitumi kusoma basi
ni kazi bure ninashoowaomba ni ninyi kujituma katika kusoma ili jitihada
hizi za serikali ziweze kuzaa matunda” amesema.
Kwa upande wake Mkurugenzi msaidizi wa
idara ya elimu kutoka TAMISEMI, Bi, Odilia Mushi, amevitaka vitengo
vyote ya elimu kutoka TAMISEMI kuhakikisha wanaimarisha malezi kwa
watoto ili waweze kupata matokeo mazuri.
Amesema tafiti mbalimbali zinaonyesha
kuwa ufaulu hapa nchini unaongezeka na umekuwa ukipanda mwaka baada ya
mwaka na kuwataka wasimamizi kuweka njia nzuri katika kuhakikisha ufaulu
unaongezeka zaid.
Katika tuzo hizo zimetolewa kwa wanafunzi
kumi (10) bora wa shule za msingi waliofanya vizuri mitihani yao ya
darasa la saba, katika ngazi hiyo wanafunzi hao wamepewa vyeti na fedha
kiasi cha laki tano(500,000) kila mmoja.
Kwa upande wa kidato cha nne wanafunzi
kumi bora katika ngazi hiyo wametuzwa vyeti na fedha kiasi cha milioni
moja(1,000,000) kila mmoja, kwa ngazi ya kidato cha sita waliwekwa
katika makundi matatu na kuwa na idadi ya wanafunzi tisa(9) ambapo kila
mmoja ametuzwa vyeti na fedha taslimu milioni moja na laki
tano(1,500,000).
Zawadi nyingine zimeenda kwa shule kumi
bora kwa kila ngazi na kutunukiwa vyeti kila shule, na shule zile
zilizoongeza ufaulu kutoka ngazi moja kwenda nyingine kwa kila ngazi
ikiwa ni shule za msingi na sekondari kidato cha nne na sita.
No comments:
Post a Comment