Naibu Waziri wa
Kilimo Mhe Omary Mgumba (Mb) akijibu swali bungeni leo tarehe 10 Juni 2019 wakati
wa mkutano wa kumi na tano wa Bunge la Bajeti Jijini Dodoma. (Picha Zote Na Mathias
Canal, Wizara ya Kilimo)
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba (Mb) akijibu swali bungeni leo tarehe 10 Juni 2019 wakati wa mkutano wa kumi na tano wa Bunge la Bajeti Jijini Dodoma.
Na Mathias Canal, Wizara ya
Kilimo-Dodoma
Serikali
imearifu kuwa inafanya utafiti na tathmini ya kina ya maji kujaa kwenye
mashamba ya wakulima katika maeneo mbalimbali nchini.
Naibu
Waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba ameyasema hayo Bungeni Jijini Dodoma leo tarehe
10 Juni 2019 wakati akijibu swali la Mhe Yahaya Omary Massare wa Jimbo la
Manyoni Magharibi aliyetaka kufahamu serikali ina mpango gani kuwasaidia
wananchi kwa kuwajengea mifereji ya kuongoza maji yasiingie mashambani.
Mbunge
huyo alisema kuwa Eneo la Mbuga linalozunguka Mji wa Itigi pamoja na kufaa kwa
kilimo cha mazao mbalimbali kama Mahindi, Alizeti, Choroko na Dengu lakini eneo
hili linajaa maji na kufanya kilimo kuwa kigumu.
Mhe
Mgumba aliongeza kuwa Utafiti na tathmini hiyo itakapokamilika itakuja na
mikakati na mapendekezo stahiki yatakayosaidia kutatua changamoto ya kujaa maji
mashambani na kuwasaidia wakulima wa
eneo la mbuga linalozunguka mji wa Itigi ili kuongeza uzalishaji na tija.
Aliongeza
kuwa eneo la mbuga linalozunguka mji
wa Itigi limekuwa likijaa maji pale mvua zinapokuwa juu ya wastani ambapo historia
inaonesha kuwa bonde hili lilijaa maji kipindi cha mwaka 1997/1998 wakati wa mvua
za E-lnino na katika msimu wa
2015/2016 baada ya miaka tisa tangu wakati wa mvua za E-lnino mwaka 1997/98.
Aidha, alisema kuwa Serikali imelichukua
suala la Mheshimiwa Mbunge na itatuma wataalam wa Kilimo na Tume ya Umwagiliaji
kwa ajili ya kwenda kufanya utafiti na tathmini ya kina ya maji kujaa kwenye
mashamba ya wakulima.
Utafiti
na tathmini hiyo itakapokamilika itakuja na mikakati na mapendekezo stahiki
yatakayosaidia kutatua changamoto ya kujaa maji mashambani na kuwasaidia wakulima wa eneo la mbuga linalozunguka mji
wa Itigi ili kuongeza uzalishaji na tija.
MWISHO
No comments:
Post a Comment