Na Mwandishi Wetu.
TIMU
ya soka ya taifa ya Tanzania imechapwa bao 1-0 na wenyeji, Misri katika
mchezo wa kirafiki leo Uwanja wa Borg El Arab mjini Alexandria.
Bao
pekee la wenyeji kwenye mchezo huo maalum kujiandaa na Fainali za Kombe
la Mataifa ya Afrika (AFCON) zinazotarajiwa kuanza Juni 21 hadi Julai
19 nchini Misri limefungwa na kiungo wa Aston Villa ya England, Ahmed El
Mohamady dakika ya 64 akimalizia pasi ya beki wa Pyramids ya nyumbani,
Ahmed Ayman Mansour.
Pamoja
na kufungwa, Taifa Stars inayofundishwa na Mnigeria, Emmanuel Amunike
ikiongozwa na Nahodha wake, mshambuliaji wa KRC Genk ya Ubelgiji, Mbwana
Samatta ilicheza vizuri – lakini ukweli tu ilizidiwa na Mafarao.
Kocha
Mmexico anayeinoa Misri aliwaacha benchi muda wote wa mchezo nyota wa
Ligi Kuu ya England, kiungo Mohamed Elneny wa Arsenal na mshambuliaji
Mohamed Salah wa Liverpool.
Taifa
Stars itacheza mechi zake tatu za Kundi C AFCON 2019 mfululizo dhidi ya
Senegal Juni 23, Kenya Juni 27 na Algeria Julai 1 kisha kuangalia
matokeo yake kama yataipeleka hatua ya mtoano.
Mbali
na Taifa Stars kupangwa Kundi C AFCON 2019 pamoja na jirani zao, Kenya,
Algeria na Senegal – wenyeji, Misri wapo Kundi A pamoja na na Zimbabwe,
Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Kundi
B linaundwa na Burundi, Madagascar, Guinea na Nigeria, Kundi D
linaundwa na Namibia, Afrika Kusini, Ivory Coast na Morocco, wakati
Kundi E kuna Angola, Mauritania, Mali na Tunisia na Kundi F ni Guinea
Bessau, Benin, Ghana na mabingwa watetezi, Cameroon.
Taifa
Stars imefuzu AFCON ya mwaka huu baada ya kumaliza nafasi ya pili
kwenye Kundi L kwa pointi zake nane, nyuma ya jirani zao wa Afrika
Mashariki, Uganda walioongoza kwa pointi zao 13 wakizipiku Lesotho
iliyomaliza na pointi sita na Cape Verde pointi tano.
Mwaka
huu, Tanzania itashiriki AFCON kwa mara ya pili tu kihistoria baada ya
mwaka 1980 nchini Nigeria ambako ilipangwa Kundi A pamoja na wenyeji,
Nigeria, Misri na Ivory Coast na kushika mkia.
Mwaka
1980 ilifungwa mechi mbili, 3-1 na Nigeria na 2-1 na Misri kabla ya
kutoa sare ya 1-1 na Ivory Coast na kuishia Raundi ya kwanza tu, wakati
timu nane tu zinashiriki michuano hiyo.
Michuano itaanza Juni 21 hadi Julai 19 na Taifa Stars itachezea mechi zake Uwanja wa Juni 30 na Al Salam mjini Cairo.
Na
katika CHAN, Taifa Stars itaanzia nyumbani dhidi ya Sudan Julai 26
kabla ya kurudiana Agosti 2 na ikifuzu mtihani huo itamenyana na mshindi
kati ya Kenya na Burundi.
Kikosi
cha Misri kilikuwa; Ahmed Al Shenawy/Mahmoud Gennesh dk46, Ahmed
Hegazi, Ayman Ashraf/Ahmed Ayman Mansour dk46, Mahmoud Alaa, Ahmed El
Mohamady, Abdalla El Said, Walid Soliman/Mahmoud Ibrahim Hassan
‘Trezeguet’ dk61, Tarek Hamed/Ali Ghazal, Amr Warda/Marwan Mohsen dk89,
Nabil Emad Dunga na Ahmed Ali/Ahmed Hassan Mahgoub ‘Koka’ dk46.
Tanzania;
Aishi Manula, Gardiel Michael, Hassan Kessy, Aggrey Morris/Ally Sonso
dk74, Kelvin Yondani, Himid Mao, Simon Msuva, Feisal Salum, John
Bocco/Thomas Ulimwengu dk62, Mbwana Samatta na Farid Mussa/Mohammed
Hussein ‘Tshabalala’ dk78
No comments:
Post a Comment